Mtwara: Taharuki Tandahimba baada ya madai ya mtoto mchanga kutabiri mvua ya ajabu; wakesha wakinywa uji wa Muhogo

kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,655
2,000
uji1.jpg

Waungwana kuna tetesi zinaenea kwa kasi kwamba, ktk nchi ya Msumbiji kijiji cha Nangadi, Jana tarehe 9 saa tano usiku amezaliwa mtoto.

Baada tu ya kuzaliwa amefumbua macho na kuweza kuongea. Mtoto amesema ktk eneo la Tandahimba mkoa wa Mtwara Tanzania, kutanyesha mvua isiyokua ya kawaida na mvua hiyo itaambatana na wadudu, hao wadudu wakikung'ata tu, wewe na familia yako yote mnakufa mmoja mmoja.

Mtoto akatoa na suluhisho kwa kuwaelekeza namna ya kujikinga na janga hilo. Amesema kinga yake ni kupika uji wa muhogo na unywe.
uji.jpg

Hivi tunavyozungumza Tandahimba na vijiji vyake usiku kucha leo wamekesha wakikoroga uji wa muhogo, maana taarifa ilikolea zaidi baada ya baadhi ya misikiti kuwatangazia kufanya hivyo wananchi wakati wakiadhin sala ya alfajiri.

Sasa Mimi naamini Jf ni familia pana zaidi halishindikani jambo, kama kuna mtu mwenye info zaidi ya hapa atutosheleze.
Asante.
ujii.jpg
ujii2.jpg
ujii3.jpg

=====

Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Mtwara na maeneo mengine ya mikoa ya jirani wamejikuta wakikesha nje ya nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji utokanao na unga wa muhogo.

Wakazi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza.

Imedaiwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.

Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu ukweli wa jambo hilo, watu waliendelea kuamshana usiku wa manane kunywa uji huo.

Chanzo: Azam
 

Balungi

JF-Expert Member
May 25, 2011
219
250
Usiku huu watu wanasonga uji wa muhogo na kunywa.
Eti kuna mtu anasambaza taarifa kuwa kuna mtoto amezaliwa Nangadi Msumbiji na akasema kuwa kutakuwa na mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali ambao utaleta madhara na upele hivyo dawa yake ni kusonga uji wa muhogo na kunywa tena nje uani.
My take: Huu ni uzushi tena katika Uislamu ni Shirk juu ya uwezo wa Allah, aliyetengeneza uzushi huo anapaswa kukamatwa na kushtakiwa
 

patricl

JF-Expert Member
Oct 2, 2015
426
250
Usiku huu watu wanasonga uji wa muhogo na kunywa.
Eti kuna mtu anasambaza taarifa kuwa kuna mtoto amezaliwa Nangadi Msumbiji na akasema kuwa kutakuwa na mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali ambao utaleta madhara na upele hivyo dawa yake ni kusonga uji wa muhogo na kunywa tena nje uani.
My take: Huu ni uzushi tena katika Uislamu ni Shirk juu ya uwezo wa Allah, aliyetengeneza uzushi huo anapaswa kukamatwa na kushtakiwa
Mbona mimi nimesikia uji upikiwe barazani, katikati ya n'lango...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom