Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu yoyote anayekwaza wawekezaji nchini atachukuliwa hatua kali, hivyo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amchukulie hatua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara, Bw. Maisha Selemani Mtipa baada ya kumtaka mwekezaji alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili ya gharama za vikao ili aweze kupatiwa eneo.
Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 01, 2019), wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji na Maonesho ya Biashara mkoa wa Mtwara lililofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara. “Yoyote anayekwaza uwekezaji nchini kwa kuwasumbua wawekezaji tutamshughulikia kabla ya kuwasumbua wawekezaji.”
Amesema Bw. Mtipa amemwandikia barua mwekezaji wa kampuni ya MBR Internation Company Limited akimtaka alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili y a kulipa kamati mbalimbali zikiwemo sh. milioni 1.95 kwa kamati ya Menejimenti ya Halmashauri.
Waziri Mkuu amesema “fedha nyingine sh. milioni 2.27 kwa kamati ya kugawa ardhi ya wilaya, sh. milioni 4.43 kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango sh. milioni 5.14 na sh milioni 17.79 Baraza la madiwani ili wagawane tu, huu ni utaratibu wa wapi? huku ni kufukuza na kukwaza wawekezaji.”
Waziri Mkuu amesema Serikali imeshaondoa tozo zaidi ya 150 zilizokuwa zinakwaza wawekezaji kupata uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo haitaki kusikia mahali popote panawekwa tozo zenye kuwakwaza wawekezaji. Amesema hatua zitakazochukuliwa kwa Bw. Mtipa ziwe fundisho kwa halmashauri zote nchini.