Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,646
- 35,981
Binafsi ni mtumishi wa umma. Nimewahi kukopa mara 1 na kufanya top up mara 2. Kwa lugha nyepesi ni kwamba nimekopa mara 3.
Kwakweli hali ni mbaya, topup ni wizi wa wazi kabisa. Hata hii mikopo ni unyonyaji ila tu watumishi hukopa kwa aidha shida ya haraka au kukosa maarifa. Muda mwingine hukopa ili tu mtu ajikwamue aweze kununua usafiri, kujenga au kulipa ada yake au ya mtoto.
Ashukuriwe Mungu sasa nina miaka 3 sijakopa wala kufanya topup. Nasubiri deni liishe nikope parefu kidogo niache kazi. Maana siku hizi ukiacha kazi ili ukajiajiri hupati kirahis ile fedha yako kutoka mfuko uliochangia.
Kwakweli watumishi wa umma ukiondoa wezi na mafisadi siku zao za furaha zinahesabika.
Katika mwezi wa siku 28-31 mtumishi wa umma hupata furaha siku 5- 10 tu.
Serikali iwakopeshe watumishi wake mikopo isiyo na riba ili kuwaondolea ufukara na umaskini.
Kwakweli watumishi wengi ni mafukara, kadi zao za benki zimewekwa rehani jambo ambalo ni aibu.
Hizi microfinance institutions zimewarubuni watumishi. Wengi huziendea ili kupata mkopo wa chap wasolve shiida zao baadaye zinageuka kuwa mwiba.
Hata hizi benki kubwa bado zinawaumiza watumishi wa umma ingawa kupata mkopo wenyewe mpaka muzungushane.