MTWARA: Wanafunzi 9 wakamatwa kwa kuhamasisha maandamano kupitia WhatsApp na Telegram

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linawashikilia wanafunzi 9 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba, wakituhumiwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwamo WhatsApp na Telegram kuhamasisha maandamano.


IKUMBUKWE KUWA: Mnamo mwezi Machi mwaka huu, Rais Dkt. John Magufuli aliwaonya vikali watu wanaopanga kufanya maandamano nchini akisema kwamba hawataruhusiwa.

"Wapo watu wangependa nchi hii kila siku tuwe na migogoro," alisema Dkt Magufuli.

"Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli, wangependa kila siku tuko barabarani tunaandamana. Watu wao wanahamia huku, wao wanataka wabaki wanaandamana kule.

Nitasema ngoja waandamane wataniona. Kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri."

"Niliapa kwa katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani."
 
Jamani mambo sasa alikwishasema maandamano ya kwenye mtandao hana shida nayo......hebu waachieni hao watoto waendelee na masomo.
 
Huu upuuzi Jeshi la Polisi badala kupambana na mambo yenye faida kwa Taifa wanahangaika na watu wanaomkosoa Raisi .Mungu mwenyewe wapo wanaomkosoa sembuse mwanadamu huu ujinga
 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, linawashikilia wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba kwa tuhuma za kumkashifu Rais John Magufuli na kuhamasisha maandamano ya Aprili 26.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp na Telegram kumkashifu Rais na kuhamasisha maandamano hayo.

Kamanda Mkondya bila kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa madai ya sababu za kiupelelezi, alisema daktari huyo ni kutoka Halmashauri ya mji wa Nanyamba.

“Ninatoa onyo watu wajiepusha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kusababisha uvunjifu wa sheria za nchi. Watuhumiwa wote tunawashikilia kwa upelelezi zaidi,” alisema.

Katika tukio lingine, Kamanda Mkondya alisema wanawashikilia wahamiaji haramu 23 waliokutwa katika nyumba ya kulala wageni eneo la Chikongola, Wilaya ya Mtwara.

“Wahamiaji hawa wanatoka nchi tatu tofauti, 13 kutoka nchi ya Demokrasia ya Congo, saba kutoka Rwanda na wawili kutoka Burundi, katika mahojiano wamesema walikuwa wakielekea Ufaransa kwa kupitia visiwa vya Comoro,” alisema.


Pia alisema wanawashikilia watu 13 ambao wanajihusisha na mtandao wa wizi wa pikipiki katika kijiji cha Chikongo, wilayani Tandahimba.

Kamanda Mkondya alidai kuwa mtandao wa wezi hao unaongozwa na Mohamed Juma (simba).

Muungwana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom