Mtwara: Taharuki Tandahimba baada ya madai ya mtoto mchanga kutabiri mvua ya ajabu; wakesha wakinywa uji wa Muhogo

Uongo ukiongelewa mara nyingi binadamu huamini ni ukweli.Wajinga ndio waliwao
 
Inasadikika kuwa Msumbiji wana siku yao ya wajinga.Sasa hawa ndugu zetu wa pale mpakani huwa wanaenda kupata mahitaji yao huko wakati mwingine.Walipokutana na huo uzushi wakaubeba kama ulivyo na kama ujuavyo habari za majanga husambaa haraka nao wakasambaziana na wengine kufikia kupigia simu ndugu zao walio nje ya Mtwara na Lindi.Ila na nyie watani zangu mvua na uji wa muhogo wapi na wapi?Tena uji wenyewe usiwe na sukari wala chumvi unaunywaje!!Hakuna cha mtoto wala mdoli yote ni kushindwa kujiuliza maswali ya msingi kabla ya kuchukua hatua.Kwani jee bwana wewe ule unga wa nhogo kufanya kuumaliza kwene uji!?ntalala njaa
 
Ukitaka kupima kiwango cha ujinga wa jamii yako na ubora wa elimu kwa watu ktk jamii yako basi angalia mwitikio ktk habari za uzushi na ujinga kama hizi. Huku mbagala ni balaa watu wanahaha kutafuta unga wa muhogo. Karne hii bado tunaamini ktk abracadabra
Hakuna kitu kama Hiko mbagala
 
Maeneo hayo % kubwa watu wake hawana elimu zaidi ya kuamini ktk ushirikina tu, bado elimu inahitajika sn hayo maeneo, vp kama huyo mtoto mtabiri angewaambia wasivae mavazi yoyote yale kama kinga ya janga hilo ? Shabash!!
 
View attachment 672395
Waungwana kuna tetesi zinaenea kwa kasi kwamba, ktk nchi ya Msumbiji kijiji cha Nangadi, Jana tarehe 9 saa tano usiku amezaliwa mtoto.

Baada tu ya kuzaliwa amefumbua macho na kuweza kuongea. Mtoto amesema ktk eneo la Tandahimba mkoa wa Mtwara Tanzania, kutanyesha mvua isiyokua ya kawaida na mvua hiyo itaambatana na wadudu, hao wadudu wakikung'ata tu, wewe na familia yako yote mnakufa mmoja mmoja.

Mtoto akatoa na suluhisho kwa kuwaelekeza namna ya kujikinga na janga hilo. Amesema kinga yake ni kupika uji wa muhogo na unywe.
View attachment 672394
Hivi tunavyozungumza Tandahimba na vijiji vyake usiku kucha leo wamekesha wakikoroga uji wa muhogo, maana taarifa ilikolea zaidi baada ya baadhi ya misikiti kuwatangazia kufanya hivyo wananchi wakati wakiadhin sala ya alfajiri.

Sasa Mimi naamini Jf ni familia pana zaidi halishindikani jambo, kama kuna mtu mwenye info zaidi ya hapa atutosheleze.
Asante.
View attachment 672435 View attachment 672436 View attachment 672437
=====

Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Mtwara na maeneo mengine ya mikoa ya jirani wamejikuta wakikesha nje ya nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji utokanao na unga wa muhogo.

Wakazi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza.

Imedaiwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.

Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu ukweli wa jambo hilo, watu waliendelea kuamshana usiku wa manane kunywa uji huo.

Chanzo: Azam
Kweli wajinga ndio waliwao.Huyo mtoto ana roho mchafu na roho huyo nia yake ni kuleta tu hofu kwa watu,nothing will happen.Tusisahau kwamba Shetani ni mwongo na baba wa uongo.

Hata hivyo dah,badala ya watu kumwomba Mungu awaepushe na hilo janga kama kweli lipo,which is not true anyway, wanaamua kumtii roho mchafu na kufakamia miuji.Noma sana.Hivi pepo mchafu atakupaje tiba?Ridiculous.
 
Back
Top Bottom