Mtwara: Taharuki Tandahimba baada ya madai ya mtoto mchanga kutabiri mvua ya ajabu; wakesha wakinywa uji wa Muhogo

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,368
2,000
Shubamittt!!
Wazungu wanakuna vichwa kwenda angani sisi tunakesha nje kunywa uji wa muhogo
 

kauga JR

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
3,512
2,000
Hizo habari ni kama babu wa yuleee aliyepiga pesa
Biashara ya mihogo ilidoda/ ilikosa soko, so watapataje soko lazima watengeneze SCENE, mm nipo huku mvua ni za kawaida sana.
 

shiu yang

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
3,294
2,000
FB_IMG_1515572709785.jpg

Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Mtwara na maeneo mengine ya mikoa ya jirani wamejikuta wakikesha nje ya nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji utokanao na unga wa muhogo.

Wakazi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza.

Imedaiwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.

Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu ukweli wa jambo hilo, watu waliendelea kuamshana usiku wa manane kunywa uji huo.

chanzo;Priority10News


Watakuwa wamekunywa wengi ndio maana haijanyesha
 

mkandu

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
225
500
Kama kuna Wakristo walikunywa huo uji basi hao ni wale ambao "imani" yao ni haba. Siyo Wakristo wote wanaimani thabiti.
Naona kwa jinsi ulivyojieleza naamink hata ww ungekuwepo ungekuwa mmoja wapo wa wanywaji kwa kuwa unaonekana ni mtu ambae hauishughulishi fikra yako.
Ulichojibia kimetafsiri uwezo wako kifkra labda nikujuze tu mm niko huku Mtwara na sijanywa kwa imani yangu ya kiislam ila wapo wengi walokunywa na hii ni kwa sababu ya elimu ndogo wakizokuwa nazo na wengine imani ndogo ni km wale walokaenda Loliondo kwa mchungaji au wale walokalishwa nyasi na mchungaji kwa kuaminishwa ni dawa hawa wote ni uchache wa elimu na wengine imani ndogo tukienda matendo ya kishirikina huwezi kufananisha Ukanda wa pwani na huko kwingine tumia minzani ya mauaji ya Albino, mauaji ya vikongwe na kukatana sehemu za siri ukiipata takwimu yake sidhani km utakuja kunasibisha ukanda wa pwani na sehemu nyingine kiustaraabu wa kiimani.
Mkoa unaoongoza kwa makanisa Tz mkoa wa Mbeya ndio ulokashika nafasi ya kwanza kwa mwaka wa 2015-2016 cjajua mwaka jana ilikua nafasi gani ila kwa maelezo ya polisi walisema matukio mengi yamehusishwa na imani hzo za kishirikina.
Kuna wimbi la watumishi na wadandaji wakifika ukanda wa pwani huwa wanahamia moja kwa moja kwa kushawushiwa tu na ustaraabu wa watu wake ukanda huu ubaguzi ni nadra sio km kwa wenzetu tumeishi huko na tumejionea.
Nimejaribu kukuweka sawa mkuu.
 

Kiteitei

JF-Expert Member
Jan 14, 2009
1,517
2,000
huu ubunifu safi sana,lazima tuuze mihogo yetu tena kwa bei ya juu,maana sio mihogo tuuu bali ni kifoproof!!
 

KISHANDU

Member
Mar 11, 2017
22
75
Mimi nipo huku Tandaimba kikazi, hata hapa kwenye guest house tuliyofikia walituamsha wenyeji, eti na sisi tunywe uji tujikinge na balaa hilo
 

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,907
2,000
Ni Kweli nilishuhudia kwa macho yangu wanaamshana kunywa uji nikaona ni upuuzi tu na imani za kishirikina zimewatawala
 

tofali

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
4,011
2,000
Yale yale...BABU WA LOLIONDO
Tarajieni mihogo kupanda bei km sio kuadimika...
Wat a marketing strategy
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom