Mtwara: Madiwani wa Mji Masasi wadai malipo ya Korosho yamechochea biashara ya ngono

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Messages
200
Points
250

Suley2019

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2019
200 250
Malipo ya Korosho kwa wakulima wilayani Masasi Mkoani Mtwara yametajwa kuwa ni chanzo cha ongezeko la uwepo wa kina dada wanaofanya biashara ya ngono wilayani humo ili kujipatia fedha hizo za korosho.

Hayo yalisemwa jana wilayani Masasi na Madiwani wa halmashauri ya mji Masasi walipokuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kikao cha baraza la Madiwani.

Walisema katika wilaya ya Masasi hivi sasa kumekuwa na makundi mbalimbali ya wasichana kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania ambao wanafanya biashara ya ngono.

Diwani wa kata ya Mkuti, Hamza Machuma alisema kata yake ya Mkuti kuna makundi ya wasichana ambao wamekodi vyumba mitaani na biashara yao kubwa ni biashara ya ngono.

Alisema wasichana hawa mara nyingi wamekuwa wakionekana hasa katika kipindi cha misimu ya mauzo ya zao la korosho kwa vile wanafahamu kipindi hiki wakulima wanapata fedha za zao hilo.

"Tunaomba hatua zichukuliwe dhidi ya makundi haya kwani biashara inayofanyika na hawa wadada sio rasmi," alisema Machuma

Naye diwani wa kata ya Mkomaindo, Ally Salvatory alisema halmashauri isisite kuchukua hatua ili kuwanusuru wakulima wasipoteze fedha zao.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa jimbo la Masasi, Rashidi Chuachua alisema kwa kasi ya wasichana kutoka maeneo mbalimbali kuja Masasi kwa ajili ya kufanyashughuli ya biashara ya ngono ni kubwa na lazima idhibitiwe.

"Tumeona maeneo mbalimbali hapa nchini wasichana kama hawa ambao wanafanyabiashara hii ambayo sio rasmi wakichukuliwa hatua na sisi hapa kwetu tusifumbie macho," alisema Chuachua

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Masasi, Gimbana Ntavyo alisema awali wataalamu wa halmashauri hiyo wamekuwa wakiwatembelea kwenye maeneo na kuwapa elimu mbalimbali ikiwemo ya ujasiliamali.

Alisema lengo kuwapa elimu ya masuala ya ujasiliamali na afya ni kuona wanaachana na shughuli hiyo badala yake watafute shughuli zingine za kihalali na waweze kujipatia kipato.

Chanzo: Mwananchi
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Messages
10,808
Points
2,000

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2012
10,808 2,000
FURAHA UCHANGAMFU WA MJI,MZUNGUKO WA FEDHA NI PAMOJA NA UKAHABA.
#kila mtu aishi apendavyo,hao wadada wanawahusu nini hao madiwani.
Ni vyema juhudi zoa wakazielekeza zaidi kwrnye maendeleo ya eneo lao kuliko ujinga huo.
#dumbshits.
 
TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Messages
3,809
Points
2,000

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2010
3,809 2,000
Malipo ya Korosho kwa wakulima wilayani Masasi Mkoani Mtwara yametajwa kuwa ni chanzo cha ongezeko la uwepo wa kina dada wanaofanya biashara ya ngono wilayani humo ili kujipatia fedha hizo za korosho.

Hayo yalisemwa jana wilayani Masasi na Madiwani wa halmashauri ya mji Masasi walipokuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kikao cha baraza la Madiwani.

Walisema katika wilaya ya Masasi hivi sasa kumekuwa na makundi mbalimbali ya wasichana kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania ambao wanafanya biashara ya ngono.

Diwani wa kata ya Mkuti, Hamza Machuma alisema kata yake ya Mkuti kuna makundi ya wasichana ambao wamekodi vyumba mitaani na biashara yao kubwa ni biashara ya ngono.

Alisema wasichana hawa mara nyingi wamekuwa wakionekana hasa katika kipindi cha misimu ya mauzo ya zao la korosho kwa vile wanafahamu kipindi hiki wakulima wanapata fedha za zao hilo.

"Tunaomba hatua zichukuliwe dhidi ya makundi haya kwani biashara inayofanyika na hawa wadada sio rasmi," alisema Machuma

Naye diwani wa kata ya Mkomaindo, Ally Salvatory alisema halmashauri isisite kuchukua hatua ili kuwanusuru wakulima wasipoteze fedha zao.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa jimbo la Masasi, Rashidi Chuachua alisema kwa kasi ya wasichana kutoka maeneo mbalimbali kuja Masasi kwa ajili ya kufanyashughuli ya biashara ya ngono ni kubwa na lazima idhibitiwe.

"Tumeona maeneo mbalimbali hapa nchini wasichana kama hawa ambao wanafanyabiashara hii ambayo sio rasmi wakichukuliwa hatua na sisi hapa kwetu tusifumbie macho," alisema Chuachua

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Masasi, Gimbana Ntavyo alisema awali wataalamu wa halmashauri hiyo wamekuwa wakiwatembelea kwenye maeneo na kuwapa elimu mbalimbali ikiwemo ya ujasiliamali.

Alisema lengo kuwapa elimu ya masuala ya ujasiliamali na afya ni kuona wanaachana na shughuli hiyo badala yake watafute shughuli zingine za kihalali na waweze kujipatia kipato.

Chanzo: Mwananchi
Haija anza leo na wanacho s uwen Uwenda na wao wateja
 
Katumbasongwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2018
Messages
216
Points
250

Katumbasongwe

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2018
216 250
Mi nilijua vibaka au majambazi, madiwani waache ukuda,siku hizi Kila mtu anashinda mechi zake home! Don't hate a player, hate the game!

Forum statistics

Threads 1,381,426
Members 526,090
Posts 33,799,888
Top