MTV EMA wampokonya tuzo Wizkid na kumpa Alikiba aliyestahili kushinda

Francis Mawere

JF-Expert Member
Nov 17, 2015
954
825
Katika hatua ambayo imewafurahisha mashabiki wengi wa muziki nchini, MTV EMA wanadaiwa kumpokonya tuzo ya Best African Act na Worldwide Act, Wizkid na kumpa Alikiba ambaye alistahili kushinda.
Siku chache zilizopita, kulitokea sintofahamu baada ya Wizkid kutangazwa mshindi ilhali kwenye website ya tuzo hizo, kura zilionesha kuwa ni Alikiba ndiye aliyeshinda.

Alikiba amethibitisha taarifa hizo wakati akichat live Jumatano hii kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Amesema baada ya mashabiki wake kulalamika kuhusiana na mkanganyiko huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri kuwa na makosa na kuutumia ujumbe uongozi wake kuwa Alikiba ndiye mshindi halali, na sio Wizkid.

“Sasa ndio nimepata confirmation kwamba ni kweli tuzo inakuja Tanzania na vile vile mimi siwezi kuzungumzia, nitasubiri mpaka nizishike,” amesema Kiba.

Muimbaji huyo amedai kuwa habari hizo amezipokea kwa furaha kubwa na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kushinda na kuwa nyuma yake.

Wakati hup huo Kiba amempongeza Wizkid kwa ushindi wa tuzo nyingine ya Afrima. Kwa upande wa Wizkid, tayari amefuta post zote za Instagram alizokuwa ameweka kushangilia ushindi huo.

BONGO5
 
Wajinga hao km ningekuwa Wizkid sikubali tena waniweke ktk nomination......
 
Back
Top Bottom