Mtwara: Mwalimu mmoja afundisha darasa la kwanza hadi la saba

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Fikiria shule nzima ina mwalimu mmoja anayefundisha madarasa sita. Ndiye mwalimu wa wanafunzi wote 99. Ndiye mwalimu wa darasa la awali (chechekea). Anapanga vipindi na kusimamia taaluma na nidhamu.

Si hivyo tu, lakini mwalimu huyu na wanafunzi wake wanatumia chumba kimoja cha darasa.

Penye nia hapakosi njia, Bosco Chilumba ameamua kufanya peke yake kazi zinazopaswa kufanywa na walimu wengi katika shule hiyo ya msingi Chikotwa iliyopo wilayani Nanyumbu yenye darasa la awali hadi la tano.

Licha ya changamoto hizo, mwalimu huyo amefanikiwa kuwa na rekodi nzuri ya ufundishaji kwani wanafunzi wake kuanzia darasa la pili hadi la tano wanajua kusoma kasoro wawili wa darasa la pili na mmoja wa darasa la tatu ambao wanasoma kwa ‘kuungaunga’ maneno.

Si hivyo tu hata kwa matokeo ya mtihani wa darasa la nne mwaka huu wanafunzi wote wa shule hiyo wamefaulu na kuingia darasa la tano.

Chilumba (33) aliyehamia katika shule hiyo tangu mwaka 2015, aliikuta ikiwa na wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili, na mengine yote ameanza nayo mwenyewe.

“Mwanzo nilikuwa nawaweka wanafunzi wote darasani (wa awali hadi darasa la tano), baadaye nikaona inakuwa usumbufu kwa sababu ukifundisha darasa hili wengine wanapiga kelele inakuwa ni bughudha, lakini mfumo wa sasa wanaingia darasa mojamoja,” anasema Chilumba akimaanisha kwamba wanabadilishana kwa zamu.

“Katika ufanyaji kazi wangu madarasa ambayo nayapa kipaumbele zaidi ni la kwanza na pili ili wajue kusoma na darasa la nne nawapa kipaumbele kwa sababu wanakuwa na mtihani wa kitaifa.”

Anasema kutokana na kuwa peke yake na wingi wa majukumu hawezi kufuatilia ratiba ya masomo vizuri na kuitekeleza kama inavyotakiwa kutokana na kufundisha wanafunzi wote.

“Namna ya kuwafikia vizuri ni ngumu kwani niko peke yangu, kama mwalimu mkuu wakati mwingine kuna taarifa mbalimbali natakiwa kupeleka ofisini halmashauri (ya wilaya),” anasema. Mwalimu huyo anasema kuna wakati wanafunzi wake humaliza wiki bila kumuona shuleni na hivyo kwa kipindi chote kutofundishwa chochote.

“(Lakini) wakati mwingine ninapotoka wakiwa shuleni namuomba mwenyekiti wa kamati ya wazazi awaangalie kwa sababu za kiusalama,” anasema.

“Lakini naendelea kufanya kazi kwa sababu ni ajira yangu na ninaipenda, kwa hiyo sikuona shaka kuendelea kuishi katika mazingira haya na nashukuru Mungu anasaidia watoto wanajua kusoma vizuri licha ya kuwa niko peke yangu.”

Licha ya kutokuwapo kwa vyumba vingi vya madarasa, mwalimu huyo pia hana nyumba ya kuishi shuleni, akiwa anaishi katika nyumba ya kupanga.

“Katika nyumba ambayo naishi tayari nimepewa notisi natakiwa kuikabidhi ifikapo mwezi wa tano, hili kidogo linanipa wakati mgumu kutokana na mazingira ya hapa kama unavyoona,”anasema mwalimu Chilumba ambaye katika taaluma ya ualimu alisomea masomo ya sayansi.

Anasema kutokana na kukosekana nyumba anadhani ndio sababu ya Serikali kushindwa kupeleka walimu wengine katika shule hiyo.

Wasifu
Mwalimu Chilumba ni mwenyeji wa Masasi mkoani hapa aliyepata elimu yake ya msingi katika Shule ya Chiwale na Sekondari ya Lukuledi wilayani humo, kisha alijiunga na Chuo cha Ualimu Nachingwea mkoani Lindi na kuajiriwa mwaka 2009. Chilumba ana mke na watoto watatu, wawili ni pacha wanaosoma darasa la kwanza wilayani Masasi na mwingine darasa la awali katika Shule ya Chikotwa anakofundishwa na baba yake.

“Kwa hapa kijijini niko na mke wangu na mtoto wangu mdogo ambaye ni mmoja wa wanafunzi wangu wa darasa la awali na wengine (pacha) wako kwa bibi yao Masasi wanasoma darasa la kwanza ,”anasema Chilumba.

Anasema wakati anakwenda kuripoti shuleni hapo, alilazimika kutumia usafiri wa trekta kumfikisha katika kitongoji hicho pamoja na mizigo yake, kutokana na hali ya miundombinu ambayo ilikuwa vigumu kwa magari mengine kuweza kufika eneo hilo.

“Ikalazimika itumike trekta (kunileta), lakini nayo ilikwama ikalazimika kushusha vyombo na wananchi kuvibeba kichwani hadi nyumbani.”

Uongozi unasemaje?
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Hamis Dammbaya anasema walikuwa na mpango wa kuongeza walimu watatu katika shule hiyo Januari, lakini mazingira hayaruhusu hadi watakapokamilisha ujenzi wa nyumba za walimu.

“Lazima kwanza tuhakikishe tunakuwa na nyumba za walimu kisha tunapeleka walimu wakati tunaendelea na utaratibu wa madarasa,” alisema Dammbaya.

“Huwezi ukapeleka mwalimu Chikotwa kitongoji ambacho kwanza kina watu wachache, lakini pili hawana miundombinu ambayo unaiona unaweza kupeleka walimu wakaishi.”

Kuhusu suala la makazi endapo wataongezewa walimu, mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Hamis Burian anasema, “ofisi ya chama (CCM) hiyo hapo, walishatoa hilo jengo ili mwalimu mwingine aongezeke.”

Akizungumzia ujenzi wa madarasa, mwenyekiti wa kitongoji cha Chikotwa, Kassim Mohamed anasema tangu 2017 wanaendelea kuchangishana kila kaya Sh10,000 kwa ajili ya kununua saruji na tayari wamefyatua sehemu ya matofali yanayotakiwa.

Mkazi wa kitongoji hicho, Rashid Hassan anasema hawapendezwi na mazingira ya shule hiyo, lakini wamekwama kiuchumi kutokana na mazao mchanganyiko wanayotegemea kukosa soko la uhakika, huku akiwaomba wasamaria wema kuwasaidia.

MIKAKATI YA SERIKALI
Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Moses Machali anasema: “Tunapojen-ga kwa maana ya Serikali na wanan-chi tunapaswa kushirikiana.”Anasema Shule ya Chikotwa ime-kuwa iko hivyo kutokana na mwamko mdogo wa wananchi, lakini ipo mipango ya kutaka kujenga madarasa na nyumba za walimu.

Kuhusu mwalimu mmoja kufundi-sha peke yake shuleni hapo, anasema Idara ya Elimu imekuwa ikipanga walimu kutegemeana na mahitaji ya shule au kijiji husika.Anasema inawezekana halmashauri imeona kulingana na idadi ya wana-funzi katika shule hiyo pengine mwalimu mmoja anakidhi kuwahudu-mia wanafunzi.Hata hivyo, anasema ipo haja ya kupeleka mwalimu mwingine ili inapo-tokea dharura kwa aliyepo wanafunzi wasome.

“Natoa wito kwa mkurugenzi mtendaji kupitia Idara ya Elimu Msingi kuhakikisha wanapeleka mwalimu mwingine na tumeshazungumza, na nasisitiza hili kama bado kwa sababu nilishawapa maelekezo,” anasema Machali.Akizungumzia shule hiyo ilivyoanza, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Hamis Dammbaya anasema wazazi wengi wana utaratibu wa kuhama kutoka kijiji kimoja kwenda kingine kwa ajili ya kutafuta masham-ba.

“Shule ya Chikotwa asili yake ni moja ya kata ya Nanyumbu sasa wazazi wakahama kutoka kitongoji cha Nanyumbu na Chungu zilipo shule ambazo Serikali ilizijenga na kuweka miundombinu yote, wakaenda Chikot-wa kwa ajili ya kutafuta maeneo ya kulima,” anasema Dammbaya.“Walipofika pale walijenga darasa lao moja wakasema ni maalumu kwa ajili ya watoto ambao umri wao ni mdogo, ili wakishakua wahamie katika shule mama.”Anasema,

“Kwa hiyo baada ya kui-fungua kama shule shikizi wakaomba usajili na miaka ya nyuma hakukuwa na utamaduni wa kukagua shule kabla ya kuona kama inajitosheleza na hivyo kusababisha isajiliwe bila utaratibu kufuatwa.”“Baada ya kuifungua ikaanza darasa la kwanza, la pili, kwa hiyo wataalamu wanakuja kushtuka shule kumbe ina darasa moja kwa madarasa mengine hakuna, na tulikutana na shule nyingi za aina hiyo.”

“Sasa tumeweza kurekebisha zaidi ya shule 53, lakini zaidi ya shule 43 tulizikuta watoto wanasoma chini ya mikorosho na hatujamaliza ikiwemo Chikotwa kwa sababu si kazi rahisi.” anasema mkurugenzi huyo.Dammbaya anasema halmashauri hiyo imetenga zaidi ya 125 milioni kwa ajili ya kufanya maboresho katika shule za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
asilimia hata 10 ya kununua ndege na kujengea madaraja, tafadhali wamuwezeshe
 
Mwalimu Bosco Chilumba wa shule ya Msingi Chikotwa Wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara anafundisha madarasa 6 peke yake, akiwa ni mwalimu pekee wa shule hiyo.

#Pichani Mwalimu Bosco Chilumba Akiwa Darasani Anafundisha.

#ElimuBure
FB_IMG_1552302580833.jpg
 
Msiseme kwenye mitandao. Mtwangie waziri simu agizo la Raisi
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Weye sio mzalendo kabisa. Hivi unawezaje kuisema vibaya nchi yako kwenye mitandao?? Tena ukaweka na picha? Nadhani umetumwa na Chadema wewe
 
IMG-20190311-WA0059.jpg

Ni mwalimu Bosco Chilumba wa Shule Ya Msingi Chikotwa Iliyopo Wilaya Ya Nanyumbu

Mwalimu huyo amelazimika kufundisha masomo yote kinyume na kanuni za taaluma ya ualimu
 
Back
Top Bottom