Mtumishi wa Umma anawezaje kupata ajira kwenye International organisations kama UN, SADC, AU, EAC

Bandugu salama?

Nadhani humu nitapata jibu la jambo langu ambalo limekuwa likinisumbua kwa miaka.

Mimi ni mtumishi wa Umma wa Halmashauri mwenye miaka 31.
Niliajiriwa 2012 (nikiwa na Diploma, nikawa Afisa mdogo sana (uongozi wangu ulikuwa ndani ya kata).

2013 nikaenda Shule na kupata Bachelor, na 2016 nikaunga Masters.

Nilirudi 2018 kazini, nikahamia bomani na sasa ni Kaimu Mkuu wa Idara.

Tokea 2020 nimekuwa nikiapply sana Kazi kwenye international Organisations kama SADC, AU, UN, EAC na nyengine kibao ila sijawahi itwa hata interview.

Na kinachonishangaza ni kwamba hizi ajira huwa zinatangazwa na Wizara ya Utumishi kupitia website yao.

Nimekuwa nikiapply sana ila sijawahiitwa hata interview.

Sasa bandugu hebu naomba muongozo na Msaada wa kupata hizi post.

1. Je, nakosea kuandika CV?
Mwenye muongozo (link) anipe nione format waitakayo

2. Nakosea kuandika Cover letter?
Mwenye muongozo (link) anipe nione format waitakayo.

Mwenzenu natamani sana kwenda kufanya Kazi huko NAIROBI, GENIVA, ADDIS ABABA na kwengineko.

Rohoni naona kabisa Halmashauri HAINITOSHI.

Nahitaji big challenge in my employment.

ASANTENI.

#YNWA
Mara nyingi sana (sio zote), hizi UN Agencies zinapenda kuchukua watu ambao tayari wana experience ya kufanya kazi na NGOs.

Au kama upo kwenye kitengo flani Serikalini ambacho kuna programmes za UN unazirun, ni rahisi kukuchukua kwani tayari wanakuwa wameshauona weledi wako (evidence zipo)

Ushauri ni kwamba kama una vision ya kuingia UN huko mbele ya safari, anza kuapply kazi kwenye hizi non UN International organisations (INGOs) kwanza hapa Tanzania. Ukipata na ukafanya angalau miezi 6, unaweza sasa kuanza kuapply za UN au hata INGO nje ya Nchi

CV yako ina pages ngapi? Kama una experience ya kazi mbili tu, UN tena nje ya mipaka huwezi kupata .

Kila la kheri
 
Kama huna Kingunge wa kukusimamia hizo sahau Mkuu. Bora uhangaike nazo utakazoziona Google.

The point is ...
Huwa na apply mara kibaoo ajira zao, na huwa zinapitia Utumishi.
Hivyo Kuna zile ambazo Wana hamasisha watumishi wa umma ku apply.

#YNWA
 
Ila upate kiurahisi lazima uwe umefanya kwenye recognized international organization inakuwa rahisi maana wanaamini unajua protocol za organization nyingi za kimataifa hazitofautiani sana
 
Sipati kivipi?

Sijawahi apply shirika la humu nchini na Wala siyataki.

Nahitaji kupanda ndege kwenda kufanya Kazi na watu tofauti na Watanzania.
Anza ku apply kwenye hizi international organization zinazo operates hapa Tanzania ka ngazi yako, hivi hivi direct kwenye huko mbelezi ni ngumu
 
Mwenzio akili yangu ndogoo kama tunda la ubuyu.

Hebu elezea kidogo.

#YNWA

Kwanza kabisa futa hiyo kauli kwamba una akili ndogo. Msomi wa kiwango cha Masters kujidharau au kujiona duni tayari kosa la kwanza hilo.

Turudi kwenye swali lako mkuu.
Ukifanikiwa kuitwa au kufanya usaili/ interview, unatakiwa uongee vizuri kiasi cha kuwashawishi jamaa kwamba uko vizuri kwenye kuwasilisha hoja zako. Na ukipata kazi, mambo mengi kule ni kuandika, kuanzia email, reports na mambo mengine, lazima uwe mwandishi mzuri ili kujihakikishia kubaki kwenye ajira.

Nafikiri hapo tumeelewana kiongozi.
 
Amen.

#YNWA

Kikubwa tu inabidi uendelee kujinoa na kuongeza ujuzi na uzoefu kwenye maeneo kadhaa ili kuongeza nafasi za kuibuka kidedea kwenye mchujo. Ushindani ni mkubwa sana, na watu wako vizuri lakini haimaanishi hauwezi kupata.

Kingine watu hawawi makini kwenye mchakato wa kujaza taarifa zao kwenye zile application zao. Mfano unaweza usiandike miaka ya uzoefu wako wa kazi au elimu kama wanavyotaka, hapo system itakuchuja na kukutupilia mbali, hauingii hata kwa long list achilia mbali shortlist.
 
Bandugu salama?

Nadhani humu nitapata jibu la jambo langu ambalo limekuwa likinisumbua kwa miaka.

Mimi ni mtumishi wa Umma wa Halmashauri mwenye miaka 31.
Niliajiriwa 2012 (nikiwa na Diploma, nikawa Afisa mdogo sana (uongozi wangu ulikuwa ndani ya kata).

2013 nikaenda Shule na kupata Bachelor, na 2016 nikaunga Masters.

Nilirudi 2018 kazini, nikahamia bomani na sasa ni Kaimu Mkuu wa Idara.

Tokea 2020 nimekuwa nikiapply sana Kazi kwenye international Organisations kama SADC, AU, UN, EAC na nyengine kibao ila sijawahi itwa hata interview.

Na kinachonishangaza ni kwamba hizi ajira huwa zinatangazwa na Wizara ya Utumishi kupitia website yao.

Nimekuwa nikiapply sana ila sijawahiitwa hata interview.

Sasa bandugu hebu naomba muongozo na Msaada wa kupata hizi post.

1. Je, nakosea kuandika CV?
Mwenye muongozo (link) anipe nione format waitakayo

2. Nakosea kuandika Cover letter?
Mwenye muongozo (link) anipe nione format waitakayo.

Mwenzenu natamani sana kwenda kufanya Kazi huko NAIROBI, GENIVA, ADDIS ABABA na kwengineko.

Rohoni naona kabisa Halmashauri HAINITOSHI.

Nahitaji big challenge in my employment.

ASANTENI.

#YNWA
Kukusaidia tu, fahamu haya:

1. Hakuna shirika lolote la kimataifa litataka kuajiri mtu kutoka halmashauri au mwenye uzoefu wa kazi za halmashauri. Kwanini? Utendaji wa kazi za halmashauri kwa sehemu umejaa siasa, ubabaishaji (unprofessional) na ushamba (poor exposure). Hivyo uzoefu wako wa kazi za halmashauri ni kikwazo cha kukosa kazi za kimataifa moja kwa moja.

2. Elimu pekee sio kigezo cha kupata kazi kwenye mashirika ya kimataifa. Kwa sasa hapa Tz, watu wenye elimu ngazi ya masters wapo wengi mnoo, na wote wanasikilizia kupata kazi popote. Ukienda Kenya ndio unaweza ukaogopa hata kusema kuwa una Masters, maana graduates wa masters kwao ni kama graduates wa undergraduate hapa Tz. Mashirika ya kimataifa yanataka Elimu mahususi+Uzoefu mahususi.

3. Ajira nyingi za mashirika ya kimataifa ni ajira za mkataba na mahususi, yaani zinalenga jambo fulani kwa muda fulani. Zinamfaa sana mtu special katika uzoefu wa jambo fulani na huru kiajira (freelancer). Kwako sidhani sana kama zinakufaa au utawafaa, unapoteza muda wako au kuwapotezea muda.

4. Mambo ya msingi sana ya kufanya ukitaka kupata kazi za mashirika ya kimataifa.
-Jitahidi ufanye kazi na mashirika yoyote binafsi yenye mtandao wa kimataifa yaliyopo hapa hapa Tanzania.

-Jitahidi upate nafasi ya kuishi au kufanya kazi nje ya Tanzania. Kama huna exposure ya nje ya Tanzania, kuzipata hizo kazi ni ngumu na ukipata hiyo kazi itakutesa sana.

-Onyesha uzoefu wako kwa kusimamia kazi yoyote mahususi itakayoweza kutambulisha ujuzi wako kimataifa.

Note:
Hayo yote niliyoandika ni kwa uzoefu wangu binafsi, nimewahi kufanya kazi na mashirika hayo miaka kadhaa kwa ngazi ya chini, na huenda nikaendelea kufanya nao kwa miaka mingine kadhaa ikiwa nitafanikiwa kupanda ngazi ya juu zaidi.
 
Tatizo nadhani liko hapa. Hawa jamaa kama wamepewa madaraka ya kuchuja waombaji basi upeleka watu wao tu. Kama hawakujui, haupelekwi. SADC ndio wana mtindo huo. Wanataka maombi yapitie Wizara ya mambo ya Nje ya nchi yako. Hata mimi nimewahi kuomba kupitia Mambo ya Nje mara nyingi bila mafanikio. Ila nikiomba kwenye mashirika ambayo yanapokea maombi moja kwa moja kutoka kwa waombaji huwa napata interviews.

Kwa ujumla wake, mashirika haya ni very competitive. Siyo rahisi kupata kazi huko. Hiyo haina maana kuwa haiwezekani. Unashindanishwa na dunia nzima - waliosoma international school, wanaongea international languages kama mother tongue, etc. Unashindana na the best of the best. Cha muhimu endelea kuomba. Ili upate interview 1 inabidi uwe umeomba mara nyingi sana. Ndio uzoefu wangu huo.

Asante.

Mpaka Leo naendelea kupambana.

#YNWA
 
Kukusaidia tu, fahamu haya:

1. Hakuna shirika lolote la kimataifa litataka kuajiri mtu kutoka halmashauri au mwenye uzoefu wa kazi za halmashauri. Kwanini? Utendaji wa kazi za halmashauri kwa sehemu umejaa siasa, ubabaishaji (unprofessional) na ushamba (poor exposure). Hivyo uzoefu wako wa kazi za halmashauri ni kikwazo cha kukosa kazi za kimataifa moja kwa moja.

2. Elimu pekee sio kigezo cha kupata kazi kwenye mashirika ya kimataifa. Kwa sasa hapa Tz, watu wenye elimu ngazi ya masters wapo wengi mnoo, na wote wanasikilizia kupata kazi popote. Ukienda Kenya ndio unaweza ukaogopa hata kusema kuwa una Masters, maana graduates wa masters kwao ni kama graduates wa undergraduate hapa Tz. Mashirika ya kimataifa yanataka Elimu mahususi+Uzoefu mahususi.

3. Ajira nyingi za mashirika ya kimataifa ni ajira za mkataba na mahususi, yaani zinalenga jambo fulani kwa muda fulani. Zinamfaa sana mtu special katika uzoefu wa jambo fulani na huru kiajira (freelancer). Kwako sidhani sana kama zinakufaa au utawafaa, unapoteza muda wako au kuwapotezea muda.

4. Mambo ya msingi sana ya kufanya ukitaka kupata kazi za mashirika ya kimataifa.
-Jitahidi ufanye kazi na mashirika yoyote binafsi yenye mtandao wa kimataifa yaliyopo hapa hapa Tanzania.

-Jitahidi upate nafasi ya kuishi au kufanya kazi nje ya Tanzania. Kama huna exposure ya nje ya Tanzania, kuzipata hizo kazi ni ngumu na ukipata hiyo kazi itakutesa sana.

-Onyesha uzoefu wako kwa kusimamia kazi yoyote mahususi itakayoweza kutambulisha ujuzi wako kimataifa.

Note:
Hayo yote niliyoandika ni kwa uzoefu wangu binafsi, nimewahi kufanya kazi na mashirika hayo miaka kadhaa kwa ngazi ya chini, na huenda nikaendelea kufanya nao kwa miaka mingine kadhaa ikiwa nitafanikiwa kupanda ngazi ya juu zaidi.

Sasa baharia unataka kuniambia wewe ulitoka tu chuo ukapata Kazi kwao?

Nipe ile mbinu uliyotumia ulivyotoka chuo ukapata Kazi kwao.

#YNWA
 
Back
Top Bottom