Mtwara: Taharuki Tandahimba baada ya madai ya mtoto mchanga kutabiri mvua ya ajabu; wakesha wakinywa uji wa Muhogo

Ukitaka kupima kiwango cha ujinga wa jamii yako na ubora wa elimu kwa watu ktk jamii yako basi angalia mwitikio ktk habari za uzushi na ujinga kama hizi. Huku mbagala ni balaa watu wanahaha kutafuta unga wa muhogo. Karne hii bado tunaamini ktk abracadabra
 
huo ni uzushi tu.... hauna tofauti na ule uzushi uliotungwa miaka iliyopita mbagala/kongowe kwamba mtoto alikojolea Quruan... matokeo yake ni uvunjifu wa amani na taharuki ktk jamii

raia wanapaswa kuchunguza chanzo cha habari na kujua tofauti ya uzushi na taarifa rasmi inatolewa na nani..
 
Hivi sisi Waafrika tuna laana?!
Yaani mtu mzima na akiri zake anaamini uzushi+upuuzi kama huu! Watu wanatimkia Anga za juu sisi tunawaza mazingaombwe haya na ushirikina. Tutaendelea lini
 
Wakulima wa muhogo are very smart

Wamecreate demand kiulaiiini and now wanapiga pesa kinyama

Smart move.Not all rumors are spred by idiots and believed by fools.Some rumours are spred by smart people
 
Nimecheka sana hii habari,kuna mtu anataka kuuza dawa tu,ama huyo jamaa alikuwa na stock kubwa sasa wanatengeneza namna ya kuitoa. Kweli vyuma sio mchezo.

Tuko pamoja mkuu. Pia kuna habari hapa Dar kuwa baada ya watu wengi kukimbilia kwenye MIHOGO na Pweza kutibu ule ugonjwa.. Eti jamaa kapewa FEZA na watu wa viwanda vya viagra ili atoe utafiti kuonya juu ya kula mihogo mibichi. Nasikia tahadhari ya Pweza iko jikoni itatoka hivi karibuni
 
Usiku huu watu wanasonga uji wa muhogo na kunywa.
Eti kuna mtu anasambaza taarifa kuwa kuna mtoto amezaliwa Nangadi Msumbiji na akasema kuwa kutakuwa na mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali ambao utaleta madhara na upele hivyo dawa yake ni kusonga uji wa muhogo na kunywa tena nje uani.
My take: Huu ni uzushi tena katika Uislamu ni Shirk juu ya uwezo wa Allah, aliyetengeneza uzushi huo anapaswa kukamatwa na kushtakiwa



Mtoto azaliwe msumbiji na uju unywewe Tandahimba

Niwakumbushe tu kuwa "Msiogope mahali mlipo, wala msiwafuate, kamwe msiwafuate, kama umeme umulikavyo upande huu wa nchi hata mwingine, ndivyo atakavyokuja mwana wa Adamu katika siku yake"
 
Hahaa nimesikia mtwara ni moja ya sehemu wanayolima mihogo kwa wingi sana, sasa baada ya korosho kuwekewa soko zuri bidhaa za mhogo zinakosa soko, hii ni trick tu bwana.. watu wale mhogo unaodorola masokoni
 
Hiki ni kipimo tosha kwa jamii yetu, JAMII YETU KWA KIASI KIKUBWA BADO NI PRIMITIVE, huhitaji kufanya tafiti katika mazingira kama haya, SERIKALI NI VYEMA IKAJIFUNZA HAPA NA KUIJUA JAMII YAKE IPO WAPI MPAKA SASA..
 
Ukitaka kupima kiwango cha ujinga wa jamii yako na ubora wa elimu kwa watu ktk jamii yako basi angalia mwitikio ktk habari za uzushi na ujinga kama hizi. Huku mbagala ni balaa watu wanahaha kutafuta unga wa muhogo. Karne hii bado tunaamini ktk abracadabra
Adi Tanzania mbagala zimefika
 
Kama umewahi kufika maeneo ya kusini huko wala hutoshangaa habari km hii maana watu wanaamini sn imani za kishirikina huko
 
kwa ambao hamfahamu pwani ya kusini mwa Tanzania na majirani zake ushirikina sehemu ya maisha ya kila siku yaani kila baada ya nyumba moja utakuta mganga...mambo ya ngoma za kishetani na ulozi ni vitu vya kawaida sana yaani mfano Arusha watu wanaficha sana hirizi huku hata waheshimiwa zinavaliwa hasharani bila shida...binafsi nimeona usiku wa kuamkia leo watu hajalala ni kunywa uji wa muhogo..kwa wageni imetupa mshangao sana....kati ya vyanzo vya umasikini pande hizi ni ushirikina
 
Ats kama angetabili Mimi ninamsikia nisingeweza kukubari Kunywa uwo uji wa muhogo...
Wanaokynywa uji wa muhogo ni wale wasiyomuogopa Allah.
 
Back
Top Bottom