Mtunga Sheria anapovunja Sheria....!!!

Mfua suleiman

Member
Feb 27, 2014
60
62
NUKUU:
"Pamoja na bei ya nyanya kushuka tunaendelea kulima" - Peter Msigwa
(Mwisho wa Kunukuu)

Maneno hayo na picha hizi zimewekwa kwenye Facebook Akaunt ya Mbunge wa Iringa Mjini Ndg. Peter Msigwa na yeye mwenyewe.

MUHIMU:
Haki za watoto zipo wapi?

Kama Msigwa angekua ni mzazi wa watoto hawa angekubali watoto wake kufanyiwa ukatili wa aina hii?

Dada yangu Hajjat Mtarajiwa Ummy Mwalimu Wizara yako ina dhamana ya jambo hili na natarajia kuona haki ya watoto hawa inalindwa na hatua stahiki kwa mwajili wao Ndg. Msigwa zinachukuliwa.

"Tuungane pamoja kulinda haki za watoto"

[HASHTAG]#MtotoWamwenzioNiWako[/HASHTAG]
 

Attachments

  • 1479937588581.jpg
    1479937588581.jpg
    39.5 KB · Views: 30
  • 1479937623655.jpg
    1479937623655.jpg
    30.5 KB · Views: 27
Ndugu zangu hizi kazi ndogo ndogo tumezifanya sana tukiwa wanafunzi wa shule za msingi.Nia ni kupata kipato kidogo kwa ajili ya kununua vitu vidogo vidogo.Kazi hizi zilifanyika baada ya kurudi nyumbani na siku za jmosi ambazo hakuna masomo.Hivyo sio cha ajabu hapo hao watoto kubeba ndoo za nyanya.Watu waache ushabiki usio na tija.Sasa hivi maisha ni magumu sana hasa vijijini tunakotoka.
 
Usikute hao watoto wanasaidia wazazi wao kupeleka nyanya hapo ili kupata chochote kitu nyumbani, haina tofauti na mtoto kumsaidia mama kuosha vyombo au kuchota maji.

Tungepata majibu yasiyo na ukakasi katika hili kwanza,
Hao watotot ni waajiriwa? Wanafanya kazi kwa huyo Mh? Au wanafanya hayo kw makubaliano gani?
 
Back
Top Bottom