Mtumishi benki ya EXIM kamatwa na mamilioni ya wizi gesti

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
14,868
2,000
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtunza fedha wa Bank ya Exim Martin Lazaro Temu (33), kwa tuhuma za wizi wa Fedha Shilingi milioni 120, dola 9,513 na Euro 50 mali ya mwajiri wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema mtuhumiwa huyo baada ya tukio la wizi alitoroka na amekamatwa mkoani Singida katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Manonga.

Amesema mara baada ya kukamatwa kufuatia msako uliofanywa na Jeshi hilo walimkuta akiwa na fedha kiasi cha shilingi Milioni 37,522,000 ikiwa ni sehemu ya pesa alizoziiba na anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Pamoja na mtuhumiwa huyu ambaye alijificha mafichoni alipofanya wizi lakini tukamkamata pia yupo mtuhumiwa mwingine jina tunalihifadhi na msako mkali dhidi yake unaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria,” ameongeza Muroto.
Awali akizungimzia tukio la kwanza Kamanda Muroto amesema wanamshikilia Ashraf Abdalah Sani (31), aliyekutwa na gari aina ya Nissan yenye namba za usajili T793 CFT analoitumia katika uhalifu na kukutwa na vitu mbalimbali ambavyo ni rim 9 za gari, matairi matano, jeki 2 na spana akiwa maeneo ya Bahi Road jijini Dodoma.

“Mtuhumiwa ni mkazi wa Mwanza Nyakato na amefika hapa kwa shughuli za kiuhalifu na mbinu anayoitumia ni kwenda kwenye kumbi za starehe, mikutano au mikusanyiko ya watu kisha kuegesha gari yake pembeni mwa gari jingine na kufungua matairi na kuondoka nayo kwenda kuyauza sasa tumemkamata,” amefafanua Kamanda Muroto.
Katika tukio la tatu, Moroto amesema Polisi mkoani Dodoma inamshikilia Isack Martin Okwango (27), akiwa na vifaa vya uvunjaji ambavyo ni Jeki moja, bisibisi moja, simu za wizi tatu, camera moja, laptop moja, flash diski nne na kisu kimoja ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.

“Mtuhumiwa amekamatwa akiwa katika nyumba ya wageni eneo la Makole na ni mkazi wa Buzuruga Mwanza na Buguruni Dar es salaam, akiwa hapo lodge alijiandikisha kwa jina la bandia la Bill Martin tumemkamata na atafikishwa Mahakamani,” amesema.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Muroto ameitaka jamii na wamiliki wa nyumba za wageni kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha uhalifu.
Aidha amesisitiza wananchi kujitokeza katika vituo vya kujiandikisha kupiga kura ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini kote Novemba 24, 2019.
 

walitola

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
2,912
2,000
Duh kumbe alikuwa incharge wa cashier akaona isiwe tabuu kajipigia lakini misheni imefeli
Hata huyu dogo wa exim namfahamu...alikua branch ya tanga kabla ya kuhamishiwa Dom kama chief cashier....anamacho yenye malienge na big forehead...bahati mbaya sina picha yake humu.. ukimuona ni boya hivi ila ndo kashafanya yake
 

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
1,740
2,000
Kuiba kunahitaji mipango sio kukurupuka tu kama unaomba namba ya bar maid.

Unahitaji kujiandaa kisaikolojia.
wizi makini lazima uwe na exit plan kabla haujafanyika..

hawajasoma story ya boston bank robbery iliyoletwa humu jamvini...

unakuta mtu kama huyu ameiba hela halafu kaenda kujificha gesti huku ana simu yake ya mkononi au laini.. hajui simu zinasoma gps.. na pia hela zote kazibeba za nini kusafiri nazo?

hizo zinachimbiwa sehemu kisha anasepa na kiasi kidogo cha kumfikisha pa kujifichia.

magaidi wanakwambia sehemu safe ya mhalifu mkubwa kujificha ni karibu na makao makuu ya polisi, usalama wa taifa au makao makuu ya jeshi.. hata osama aliishi miaka zaidi ya 10 karibu na kambi kuu ya jeshi pakistan...
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,376
2,000
Duh kaiba pesa afu kaenda kujificha gest jamaa chizi kweli unaiba pesa dodoma afu unaenda kujificha bahi

Duh kweli akili kumkichwa kanikumbusha kuna jamaa alimpa mwanafunzi mimba huko kahama afu jamaa akaenda kujificha kagongwa
Wahalifu hawanaga akili
 

japotenda

Senior Member
Jan 9, 2020
122
225
wizi makini lazima uwe na exit plan kabla haujafanyika..

hawajasoma story ya boston bank robbery iliyoletwa humu jamvini...

unakuta mtu kama huyu ameiba hela halafu kaenda kujificha gesti huku ana simu yake ya mkononi au laini.. hajui simu zinasoma gps.. na pia hela zote kazibeba za nini kusafiri nazo?

hizo zinachimbiwa sehemu kisha anasepa na kiasi kidogo cha kumfikisha pa kujifichia.

magaidi wanakwambia sehemu safe ya mhalifu mkubwa kujificha ni karibu na makao makuu ya polisi, usalama wa taifa au makao makuu ya jeshi.. hata osama aliishi miaka zaidi ya 10 karibu na kambi kuu ya jeshi pakistan...
watu wanapata chance wanashindwa kutumia
 

permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
3,994
2,000
Raising capital by stealing??? Hahaa waandishi wa vitabu baadhi wanapotosha vijana,

But remember You will shorten your life.
Nchi nyingi za Ulaya wakati wa merchantalism zilipata mtaji kutokana na "looting and plundering ", hii ndio maana Carl Marx katika "Das Capital"anasema hivyo. Hivi unawakumbuka Wachina na reli ya kati??
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,323
2,000
Namkumbuka pia....alikua anachkua hela za bank anampa mme wake azungushe afu mme wake akashindwa kurudisha zile pesa ikabidi wafanye mchongo wakakodi watu kufanya kama tukio la wizi wa bank ili ionekane pesa ziliibiwa....walifanikiwa kutengeneza tukio na polisi wakaamini ni bank robbery kweli badae staff mmoja wa palepale barclays ndio akachomoa betri akasema ukweli kwamba wakati inqfanyika bank robbery pesa zilikua zishaisha strongroom zilibaki chenjichenji tu.. ndio kisa cha yule dada kudakwa afu mmewe akalala mbele.
Watu wanoko sana duh
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom