Mtuunge mkono walimu tunaofanya kazi kwa mazoea, kwani hata serikali yetu inatutendea kwa mazoea

MTABO

Member
Mar 6, 2014
97
125
Inasikitisha kuona serikali hii inayojiita ya kazi tu, na inayojitapa kukusanya matrioni kwa kila mwezi, ikishindwa kuwalipa pesa za kujikimu walimu elfu 3 tu wa ajira mpya 2017. Sio hali ya kawaida kushindwa kuwapa pesa za kujikimu walimu elfu 3 tu, bali ni tendo la makusudi lenye lengo la kuwadhoofisha walimu wapya ktk utendaji wao kazi. Haya ndio matendo ya mazoea ya serikali yetu yanayosababisha walimu wenye njaa wafanye kazi chini ya kiwango.

Jana mheshimiwa Jafo akijibu swali la nyongeza bungeni kuhusu ni lini serikali itawapatia walimu wa ajira mpya 2017 pesa za kujikimu ili wapate moyo wa kujituma kazini; Jafo bila aibu alijifanya amesahau swali na hatimae kwa makusudi akagoma kabisa kujibu swali hilo. Kisha mheshimiwa mwenyekiti wa bunge akambeba Jafo na kusema kua aliyeuliza swali ameshaelewa. Sijui mwenyekiti wa bunge alimaanisha aliyeuliza swali ameshaelewa kua seriakli imegoma kutoa pesa, au kaelewa lipi...!

Katika kipindi hiki kigumu kwa walimu wapya, kuna wadudu watu halamshauri na wakuu wa shule, wanajitekenya eti wako wanatuangalia tabia zetu. Hua najiuliza, hivi hawa wadudu wana akili kweli? utapimaje ukakamavu wa mwanajeshi mwenye njaa kali? Wakiongea hayo madudu yao, hua natamani hata niwakate makofi.

Acheni walimu tufanye kazi kwa mazoea, kwani hata seriakali yetu inatutetendea haya kwa mazoea. Tunawajibika kwa kiwango kile amabcho serikali yetu anapenda tuwajibike, kwa maana kwamba haitaki tujitume. Kila mtu abebe msalaba wake, mwanafunzi akiacha kusoma twisheni huko mtaani, nasema 'feli'. Narudia tena, 'fe li'. Ni maneno mawili tu, yaani 'fe' na 'li'.
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,769
2,000
kazi ambayo ingekuwa ya kwanza kuheshimika lakini ndo ya kwanza kudharaulika hapa nchini.
mbali na malalamiko ambayo walimu wamekuwa wakitoa miaka nenda rudi, lakini hawa walimu ndo wamekuwa chambo wakubwa wa mapapa ccm na wao bila hiyana huwatumikia hawa makafiri ccm hasa nyakati za uchaguzi kwa vijamalipo vidogo licha ya kupitia mateso mengi kwenye taaluma yenu.
walimu nyie ndo watu wa kwanza wa kuleta mabadiliko nchi muwe mnawaambia hata hao wanafunzi wenu kuwa ccm ni gonjwa hatari sana kwenye nchi yetu.
 
MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,653
2,000
Inasikitisha kuona serikali hii inayojiita ya kazi tu, na inayojitapa kukusanya matrioni kwa kila mwezi, ikishindwa kuwalipa pesa za kujikimu walimu elfu 3 tu wa ajira mpya 2017. Sio hali ya kawaida kushindwa kuwapa pesa za kujikimu walimu elfu 3 tu, bali ni tendo la makusudi lenye lengo la kuwadhoofisha walimu wapya ktk utendaji wao kazi. Haya ndio matendo ya mazoea ya serikali yetu yanayosababisha walimu wenye njaa wafanye kazi chini ya kiwango.

Jana mheshimiwa Jafo akijibu swali la nyongeza bungeni kuhusu ni lini serikali itawapatia walimu wa ajira mpya 2017 pesa za kujikimu ili wapate moyo wa kujituma kazini; Jafo bila aibu kujifanya amesahau swali na hatimae kwa makusudi akagoma kabisa kujibu swali hilo. Kisha mheshimiwa mwenyekiti wa bunge akambeba Jafo na kusema kua aliyeuliza swali ameshaelewa. Sijui mwenyekiti wa bunge alimaanisha aliyeuliza swali ameshaelewa kua seriakli imegoma kutoa pesa, au kaelewa lipi...!

Katika kipindi hiki kigumu kwa walimu wapya, kuna wadudu watu halamshauri na wakuu wa shule, wanajitekenya eti wako wanatuangalia tabia zetu. Hua najiuliza, hivi hawa wadudu wana akili kweli? utapimaje ukakamavu wa mwanajeshi mwenye njaa kali? Wakiongea hayo madudu yao, hua natamani hata niwakate makofi.

Acheni walimu tufanye kazi kwa mazoea, kwani hata seriakali yetu inatutetendea haya kwa mazoea. Tunawajibika kwa kiwango kile amabcho serikali yetu anavyopenda tuwajibike, kwa maana kwamba haitaki tujitume. Kila mtu abebe msalaba wake, mwanafunzi akiacha kusoma twisheni, nasema 'feli'. Narudia tena, 'fe li'. Ni maneno mawili tu, yaani 'fe li'.
Mishahara vipi bado hamjaanza kupata ticha?
 
MTABO

Member
Mar 6, 2014
97
125
Mishahara vipi bado hamjaanza kupata ticha?
sio wote waliopata. hata hivyo, effects za serikali kuwanyima pesa za kujikimu hao walimu ni mbini zaidi ya unavyofikiria. haya mazoea ya serikali ndio yanayodhoofisha juhudi ufanisi wa walimu. haiingii akilini eti serikali imeshindwa kuwapa pesa za kujikimu walimu elfu tatu tu, tena walimu wa sayansi wanaosema kila siku wanawwahitaaji sana.
 
maneka

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
398
500
Mwalimu ni nani katika nchi hii? Kama hawaridhiki waache! Humu jf kuna walimu wangapi? Nina imani wapo wengi. Sasa iweje wapo kimya? Inamaanisha wameridhika. Wajinga ndiyo waliwao.
 
MTABO

Member
Mar 6, 2014
97
125
Mwalimu ni nani katika nchi hii? Kama hawaridhiki waache!
kwahio unamaanisha kua serikali iko sahihi kuwanyima walimu wapya pesa za kujikimu, ili walimu hao waishi kwa taabu!
kwa maana kwamba mwalimu wapya kutolipwa pesa ya kujikimu ndio sahihi, na asiyependa huo usahihi basi na aache kazi!
 
Mushi92

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,913
2,000
Wapo vijana wengi tuu waliotazamia hizo ajira lkn wakakosa na bado wanatamani sana.
Sasa nyie mzichezee tutaingiza nguvu mpya
 
MTABO

Member
Mar 6, 2014
97
125
Wapo vijana wengi tuu waliotazamia hizo ajira lkn wakakosa na bado wanatamani sana.
Sasa nyie mzichezee tutaingiza nguvu mpya
unaonekana kama hujielewi. nani anachezea nafasi, mwalimu ajira mpya anayelia njaa kwa kunyimwa pesa za kujikimu, au serikali iliyogoma kumpa mwalimu ajira mpya pesa za kujikimu?

kwanza tambua hao wanaosubri ajira, wataajiriwa na watakuja kuungana na hao wanaotaabika kwa njaa zilizosababishwa na serikali kwa kuwanyima pesa za kujikimu, na sio kwamba hawa wanaotaabika watatoka kwanza ili kupisha nafasi kwa hao wanaosubiri. kinachosubiriwa ni muda wa kutoa ajira, na sio nafasi zibaki wazi. jambo la msingi ni serikali kuacha mazoea ya kutekeleza dhambi za kutowalipa walimu ajira mpya pesa za kujikimu.
 
galindas

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
985
1,000
Wenzio tumeacha kulalamika. Fanya hivi: Nenda benki (sio nmb) kapate minimum 12m, kama upo huku mashambani kama sisi, nunua ng'ombe wa maziwa wannewenye mimba kwa 1.5m@, jenga banda kwa 1m, tafuta mkata majani. baada ya mwezi au miwili utaanza kupata maziwa atleast 15-20 lts kwa kila ng'ombe. lita kwenye vituo vya kukusanyia maziwa ni 700 kwa lita. Utapata kati ya 42000-56000 kwa siku au 1680000 kwa mwezi, mlipe mkata majani vizuri ili aishi nao kama ndugu zake, ndani ya mwaka utasahau kero zoote za kazi na wenzqko watakuheshimu pia.
 
markbusega

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
587
250
Mh Rais kazi anayo huku makinikia huku walimu wanafanya maigizo? wazazi maskini na wasiojali mstakabali wa watoto wao imeshakula kwao
 
maliedo

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
1,382
2,000
Mwalimu ni nani katika nchi hii? Kama hawaridhiki waache! Humu jf kuna walimu wangapi? Nina imani wapo wengi. Sasa iweje wapo kimya? Inamaanisha wameridhika. Wajinga ndiyo waliwao.
Mwalimu ni yule aliekufundisha kuandika na kusoma,
 
kkkt

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
368
250
Wenzio tumeacha kulalamika. Fanya hivi: Nenda benki (sio nmb) kapate minimum 12m, kama upo huku mashambani kama sisi, nunua ng'ombe wa maziwa wannewenye mimba kwa 1.5m@, jenga banda kwa 1m, tafuta mkata majani. baada ya mwezi au miwili utaanza kupata maziwa atleast 15-20 lts kwa kila ng'ombe. lita kwenye vituo vya kukusanyia maziwa ni 700 kwa lita. Utapata kati ya 42000-56000 kwa siku au 1680000 kwa mwezi, mlipe mkata majani vizuri ili aishi nao kama ndugu zake, ndani ya mwaka utasahau kero zoote za kazi na wenzqko watakuheshimu pia.
Unaandika kirahiiiiisi etie?
 
MTABO

Member
Mar 6, 2014
97
125
Mh Rais kazi anayo huku makinikia huku walimu wanafanya maigizo? wazazi maskini na wasiojali mstakabali wa watoto wao imeshakula kwao
kama walikua hawana uwezo wa kuajiri, wangeacha kuajiri kama walivyokua wameacha kuajiri tangu mwaka 2015.
kama unaona ni sahihi mwalimu kulia njaa kwasababu Rais kawanyima pesa za kujikimu, ona ni sahihi pia watoto wako wakipata elimu mbovu kwasababu ya kufundishwa na walimu wenye njaa kali iliyosababishwa na Rais wako kuwafanyia ukatili walimu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom