Mtwara: Kaimu Mkurugenzi aliyetaka Mwekezaji kulipa Tsh. Milioni 31.6 ya vikao, kuchukuliwa hatua

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,352
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu yoyote anayekwaza wawekezaji nchini atachukuliwa hatua kali, hivyo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amchukulie hatua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara, Bw. Maisha Selemani Mtipa baada ya kumtaka mwekezaji alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili ya gharama za vikao ili aweze kupatiwa eneo.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 01, 2019), wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji na Maonesho ya Biashara mkoa wa Mtwara lililofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara. “Yoyote anayekwaza uwekezaji nchini kwa kuwasumbua wawekezaji tutamshughulikia kabla ya kuwasumbua wawekezaji.”

Amesema Bw. Mtipa amemwandikia barua mwekezaji wa kampuni ya MBR Internation Company Limited akimtaka alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili y a kulipa kamati mbalimbali zikiwemo sh. milioni 1.95 kwa kamati ya Menejimenti ya Halmashauri.

Waziri Mkuu amesema “fedha nyingine sh. milioni 2.27 kwa kamati ya kugawa ardhi ya wilaya, sh. milioni 4.43 kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango sh. milioni 5.14 na sh milioni 17.79 Baraza la madiwani ili wagawane tu, huu ni utaratibu wa wapi? huku ni kufukuza na kukwaza wawekezaji.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeshaondoa tozo zaidi ya 150 zilizokuwa zinakwaza wawekezaji kupata uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo haitaki kusikia mahali popote panawekwa tozo zenye kuwakwaza wawekezaji. Amesema hatua zitakazochukuliwa kwa Bw. Mtipa ziwe fundisho kwa halmashauri zote nchini.
 
Wana CCM hao, na hawa ndio mkuu alisema amekaa akachagua wale wachapakazi, aisee!
 
Ukisikia mambo ya kipumbavu ndio haya, yaani kamati tano kujadili mradi mmoja, hapo ni halmashauiri tu bado nemc tbs nic wizarani mkemia mkuu tume ya atomic kamati za bunge. Wakati VW kule Rwanda wamepewa ardhi bure wamejengewa na jengo wamepewa na mtaji wakuanzia na soko la uhakika. sisi ni longolongo kwa kwenda mbele, halafu vijana wakihangaika ajira munawaambia wajiajiri sijui wakalime, shenzi zenu, kumbe JPM anahaki yakuwatukana. Nasikia kuna mkuu wa mkoa kaenda kwa vijana waliopiga kambi kwa mmisiri kusubiri ajira akawambia wapotee kabla hajawatia ndani, mambo gani ya hovyo hivi?
 
unachanganya boss
President hateui kaimu....

Huyo amepewa nafasi ama iko wazi hakuna mkurugenzi ama mkurugenzi yuko likizo a a nje ya kituo huyo kaimu anashikilia kwa muda mfupi tu
Wana CCM hao, na hawa ndio mkuu alisema amekaa akachagua wale wachapakazi, aisee!
 
hawa viongozi wa wilaya na mikoa wanaoteuliwa huwa hawana uchungu na maendeleo ya eneo husika. Wanatakiwa wawe wa kuchaguliwa.
 
Uko sahihi.Lakini na YEYE alishindwa kutafuta ushauri kwa wazoefu au mamlaka za juu yake?
unachanganya boss
President hateui kaimu....

Huyo amepewa nafasi ama iko wazi hakuna mkurugenzi ama mkurugenzi yuko likizo a a nje ya kituo huyo kaimu anashikilia kwa muda mfupi tu
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu yoyote anayekwaza wawekezaji nchini atachukuliwa hatua kali, hivyo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amchukulie hatua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara, Bw. Maisha Selemani Mtipa baada ya kumtaka mwekezaji alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili ya gharama za vikao ili aweze kupatiwa eneo.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 01, 2019), wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji na Maonesho ya Biashara mkoa wa Mtwara lililofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara. “Yoyote anayekwaza uwekezaji nchini kwa kuwasumbua wawekezaji tutamshughulikia kabla ya kuwasumbua wawekezaji.”

Amesema Bw. Mtipa amemwandikia barua mwekezaji wa kampuni ya MBR Internation Company Limited akimtaka alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili y a kulipa kamati mbalimbali zikiwemo sh. milioni 1.95 kwa kamati ya Menejimenti ya Halmashauri.

Waziri Mkuu amesema “fedha nyingine sh. milioni 2.27 kwa kamati ya kugawa ardhi ya wilaya, sh. milioni 4.43 kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango sh. milioni 5.14 na sh milioni 17.79 Baraza la madiwani ili wagawane tu, huu ni utaratibu wa wapi? huku ni kufukuza na kukwaza wawekezaji.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeshaondoa tozo zaidi ya 150 zilizokuwa zinakwaza wawekezaji kupata uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo haitaki kusikia mahali popote panawekwa tozo zenye kuwakwaza wawekezaji. Amesema hatua zitakazochukuliwa kwa Bw. Mtipa ziwe fundisho kwa halmashauri zote nchini.
Mbona haya mambo ni ya kawaida sana huko Halmashauri? Kuna mtu namfahamu alikuwa ni Mhanga wa fedha hizo za Muwekezaji kwani baadaye zilitumika kama rushwa kwa ajili ya kutimiza matakwa ya Muwekezaji.
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu yoyote anayekwaza wawekezaji nchini atachukuliwa hatua kali, hivyo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amchukulie hatua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara, Bw. Maisha Selemani Mtipa baada ya kumtaka mwekezaji alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili ya gharama za vikao ili aweze kupatiwa eneo.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 01, 2019), wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji na Maonesho ya Biashara mkoa wa Mtwara lililofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara. “Yoyote anayekwaza uwekezaji nchini kwa kuwasumbua wawekezaji tutamshughulikia kabla ya kuwasumbua wawekezaji.”

Amesema Bw. Mtipa amemwandikia barua mwekezaji wa kampuni ya MBR Internation Company Limited akimtaka alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili y a kulipa kamati mbalimbali zikiwemo sh. milioni 1.95 kwa kamati ya Menejimenti ya Halmashauri.

Waziri Mkuu amesema “fedha nyingine sh. milioni 2.27 kwa kamati ya kugawa ardhi ya wilaya, sh. milioni 4.43 kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango sh. milioni 5.14 na sh milioni 17.79 Baraza la madiwani ili wagawane tu, huu ni utaratibu wa wapi? huku ni kufukuza na kukwaza wawekezaji.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeshaondoa tozo zaidi ya 150 zilizokuwa zinakwaza wawekezaji kupata uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo haitaki kusikia mahali popote panawekwa tozo zenye kuwakwaza wawekezaji. Amesema hatua zitakazochukuliwa kwa Bw. Mtipa ziwe fundisho kwa halmashauri zote nchini.
Mtipa ni mbuz wakafara. Wenye kuagiza wamejichimbia na uwenda ndio umewapa kaz yakumshughulikia.
 
Nidhamu ya kazi iliyorudishwa baada ya Jk kustaafu ni ipi?, maana kila wanapopita Viongozi wanakuta Madudu kama ya wakati ule wa Rais ‘dhaifu’?

Zamani kwa sababu ya uhuru mkubwa Madudu ya Watendaji hayakusubiri ziara za Viongozi kuibuliwa lakin kutokana na mazingira ya sasa kila mtu anaogopa kuzungumzia madudu ya Serikal kuogapa kuwekwa kwenye kundi la wanaohujumu Serikal matokeo yake ndio mpaka Rais au PM afanye ziara, kwa lugha nyingine maeneo ambayo hawajapita pengine kuna ‘kufuru ‘
 
Nidhamu ya kazi iliyorudishwa baada ya Jk kustaafu ni ipi?, maana kila wanapopita Viongozi wanakuta Madudu kama ya wakati ule wa Rais ‘dhaifu’?

Ndio porojo za Ccm hizo,wanakwambia wameboresha utendaji.

MATAGA.
 
Back
Top Bottom