Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,830
- 4,727
Afisa elimu mkoa wa Mtwara bi Fatuma Kilimia amemdhalilisha Mwalimu wakike wa shule ya sekondari ya Naliendele mkoani hapo.
Mbele ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 20 ndani ya ofisi ya waalimu, bi Kilimia alizungumza maneno ya kejeli kwa mwalimu huyo kutokana na kukerwa na kitendo cha Mwalimu huyo kuwa na furaha muda wote.
Bi Kilimia alienda mbali zaidi na kudhihaki ujauzito wa Mwalimu huyo na kumwambia kuwa asitegemee kujifungua Malaika, Waziri au Rais.
Maneno hayo ya dharau na kejeli yaliyotawala kikao hicho yalipelekea Mwalimu huyo kulia mpaka mwisho wa kikao.
Hii si Mara yakwanza kwa mama huyu kutoa lugha za kejeli na dhihaka kwa walimu kwani vitendo hivi viliwahi kufanyika pia alipotembelea shule za sekondari Mangamba, Shangani, Rahaleo na shule nyingine za msingi na sekondari.
Afisa elimu mkoa yupo katika ziara ya kutembelea shule zilizofanya vibaya katika matokeo ya kidato cha pili na cha nne.