Mtwara: Uhaba wa Maji Wawalazimu Wagonjwa kufua Mashuka ya Hospitali

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,021
1,608
Changamoto ya upatkanaji wa maji katika Kijiji cha Chihangu, kilichopo wilayani Newala, imesababisha wagonjwa wanaotibiwa katika Kituo cha afya Chihangu kutakiwa kufua nguo za hospitali kabla ya kuruhusiwa

Mtwara. Changamoto ya upatkanaji wa maji katika Kijiji cha Chihangu, kilichopo wilayani Newala, imesababisha wagonjwa wanaotibiwa katika Kituo cha afya Chihangu kutakiwa kufua nguo za hospitali kabla ya kuruhusiwa.

Mkazi wa Kijiji cha Kihangu B, Musa Kajana alisema kuwa shida ya maji imewafanya wagonjwa wanaporuhusiwa baada ya kulazwa wakafue wenyewe nguo, ili waziache hospitalini hapo zikiwa safi. “Huwezi kuruhusiwa hapa mpaka ufue shuka kwa kutumia maji yako, uzirudishe shuka zikiwa safi ili zitumiwe na mgonjwa mwingine.

Baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakikataa kutumia shuka za hapa kwa sababu ya uchafu unaotokana na uhaba wa maji na ndiyo maana ukitibiwa kabla hujatoka unatakiwa uzifue ili zitumiwe na mwingine,” alisema Kajana, kwenye hafla ya kupokea mashuka 100, vitanda 10 na magorodo 10 vyenye thamani ya Sh7 milioni vilivyotolewa na Benki ya NMB wilayani Newala.

Alifafanua kuwa wanaopata shida sana katika kituo ni kina mama wanaojifungua kutokana na ukosefu wa maji kijijini na hospitalini hapo.

“Shida shuka chache zinalaliwa na idadi kubwa ya wagonjwa, na kutokana na ukame wa maji hazifuliwi, zina kunguni, wadudu kuwasha, unaporuhusiwa unaondoka na homa nyingine kama vipele,” alisema mkazi wa Kijiji cha Kihangu B, Maria Goreth

Akilizungumzia hilo, Mkuu wa kituo hicho, Dk Anthony Rioba alisema kuwa wakati wa changamoto ya maji waliwaomba wagonjwa, hususan waliofanyiwa upasuaji, kusuuza nguo za hospitali ambazo zinakuwa zimechafuka damu na uchafu mwingine kisha wao hospitali huzifua kwenye mashine na dawa.

Alisema mahitaji ya maji ni makubwa, hasa katika shughuli za upasuaji, usafi wa wodi, wagonjwa wenyewe lakini kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wake.
Alisema kabla ya msaada huo walikuwa na mashuka 47, huku mahitaji yakiwa ni 200.

Chanzo: Mwananchi
 
Alafu kina Bashiru wakiongea yanatokea mataahira kama kina fatuma kumpinga
 
Back
Top Bottom