Mtumishi kusoma imekuwa anasa siku hizi

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Vikwazo vimekuwa vingi mno

1. Walianza kusema ukienda kusoma lazima akasome fani yako. Kama wewe ni mhasibu lazima ukasomee mambo hayo sio udaktari

2. Kama hiyo haitoshi wakaja na kigezo cha kujilipia ada ili mwajiri asilipe kama unataka ruhusa. Wakati huo kila mwajiri anatenga bajeti ya kuendeleza watumishi wake.

3. Hiyo haikutosha wakaja na kigezo cha daraja. Ukienda masomoni hutapanda daraja hadi urudi na kutumikia elimu yako kwa miaka 3.
Katiba imetoa Uhuru kwa mtu yeyote kujiendeleza kwa fani yeyote atakayopendezwa nayo.

Serikali inachukulia watumishi kujiendeleza ni anasa. Mama Samia ingia na huku ili hivi vigezo visivyo na msingi viondolewe.
 
Mtumishi kusoma sana Ni upuuzi, reCategorization na increment zinatoka kiitikadi zaidi.

Serikali inatambua degree Moja,hizo nyingine Ni mbwembwe

Tumia nafas iyo iyo ulokua nayo Apo hapo kujiongezea icho kipato Cha ziada .
 
Huwa nashangaa Sana,
Eti mtumish unaingia benki kukopa mil 15 au mil 30 kwenda kusoma.

Afu ukirudi masomoni,
Unaanza kulamba watu miguu uongezewe mshahara.
 
Mnasoma kwa faida zenu,, mkumbuke vijana wanamaliza wanahitaji ajira wanaishia kujiajiri.

Tena shukuru unapotea kazini miaka 3 bado nafasi ipo nashauri mamlakaziwasimamishe kazi pindi muwapi masomoini na mkirejea muanze na kuaply kbsa.


Maana mmezidi sasa huku mnasahau kuna jopo la wasomi mtaani alafu hicho cheo kazini bado mnalalama ovyo.
 
Wataishia kutengeneza taifa la ngumbaru, watu wenye Masters na PhD serikalini watakuwa wa kuhesabu......imagine taasisi ya utafiti imesheheni watu wenye bachelor degree, kutakuwa hakuna utafiti hapo ila utopolo.....
 
Back
Top Bottom