Mtumishi unakosa nyumba , magari na maisha bora ! Si ujilipue kwenye mshahara wako ?

Wenye akili wamekuelewa Mkuu uko sahihi kabisa.
NMB, Benki ya Zanzibar na Serikali kupitia Hazina wanatoa Mikopo mpaka Mil.75 kwa wafanyakazi lkn wafanyakaz wengi wanaishi kama alivyoeleza mleta mada sijui wana shida gani kisa tu kujisifu kwamba mishahara yao haikatwi mikopo. Amazing
watumishi wa umma mathalani walimu hakuna mshahara unaowawezesha kukopa milioni 75 hakuna mikopo yao inaishia m 13 mpk 20 labda misufuria lakini sio mikopo
 
watumishi wa umma mathalani walimu hakuna mshahara unaowawezesha kukopa milioni 75 hakuna mikopo yao inaishia m 13 mpk 20 labda misufuria lakini sio mikopo
Weee boya kweli yaaan, kwahiyo mwalimu ndio umeona kuwa ana mshahara usioweza kukopa Mil zaidi ya 20?? Rudi kasome upya ngaz za mishahara na MU za mabenki za mikopo utalewa
 
Weee boya kweli yaaan, kwahiyo mwalimu ndio umeona kuwa ana mshahara usioweza kukopa Mil zaidi ya 20?? Rudi kasome upya ngaz za mishahara na MU za mabenki za mikopo utalewa
Narudia tena hakuna mshahara wa mwalimu unaomruhusu kukopa 75m na akabakiwa na 3/4 ya mshahara
 
Kwanza ujue m75 ndio hela wanayochukua baada ya kufanya kazi miaka 30 sasa mikopo yao ya nmb inalipwa ndani ya 5-6 yrs hawawezi kukopesheka 75m kuwa mwelewa
 
Ili MTU aweze kukopesheka m75 nilazima mshahara wake uweze kukatwa milioni moja na arobaini elfu kila mwezi kwa miezi 72 na kumbuka hiyo ndio 1/3 sasa mwalimu gani ambae milioni moja na arobaini ndio theluthi ya mshahara wake unaota wewe
 
Mtu analipwa mshahara mpaka laki 9 ( take home ) lakini unaishi kijinga jinga kama mkimbizi. Why usikope hata Mil 15 huko ubadilishe maisha yako ? Kula nyama mpaka mganga aseme."" Maisha yanategemeana
 
Usitukane Mkunga uzazi ungalipo.

Usitukane mamba hujavuka MTO.

Hujafa hujaumbika.

Wahenga hawakoseagi mnama.
 
Mkopo usikieni tu ndugu zanguni

nilikopa 1M mwaka jana asee kuja kugundua narudisha kama 2M asee nilijuta, SITAKI KUSIKIA MKOPO
 
Haya maisha yana mambo mengi ndugu, unaweza kukopa hiyo 15 mil na ikaisha usijue imefanya kazi gani, cha muhimu ni kumtegemea muumba zaidi.
 
Back
Top Bottom