Mtumishi benki ya EXIM kamatwa na mamilioni ya wizi gesti

Kisiwa Cha Harishi

Kisiwa Cha Harishi

JF-Expert Member
Jun 15, 2019
1,016
2,000
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtunza fedha wa Bank ya Exim Martin Lazaro Temu (33), kwa tuhuma za wizi wa Fedha Shilingi milioni 120, dola 9,513 na Euro 50 mali ya mwajiri wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema mtuhumiwa huyo baada ya tukio la wizi alitoroka na amekamatwa mkoani Singida katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Manonga.

Amesema mara baada ya kukamatwa kufuatia msako uliofanywa na Jeshi hilo walimkuta akiwa na fedha kiasi cha shilingi Milioni 37,522,000 ikiwa ni sehemu ya pesa alizoziiba na anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Pamoja na mtuhumiwa huyu ambaye alijificha mafichoni alipofanya wizi lakini tukamkamata pia yupo mtuhumiwa mwingine jina tunalihifadhi na msako mkali dhidi yake unaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria,” ameongeza Muroto.
Awali akizungimzia tukio la kwanza Kamanda Muroto amesema wanamshikilia Ashraf Abdalah Sani (31), aliyekutwa na gari aina ya Nissan yenye namba za usajili T793 CFT analoitumia katika uhalifu na kukutwa na vitu mbalimbali ambavyo ni rim 9 za gari, matairi matano, jeki 2 na spana akiwa maeneo ya Bahi Road jijini Dodoma.

“Mtuhumiwa ni mkazi wa Mwanza Nyakato na amefika hapa kwa shughuli za kiuhalifu na mbinu anayoitumia ni kwenda kwenye kumbi za starehe, mikutano au mikusanyiko ya watu kisha kuegesha gari yake pembeni mwa gari jingine na kufungua matairi na kuondoka nayo kwenda kuyauza sasa tumemkamata,” amefafanua Kamanda Muroto.
Katika tukio la tatu, Moroto amesema Polisi mkoani Dodoma inamshikilia Isack Martin Okwango (27), akiwa na vifaa vya uvunjaji ambavyo ni Jeki moja, bisibisi moja, simu za wizi tatu, camera moja, laptop moja, flash diski nne na kisu kimoja ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.

“Mtuhumiwa amekamatwa akiwa katika nyumba ya wageni eneo la Makole na ni mkazi wa Buzuruga Mwanza na Buguruni Dar es salaam, akiwa hapo lodge alijiandikisha kwa jina la bandia la Bill Martin tumemkamata na atafikishwa Mahakamani,” amesema.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Muroto ameitaka jamii na wamiliki wa nyumba za wageni kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha uhalifu.
Aidha amesisitiza wananchi kujitokeza katika vituo vya kujiandikisha kupiga kura ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini kote Novemba 24, 2019.
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
46,784
2,000
Mafanikio hayana shortcut na ukitaka shortcut utaambuka mapema sana
Hii imenikumbusha yule dada branch manager wa Barclay's Kino branch(Jina kpuni)
Walipiga Hela na mme wke.... Hesabu zikafeli
Mchongo waliyopanga ulienda syo

Ova
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
46,784
2,000
Uko sahihi kabisa Hawa vijana hawajui kabisa wanaiba wanakaa na mihelaa yote wakati watu wanakaa hata miaka 2 hawagusi hata Mia na wako mjini tu
Kna jamaa alipiga Hela kwenye kampuni moja ya sm Enzi hzo wanapiga
Kujua watu ilichkua Miaka
Jamaa kma fala ukimuona Mlokole Hvi
Utasema katoka shamba Leo kja mjini
Sahv a nakula pnshen tu

Ova
 
PETER PIERE

PETER PIERE

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
362
1,000
Wakijenga huku mitaan wanaitwa smart.. Haya wamsifie na hapo,
 
Edward Teller

Edward Teller

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
3,834
1,250
Bankers wengi wanalipwa kidogo..mishahara haiwatoshi..kila siku wanaona hela kwa nini tamaa zisiwaingie
 
Ligaba

Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
645
1,000
Duh kaiba pesa afu kaenda kujificha gest jamaa chizi kweli unaiba pesa dodoma afu unaenda kujificha bahi

Duh kweli akili kumkichwa kanikumbusha kuna jamaa alimpa mwanafunzi mimba huko kahama afu jamaa akaenda kujificha kagongwa
Ungekuwa mtihani naamini ungekuwa ushafeli.
 
T

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,048
2,000
Tamaa na kutaka maisha ya anasa kuna watesa wafanyakaz wa bank.
 
G

gen parton

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
614
250
Mtu unaiba milioni 140 dodoma unaenda gesti Singida
Watu wana IQ ndogo kweli, hapo ungeenda kujichimbia vijiji ambavyo bodaboda hazifiki , ukae huko angalau miaka 2 hadi soo lipoe kwanza, kisha unabadili jina na vitambulisho vyako unahamia mkoa wa mbali kabisa unaanzisha biashara

Kwa teknolojia ilivyokuwa siku hizi ukiiba inatakiwa umejipanga kukabiliana na system za polisi ama humalizi round
Sasa huyo abgetoboa umkute mtaani na tako la nyani mtaani mademu zetu wangekoma
 
maroon7

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
8,720
2,000
Hii imenikumbusha yule dada branch manager wa Barclay's Kino branch(Jina kpuni)
Walipiga Hela na mme wke.... Hesabu zikafeli
Mchongo waliyopanga ulienda syo

Ova
Namkumbuka pia....alikua anachkua hela za bank anampa mme wake azungushe afu mme wake akashindwa kurudisha zile pesa ikabidi wafanye mchongo wakakodi watu kufanya kama tukio la wizi wa bank ili ionekane pesa ziliibiwa....walifanikiwa kutengeneza tukio na polisi wakaamini ni bank robbery kweli badae staff mmoja wa palepale barclays ndio akachomoa betri akasema ukweli kwamba wakati inqfanyika bank robbery pesa zilikua zishaisha strongroom zilibaki chenjichenji tu.. ndio kisa cha yule dada kudakwa afu mmewe akalala mbele.
 
laii

laii

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
561
1,000
Watu mnataarifaa

Hata huyu dogo wa exim namfahamu...alikua branch ya tanga kabla ya kuhamishiwa Dom kama chief cashier....anamacho yenye malienge na big forehead...bahati mbaya sina picha yake humu.. ukimuona ni boya hivi ila ndo kashafanya yake
 
fred mwakitundu

fred mwakitundu

Senior Member
Dec 31, 2018
134
250
Wizi wa kishamba,kanikumbusha vijana wa kinyiramba waliiba pesa NBC Moshi wakaenda kufunga madishi na kununua TV kwenye nyumba za Tembe na jeneretor kila siku ni mziki tu,wakafukia pesa kwenye mfano wa kaburi,walikamatwa kama Kuku wa kideli.

mwingine wa pale Msambiazi Korogwe naye akachimba shimo chini ya kitanda na kuzifukia huko,naye akadakwa kama kuku aliyezongwa na utitiri hana pa kukimbilia,yaani huu wizi wa kishamba balaaaaa
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
11,705
2,000
Kna jamaa alipiga Hela kwenye kampuni moja ya sm Enzi hzo wanapiga
Kujua watu ilichkua Miaka
Jamaa kma fala ukimuona Mlokole Hvi
Utasema katoka shamba Leo kja mjini
Sahv a nakula pnshen tu

Ova
Aisee alitulia kama hana hata miaa
 
Msubhate

Msubhate

JF-Expert Member
May 11, 2012
1,051
2,000
Wanataka shortcut
Akili mawazo yao ni kununua tako la nyani na kutesa na mabebeiz
Alafu Mtaani utawaskia watu wanasema jamaa ni very smart kichwani

Ova
Kaka umepotea sana.
 
jaji mfawidhi

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
7,583
2,000
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtunza fedha wa Bank ya Exim Martin Lazaro Temu (33), kwa tuhuma za wizi wa Fedha Shilingi milioni 120, dola 9,513 na Euro 50 mali ya mwajiri wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema mtuhumiwa huyo baada ya tukio la wizi alitoroka na amekamatwa mkoani Singida katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Manonga.

Amesema mara baada ya kukamatwa kufuatia msako uliofanywa na Jeshi hilo walimkuta akiwa na fedha kiasi cha shilingi Milioni 37,522,000 ikiwa ni sehemu ya pesa alizoziiba na anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Pamoja na mtuhumiwa huyu ambaye alijificha mafichoni alipofanya wizi lakini tukamkamata pia yupo mtuhumiwa mwingine jina tunalihifadhi na msako mkali dhidi yake unaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria,” ameongeza Muroto.
Awali akizungimzia tukio la kwanza Kamanda Muroto amesema wanamshikilia Ashraf Abdalah Sani (31), aliyekutwa na gari aina ya Nissan yenye namba za usajili T793 CFT analoitumia katika uhalifu na kukutwa na vitu mbalimbali ambavyo ni rim 9 za gari, matairi matano, jeki 2 na spana akiwa maeneo ya Bahi Road jijini Dodoma.

“Mtuhumiwa ni mkazi wa Mwanza Nyakato na amefika hapa kwa shughuli za kiuhalifu na mbinu anayoitumia ni kwenda kwenye kumbi za starehe, mikutano au mikusanyiko ya watu kisha kuegesha gari yake pembeni mwa gari jingine na kufungua matairi na kuondoka nayo kwenda kuyauza sasa tumemkamata,” amefafanua Kamanda Muroto.
Katika tukio la tatu, Moroto amesema Polisi mkoani Dodoma inamshikilia Isack Martin Okwango (27), akiwa na vifaa vya uvunjaji ambavyo ni Jeki moja, bisibisi moja, simu za wizi tatu, camera moja, laptop moja, flash diski nne na kisu kimoja ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.

“Mtuhumiwa amekamatwa akiwa katika nyumba ya wageni eneo la Makole na ni mkazi wa Buzuruga Mwanza na Buguruni Dar es salaam, akiwa hapo lodge alijiandikisha kwa jina la bandia la Bill Martin tumemkamata na atafikishwa Mahakamani,” amesema.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Muroto ameitaka jamii na wamiliki wa nyumba za wageni kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha uhalifu.
Aidha amesisitiza wananchi kujitokeza katika vituo vya kujiandikisha kupiga kura ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini kote Novemba 24, 2019.
dogo wa IFM huyu, anatumia fedha kwa mademu, sasa amekamatwa.
Ile nyumba aliyojenga Goba ichukuliwe iwe ya serukali.
Pia muroto umejifunza saa hi hautumii tena ma press na nguo za kwendea field, dah kumbe lile neno la IGP lilikuingia japo linauma
 
Top Bottom