Mtwara kutumia gesi asilia majumbani

neema shamuhenya

JF-Expert Member
May 24, 2018
312
216
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani a m e z i n d u a mradi wa ujenzi wa mtambo wa kusambaza gesi asilia majumbani mkoani Mtwara, ambao baada ya miezi mitatu watumiaji 150 wataanza kunufaika.

Dk Kalemani alizindua mradi huo juzi katika Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mtwara baada ya kuzindua megawati nne za umeme katika Kituo cha Umeme cha Mtwara.

Alisema ujenzi wa mtambo huu umegharimu jumla ya Sh billioni 1.5 kwa ajili ya kuwapelekea watumiaji wa awali wasiopungua 150 ambao baada ya miezi mitatu, wataanza kutumia gesi hiyo majumbani.

Aliongeza kuwa matumizi ya gesi asilia ni madogo sana yaani ni kama hayapo, kwa kuwa wananchi wengi wanatumia kuni na mkaa kuliko gesi.

“Sasa mtungi wa gesi ni takriban Sh 55,000, lakini ukitumia gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani itakuwa Sh 25,000 na utatumia kwa mwezi mzima hivyo ni nafuu kwa mwananchi wa Tanzania,” alisema.

“Mwezi Mei tulianza matumizi ya gesi majumbani, lakini leo tumeanza matumizi ya gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara. Hayawi hayawi yamekuwa,” alisema.

Aidha, alieleza kuwa kuna magari zaidi ya 100 yanatumia gesi asilia jijini Dar es Salaam, hivyo kuazia Machi mwakani, wataanza usanifu ili magari ya Mkoa wa Mtwara nayo yaanze kutumia gesi asilia.

Alitoa mwito kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanza kutoa elimu mara moja kwa wiki kwa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara ili kuhakikisha kuwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo wanapata uelewa mzuri katika matumizi ya gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alieleza kuwa “umeme tunaoutumia kwa sasa, asilimia 60 inatokana na gesi asilia na sasa gesi hii inaweza kutumika kwa matumizi ya majumbani na wananchi watanufaika moja kwa moja na gesi asilia inayozalishwa kutoka Mkoa wa Mtwara”.

Naye Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia alimpongeza Dk Kalemani kwa kuwa msikivu na mwepesi wa kutimiza ahadi zake kwa wabunge wenzake.

Alitoa mwito kwa TPDC kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na Lindi ili kuondoa woga na kuwaelimisha matumizi bora ya gesi asilia
 
"Gesi kwanza chama baadae"

"Gesi haitoki"

Nimeikumbuķa Mtwara ya enzi zile, porojo zilikuwa nyingi mara mtwara itakuwa kama dubai mambo ya uchumi wa gesi
 
Back
Top Bottom