Mpitagwa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2012
- 2,339
- 1,119
Mtumishi mwandamizi wa serikali ya Tanzania, kwenye kitengo cha kurusha ndege za rais mzee Kileo, leo amefukuzwa kwenye nyumba aliyopewa na serikali kuanzia mwaka 1972.
Akiongea na Channel 10 kwa uchungu mzee Kileo amelalamika kuwa amekuwa rubani mwadilifu akirusha ndege za marais wote waliopita na sasa ni mshauri wa rais kwenye masuala ya anga amesikitishwa sana na kutolewa vifaa nje ya nyumba kunakofanywa na kampuni ya udalali kwa idhini ya mahakama. Amedai wenzake waliokimbia serikalini sasa ni matajiri wa kutupwa wengine wakimiliki meli na wengine ndege. Yeye aliyevumilia ndoo yanamkuta haya.
Dalali mwenye kazi hiyo amedai kuwa amepewa kazi ya kuvunja nyumba hiyo na benki ya TIB ambao wanataka kutumia eneo hili kwaajili ya ujenzi wa Benki ya Wakulima.
Changamoto, nani atakubali kuwa mtumishi mwaminifu ili baadaye yaje yamkute haya ya mzee Kileo? Kitendo kama hiki hakichangii tabia ya ufisadi na rushwa serikalini ili watu wachukue chao mapema?