Mtunza Ghala, Chama Kikuu cha Ushirika Kagera (1990) Ltd (Nafasi 1)

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,432
1,387
Chama Kikuu cha Ushirika Kagera (1990) Ltd kinaundwa na vyama vya msingi 134 kutoka katika wilaya tatu za Muleba, Bukoba na Misenyi. KCU (1990) LTD yenye makao makuu katika manispaa ya Bukoba, inaendesha shughuli zake chini ya Sheria ya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013, Ili kutekeleza kwa ufanisi shughuli zake, KCU (1990)Ltd inatangaza nafasi ifuatayo:-

2. MTUNZA GHALA (NAFASI 1)

MAJUKUMU


  • Kutunza mali kwenye ghalala kahawa kwa ufasaha.
  • Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji na usambazaji wa Kahawa:
  • Kusimamia utunzaji wa mali iliyomo kwenye Ghala:
  • Kupokea, kukagua ubora wa kahawa. kisha kuhifadhi kahawa kwa ufasaha.
  • Kubuni mfumo wa uwekaji na utunzaji wa Kahawa & vifaa ghalani (Location index design)
  • Kuhesabu na kutunza mali iliyomo ghalani mara kwa mara {Perpetual Stock Checking
  • Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya Mali iliyomo ghalani kila kuwa na uwezo wa kila mwezi siku mwisho wa Msimu wa kahawa (Seasonal Stock taking)
  • Kusimamia manunuzi, utunzaji na matumizi bora ya vifaa vya kazi ghalani;
  • Kushauri uongozi kuhusu mpango endelevu wa kuhimiza usalama wa bidhaa{Kahawa) toka kwa mkulima hadi kwa Mlajic(From producer up to the end consumer)
    Kufanya shughuli nyinginezo atakazoelekezwa na msimamizi wake wa kazi.

VIGEZO NA UZOEFU

  • Awe amehitimu shahada ya Biashara yenye mchepuo wa ugavi au Stashahada ya juu ya ugavi (Advanced Diploma in Material Management) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na bodi PSPTB (Procurement, Supplies Professionals & Technicians Board ya Tanzania)
  • Awe na uwezo wa kuturnia lugha ya Kiswahili na kingereza kwa ufasaha
  • Awe na uwezo wa kutumia kompyuta katika program zifuatazo: Word. Excell, Power Point na Internet
  • Awe najewa ustiawanakuunwa wakosaana
  • Awe ni raia wa Tanzania
  • Awe na umri usiozidi miaka 45
  • Awe na uzoefu usiopungua miaka 3
  • Mwenye uzoefu wa kutunza maghala ya kahawa ni faida ya nyongeza

Kwa ambaye ana sifa na vigezo vilivyotajwa hapo juu, anaweza kutuma maombi kwa barua iliyoandikwa kwa mkono na kusainiwa kwa njia ya Posta, ikiambatana na maelezo binafsi (CV)
yenye anuani, namba ya simu na barua pepe, picha ndogo mbili, nakala za vyeti na wadhamini watatu wenye mali zisizo hamishika (Fxed assets) au watumishi wenye mikataba ya kazi ya kudumu kwa anuani liyopo hapa chini.

Waliokwisha kutuma maombi wasitume tena. Aidha, ambao hawatapata wito wa kuhudhuria usahili wajue kuwa hawakukidhi vigezo vinavyohitajika.

Mwisho wa kupokea maombi ni Ijumaa, tarehe 26/04/2022 saa 10.00 ioni

MENEJA MKUU, KCU (1990) LTD

S.LP 5, BUKOBA
 
Back
Top Bottom