Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,012
- 95,356
Wajinga ndio waliwaoHakika upumbavu umewapata wapumbavu...
Wajinga ndio waliwaoHakika upumbavu umewapata wapumbavu...
Hahahah rejea ya semunge na grandpa wa taifaApo chacha,,, mkuu mpk nikahoji ndo mila za uku zilivyo.... Maana umasaini havipo vitu HV ..
Hakuna kitu kama Hiko mbagalaUkitaka kupima kiwango cha ujinga wa jamii yako na ubora wa elimu kwa watu ktk jamii yako basi angalia mwitikio ktk habari za uzushi na ujinga kama hizi. Huku mbagala ni balaa watu wanahaha kutafuta unga wa muhogo. Karne hii bado tunaamini ktk abracadabra
Kunywa tu, hata wangesema kinyesi cha nguruwe/ cha binaadam we kula tu,Ningekuwa huko ningekunywa uji pia, mambo ya kuleta ujuaji haya eti elimu, elimu elimu ni upuuzi nakunywa zangu nalala fresh ikija sawa isipo kuja pia sawa
Kweli wajinga ndio waliwao.Huyo mtoto ana roho mchafu na roho huyo nia yake ni kuleta tu hofu kwa watu,nothing will happen.Tusisahau kwamba Shetani ni mwongo na baba wa uongo.View attachment 672395
Waungwana kuna tetesi zinaenea kwa kasi kwamba, ktk nchi ya Msumbiji kijiji cha Nangadi, Jana tarehe 9 saa tano usiku amezaliwa mtoto.
Baada tu ya kuzaliwa amefumbua macho na kuweza kuongea. Mtoto amesema ktk eneo la Tandahimba mkoa wa Mtwara Tanzania, kutanyesha mvua isiyokua ya kawaida na mvua hiyo itaambatana na wadudu, hao wadudu wakikung'ata tu, wewe na familia yako yote mnakufa mmoja mmoja.
Mtoto akatoa na suluhisho kwa kuwaelekeza namna ya kujikinga na janga hilo. Amesema kinga yake ni kupika uji wa muhogo na unywe.
View attachment 672394
Hivi tunavyozungumza Tandahimba na vijiji vyake usiku kucha leo wamekesha wakikoroga uji wa muhogo, maana taarifa ilikolea zaidi baada ya baadhi ya misikiti kuwatangazia kufanya hivyo wananchi wakati wakiadhin sala ya alfajiri.
Sasa Mimi naamini Jf ni familia pana zaidi halishindikani jambo, kama kuna mtu mwenye info zaidi ya hapa atutosheleze.
Asante.
View attachment 672435 View attachment 672436 View attachment 672437
=====
Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Mtwara na maeneo mengine ya mikoa ya jirani wamejikuta wakikesha nje ya nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji utokanao na unga wa muhogo.
Wakazi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza.
Imedaiwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.
Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu ukweli wa jambo hilo, watu waliendelea kuamshana usiku wa manane kunywa uji huo.
Chanzo: Azam