MTWARA! Kimya kingi Kina mshindo..

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
17,613
14,724
Sakata la Wanamtwara kupinga gesi kupelekwa Dar lilitulizwa kwa nguvu kubwa sana, halikumalizwa kabisa,
Tuliletewa wanajeshi na silaha za kivita + vifaru,

Viongozi wetu waliteswa sana wengine waliumizwa, dada zetu walibakwa, mali zikaibwa na nyingine kuharibiwa vibaya kwa vile tu tulidai usawa katika mgawanyo wa rasilimali.
Yote hayo hayajalipwa kwa lolote, hakuna mapya sana yaliyotekelezwa kutokana na madai yetu!

Ambayo ni pamoja na miundo mbinu mizuri, elimu na afya. Bado serikali haijaweka nia dhabiti yakukumbuka ukanda huu uliotengwa kwa kipindi kirefu. Watanzania huku Mtwara mabomba yakusafirisha gesi ndiyo yanachimbiwa ilhali hakuna la maana ambalo ni la moja kwa moja lililofanyika kwa wanajamii.

Naumia sana kuyaona haya mabomba yanavyowekwa huku, nakumbuka sana nguvu kubwa kupita kiasi iliyotumika kuwatuliza wananchi.

Nadhani ukimya wetu unaweza kuwa na kishindo kikubwa sana, kama serikali haitatekeleza yale tunayoyadai tokea mwanzo.

HAKI YETU haitapotea hivi hivi..
 
Ubabe ndio ulotumika kufanikisha malengo yao........
Hili linanikumbusha mbali juu ya kauli ya waziri wa nishati na madini Prof. Muhongo alisema
"Wakati umefika sasa kwa wanamtwara kutengeneza makundi kati ya wapenda maendeleo na wapinga maendeleo".....hayo tu.
 
big show mwenzenu kapewa chake si mwenzenu tena, piganeni na komaeni wenyewe bandugu. Tayari kuna Judas miongoni mwenu.
 
Last edited by a moderator:
kinachofuata ni kuhujumu bomba. chezea makonde wewe kama hujawahi sikia vifa ya mimaji.
 
Sakata la Wanamtwara kupinga gesi kupelekwa Dar lilitulizwa kwa nguvu kubwa sana, halikumalizwa kabisa,
Tuliletewa wanajeshi na silaha za kivita + vifaru,

Viongozi wetu waliteswa sana wengine waliumizwa, dada zetu walibakwa, mali zikaibwa na nyingine kuharibiwa vibaya kwa vile tu tulidai usawa katika mgawanyo wa rasilimali.
Yote hayo hayajalipwa kwa lolote, hakuna mapya sana yaliyotekelezwa kutokana na madai yetu!

Ambayo ni pamoja na miundo mbinu mizuri, elimu na afya. Bado serikali haijaweka nia dhabiti yakukumbuka ukanda huu uliotengwa kwa kipindi kirefu. Watanzania huku Mtwara mabomba yakusafirisha gesi ndiyo yanachimbiwa ilhali hakuna la maana ambalo ni la moja kwa moja lililofanyika kwa wanajamii.

Naumia sana kuyaona haya mabomba yanavyowekwa huku, nakumbuka sana nguvu kubwa kupita kiasi iliyotumika kuwatuliza wananchi.

Nadhani ukimya wetu unaweza kuwa na kishindo kikubwa sana, kama serikali haitatekeleza yale tunayoyadai tokea mwanzo.

HAKI YETU haitapotea hivi hivi..

Si uko Mtwara, kwanini usianze kuchimba gesi, nani alyekuzuwia?
 
Msaliti na tapeli la gesi THE BIG SHOW yupo Tabata anakula rushwa alilolipata kwa kwenda mbele Huku akishadadia udini ukabila na kila aina ya utapeli
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom