Mtwara: Amuua mzee ili aibe kuku na sola

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamshikilia Mukhsin Selemani mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Libobe wilaya ya Mtwara, kwa tuhuma za kumuua Hassan Mtipa kwa panga katika tukio la wizi.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara, – Mark Njera amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mayanga, ambapo Mukhsin aliingia kwenye nyumba ya Mtipa mwenye umri wa miaka 67 kwa lengo la kuiba kuku, sola na nguo.

Baada ya kukamatwa na polisi, mtuhumiwa huyo amekiri kuiba vitu hivyo pamoja na kufanya mauaji hayo.
 
Daa kuku anafanya mtu atolewe roho? Dhambi zakujitakia,
Ila vijana wa huko ni wavivu sana
 
Ndiyo umuue mtu kwa kuiba kuku, si ajabu kuku mwenyewe atakuwa 1 tu

Mjomba njaa mbaya Sana... Huyo mtuhumiwa angekuwa amewezeshwa kupata riziki kihalali hayo yasingetokea..

Mwaka huu ipo habari mama mmoja alimkata mwanae na kumchemsha ktk sufuria...
 
Bangi za Msumbuji kali mno, ukizoea zile ukivuta hizi za Arusha utahisi ni sigara.
Ona sasa zilivyompelekesha kijana Muksini
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom