Mtumishi benki ya EXIM kamatwa na mamilioni ya wizi gesti

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
14,946
2,000
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtunza fedha wa Bank ya Exim Martin Lazaro Temu (33), kwa tuhuma za wizi wa Fedha Shilingi milioni 120, dola 9,513 na Euro 50 mali ya mwajiri wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema mtuhumiwa huyo baada ya tukio la wizi alitoroka na amekamatwa mkoani Singida katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Manonga.

Amesema mara baada ya kukamatwa kufuatia msako uliofanywa na Jeshi hilo walimkuta akiwa na fedha kiasi cha shilingi Milioni 37,522,000 ikiwa ni sehemu ya pesa alizoziiba na anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Pamoja na mtuhumiwa huyu ambaye alijificha mafichoni alipofanya wizi lakini tukamkamata pia yupo mtuhumiwa mwingine jina tunalihifadhi na msako mkali dhidi yake unaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria,” ameongeza Muroto.
Awali akizungimzia tukio la kwanza Kamanda Muroto amesema wanamshikilia Ashraf Abdalah Sani (31), aliyekutwa na gari aina ya Nissan yenye namba za usajili T793 CFT analoitumia katika uhalifu na kukutwa na vitu mbalimbali ambavyo ni rim 9 za gari, matairi matano, jeki 2 na spana akiwa maeneo ya Bahi Road jijini Dodoma.

“Mtuhumiwa ni mkazi wa Mwanza Nyakato na amefika hapa kwa shughuli za kiuhalifu na mbinu anayoitumia ni kwenda kwenye kumbi za starehe, mikutano au mikusanyiko ya watu kisha kuegesha gari yake pembeni mwa gari jingine na kufungua matairi na kuondoka nayo kwenda kuyauza sasa tumemkamata,” amefafanua Kamanda Muroto.
Katika tukio la tatu, Moroto amesema Polisi mkoani Dodoma inamshikilia Isack Martin Okwango (27), akiwa na vifaa vya uvunjaji ambavyo ni Jeki moja, bisibisi moja, simu za wizi tatu, camera moja, laptop moja, flash diski nne na kisu kimoja ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.

“Mtuhumiwa amekamatwa akiwa katika nyumba ya wageni eneo la Makole na ni mkazi wa Buzuruga Mwanza na Buguruni Dar es salaam, akiwa hapo lodge alijiandikisha kwa jina la bandia la Bill Martin tumemkamata na atafikishwa Mahakamani,” amesema.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Muroto ameitaka jamii na wamiliki wa nyumba za wageni kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha uhalifu.
Aidha amesisitiza wananchi kujitokeza katika vituo vya kujiandikisha kupiga kura ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini kote Novemba 24, 2019.
 

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,803
2,000
Mtu unaiba milioni 140 dodoma unaenda gesti Singida
Watu wana IQ ndogo kweli, hapo ungeenda kujichimbia vijiji ambavyo bodaboda hazifiki , ukae huko angalau miaka 2 hadi soo lipoe kwanza, kisha unabadili jina na vitambulisho vyako unahamia mkoa wa mbali kabisa unaanzisha biashara

Kwa teknolojia ilivyokuwa siku hizi ukiiba inatakiwa umejipanga kukabiliana na system za polisi ama humalizi round
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
12,984
2,000
Hapo majuzi alikamatwa mfanyakazi CRDB, Leo EXIM, hawa vijana si wafanye kazi, tamaa za nini.

Naisi wanapofunga hesabu ya siku fedha zilizopo wanazimezea mate na kuzitamani
Wanatamani kusukuma matako ya nyani wangali vijana
 

abdi ally

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
1,575
2,000
Halafu walivyo wapumbavu wakiiba wanaishia kupiga misele ya ovyo Dar Mbeya Mwanza Arusha!

Wanaiba wakiwa hawana malengo pambaff kbsa hawa
Hawana plann kabisa yaan unaiba huku unatumia lain ya simu ya tz dadek lazima udakwe tu
 

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
12,146
2,000
Duh kaiba pesa afu kaenda kujificha gest jamaa chizi kweli unaiba pesa dodoma afu unaenda kujificha bahi

Duh kweli akili kumkichwa kanikumbusha kuna jamaa alimpa mwanafunzi mimba huko kahama afu jamaa akaenda kujificha kagongwa
Wakamnyakaaa...!!Akapigwa miaka 30
 

abdi ally

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
1,575
2,000
wizi makini lazima uwe na exit plan kabla haujafanyika..

hawajasoma story ya boston bank robbery iliyoletwa humu jamvini...

unakuta mtu kama huyu ameiba hela halafu kaenda kujificha gesti huku ana simu yake ya mkononi au laini.. hajui simu zinasoma gps.. na pia hela zote kazibeba za nini kusafiri nazo?

hizo zinachimbiwa sehemu kisha anasepa na kiasi kidogo cha kumfikisha pa kujifichia.

magaidi wanakwambia sehemu safe ya mhalifu mkubwa kujificha ni karibu na makao makuu ya polisi, usalama wa taifa au makao makuu ya jeshi.. hata osama aliishi miaka zaidi ya 10 karibu na kambi kuu ya jeshi pakistan...
Uko sahihi kabisa Hawa vijana hawajui kabisa wanaiba wanakaa na mihelaa yote wakati watu wanakaa hata miaka 2 hawagusi hata Mia na wako mjini tu
 
  • Thanks
Reactions: Ctr

abdi ally

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
1,575
2,000
Uzembe wake umemkamatisha. Hela kama hizo unatakiwa usiwasiliane na ndugu zako kamwe....

Ila alama za vidole zitasababisha wezi wakamatwe sana maana hata ukitupa laini bado itasoma fulani yupo hewani
Unatakiwa kuishi bila network access ya Aina yeyote ile na unatakiwa baada ya kuiba tu uwe na plan kabisa ya kutoka na Kama hauna nawashauri msiibe bora uwe masikini

Na Kama unaiba Basi unajua point zote za kutokea

" Katika panya Mia panya muerevu Yuko mmoja tu ambae anajua matundu meng ya kutokea" huu msemo Ni rahis na mgumu kuuelewa ila kwa wapigaji washaelewa
 

abdi ally

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
1,575
2,000
Ni amart usipikamatwa....
kuna njia nyingi sana za kutafuta hapa chini ya jua...
Binafsi siamini katika huo mfumo wa wizi
Wiz Ni win and loose situation tu ukicheza vizuri umewini tatizo plan zetu za wizi tunapanga wiki ndio tuibe panga plan miez na miaka ukipiga wanajua hapa tumepigwa kitaaluma kabisa
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
21,753
2,000
Hapo majuzi alikamatwa mfanyakazi CRDB, Leo EXIM, hawa vijana si wafanye kazi, tamaa za nini.
Naisi wanapofunga hesabu ya siku fedha zilizopo wanazimezea mate na kuzitamani
Janga Kubwa Sana Vijana Sijui Tunakwama Wapi Hadi Tunakuwa Na Akili Kama Nyani
Yaani Ukiingia Kwenye Shamba La Mahindi Unakula Heka Nzima Leo Leo Bila Kufikiria Kesho

Watu Wanatunza Akiba Yeye Anajibebea Anakimbia
 

cmoney

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
2,796
2,000
Ah ah wanasema asilimia 80 ya wezi wa mabank hukamatwa kipindi cha matumizi
.....you got be able to lay low until heat is down or else you are going to leave a papertrail
 

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
3,446
2,000
Wanataka shortcut
Akili mawazo yao ni kununua tako la nyani na kutesa na mabebeiz
Alafu Mtaani utawaskia watu wanasema jamaa ni very smart kichwani

Ova
Mafanikio hayana shortcut na ukitaka shortcut utaambuka mapema sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom