Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====


JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo

Pia soma: Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

- SIMULIZI: Mauaji ya Mfanyabiashara Musa Hamis Mtwara, Machozi na Damu
 
Niliagizwa kazi moja kwa POLICE....
Aisee hao wengi ni watu waliofeli maisha na kukata tamaa kabisaaaa..... YAANI ASKARI POLISI HAWANA MATUMAINI NA NI WAOGA WA MAISHA....
wao kuua maadam wana silaha na kusingizia uhalifu na jambo la kawaida.
NI WAOGA KUFANYA KAZI NA BIASHARA.... Wao ni kutapeli, kudhulumu na RUSHWA... Ni jeshi la waliofeli.
 
Ndo maana braza Hamza akaamua kufanya yake.
Wakampa na cheo Cha ugaidi.
image_search_1643081104576.jpg
 
Back
Top Bottom