sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,021
- 5,253
Barua hata ikisainiwa na ofisa elimu kama mkurugenzi haja ipitisha ni kazi bure kwa sababu mkurugenzi mdio mwajiri wako na ndio bosi wako namba moja. Hivyo kama ulienda ni dhahiri ulikiuka taratibu
Pili kitendo cha kuto pata mshahara na salary slip zikawa zinakuja pia nalo ni tatizo sababu inaonesha hazina inatuma pesa na bado inatambua kuwa wewe ni mtumish wa umma ,kwenye pesa hapo kuna usanii, kuna mtu ana access acount yako kinyume cha sheria.
Kuhusu kuto pewa barua ya kusimamishwa nalo ni kosa sababu pasipo barua halali wewe bado ni mtumishi na kwa kigezo hicho cha mshahara wako kuendelea kutoka ni dhahiri hawana pa kujificha.
Mshahara haufanyi mtu kuwa mtumishi halali, hapo linakuwa ni kosa la hao watu wa utumishi au fedha kutopeleka taarifa hazina ili mshahara huo usitishwe.. Na hiyo ndio inayoitwa mishahara kwa watumishi hewa, ni sawa na mtumishi anaelipwa nusu mshahara sababu ya kuwa na kesi ya kitumishi labda, mshahara wake huwa unakuja wote kutoka hazina lakini mwajiri anampa nusu wakati akisubiri maamuzi ya kesi yake, akishinda mtumishi basi atalipwa nusu zake zote na akishindwa zile nuzu zote zitatakiwa kurudishwa hazina..kwa hiyo ishu ya mshahara hapa ndo yale mambo ya utumishi hewa haimfanyi mlalamikaji kuwa mtumishi halali automatically..