kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 17,630
- 14,752
Sakata la Wanamtwara kupinga gesi kupelekwa Dar lilitulizwa kwa nguvu kubwa sana, halikumalizwa kabisa,
Tuliletewa wanajeshi na silaha za kivita + vifaru,
Viongozi wetu waliteswa sana wengine waliumizwa, dada zetu walibakwa, mali zikaibwa na nyingine kuharibiwa vibaya kwa vile tu tulidai usawa katika mgawanyo wa rasilimali.
Yote hayo hayajalipwa kwa lolote, hakuna mapya sana yaliyotekelezwa kutokana na madai yetu!
Ambayo ni pamoja na miundo mbinu mizuri, elimu na afya. Bado serikali haijaweka nia dhabiti yakukumbuka ukanda huu uliotengwa kwa kipindi kirefu. Watanzania huku Mtwara mabomba yakusafirisha gesi ndiyo yanachimbiwa ilhali hakuna la maana ambalo ni la moja kwa moja lililofanyika kwa wanajamii.
Naumia sana kuyaona haya mabomba yanavyowekwa huku, nakumbuka sana nguvu kubwa kupita kiasi iliyotumika kuwatuliza wananchi.
Nadhani ukimya wetu unaweza kuwa na kishindo kikubwa sana, kama serikali haitatekeleza yale tunayoyadai tokea mwanzo.
HAKI YETU haitapotea hivi hivi..