Mtumishi anapokutwa na hatia katika makosa ya jinai

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Wanabodi, habari.

Ndugu yangu ni mtumishi Wa Umma. Alikuwa na kesi ya jinai ya kumtukana mtu. Kesi imeenda mahakamani na mahakama imempiga faini. AMELIPA. Mwajiri wake amepelekewa taarifa kuwa, mtumishi wake amekutwa na hatia.

Je, haki yake ni ipi kazini?

Nimeuliza hivyo hasa kwa kuwa, wapo watu wanasema Mtumishi Wa Umma akikutwa na hatia mahakamani, basi utumishi wake unakuwa umekoma na wengine wanasema, hapana. Kama amelipa faini basi anaendelea na kazi yake kama kawaida.

Majibu yakiambatana na sheria na vifungu vyake itafaa zaidi
 
Screenshot_2022-11-30-09-02-48-578-edit_com.adobe.reader.jpg
 
Kuna code of ethics na kuna code of conduct.
Alipaswa kuwa mwadilifu siku zote za utumishi wake. Tukisimamia miongozo na kanuni za utumishi wa umma, tunamla kichwa.
Basi nusu ya waajiriwa wangekuwa wanafukuzwa kazi...

Tena ukifanya kosa la jinai mtaani lakini usiwekwe jela, basi wala taarifa zako hazitafika kazini, ila ukifungwa ndiyo kunakuwa na consequences kazini kwako.

Ukifanya kosa la jinai kazini ndiyo unachukuliwa hatua, ila huko mtaani we jitahidi usifungwe tuu.
 
Nadhani miongozo hiyo ndio inatakiwa iwekwe humuwatu wapate kuitumia
 
Back
Top Bottom