Mtumishi anaevaa sare za chama akiwa ofisini na mtu anaendesha vikao vya chama Ikulu, wana tofauti?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,983
Sheria za utumishi wa umma kwa ufahamu wangu haziruhushu mtumishi wa umma kuingia kazini/ofisini akiwa amevaa sare za chama fulani cha siasa au kuwa na chochote chenye muelekeo huo.

Sasa watu wanaofanya kikao cha chama Ikulu tena muda wa kazi,wana tofauti gani na mtumishi atakaeamua kuingia kazini na sare za chama fulani cha siasa?

Mliposema watu wafanye kazi mpaka mkazuia mikutano ya kisiasa huku nyinyi mkifanya vikao vya chama Ikulu tena muda wa kazi tuwaeleweje?
 
CDM5.jpg

Hao walioko Ikulu wamevaa sare za migambo au chadema.
 
CDM5.jpg

Hao walioko Ikulu wamevaa sare za migambo au chadema.
Hao sio watumishi wa umma na walikwenda Ikulu kama chama cha siasa kuhusu swala la kitafa(katiba) lililokuwa linasimamiwa na serikali na wao chama cha siasa wakiwa ni wadau.

Hawakwenda pale kujadili swala la kuchagua viongozi wa CHADEMA au kupanga safu ya uongozi wa chama.
 
Sheria za utumishi wa umma kwa ufahamu wangu haziruhushu mtumishi wa umma kuingia kazini/ofisini akiwa amevaa sare za chama fulani cha siasa au kuwa na chochote chenye muelekeo huo.

Sasa watu wanaofanya kikao cha chama Ikulu tena muda wa kazi,wana tofauti gani na mtumishi atakaeamua kuingia kazini na sare za chama fulani cha siasa?

Mliposema watu wafanye kazi mpaka mkazuia mikutano ya kisiasa huku nyinyi mkifanya vikao vya chama Ikulu tena muda wa kazi tuwaeleweje?
Licha ya Ikulu kuwa Ofisi ya Rais lakini ndio makazi yake pia.

Kwa watu wenye uelewa kama wako hata akiwa Off kazini mtajua yuko kazini kwa sababu umemuona Ikulu.

Kuhusu vikao, hata Mzee Lowasa huwa anahost vikao fulani fulani vya Chama nyumbani kwake

Ikulu sio sawa kwenu ambapo hamuwezi kuhost hata vikao vya harusi.

RAIS si sawa na Baba yako, hata akiwa mwenyekiti wa kamati ya harusi ni lazma aende ukumbini.

Mwisho kwa kuwa umeanza kwa kurejea Sheria ya utumishi wa Umma ni vema kama ungesema ni sheria ipi Rais ameivunja, vinginevyo post yako ni chuki dhidi ya Utawala.
 
Kwa mfano chama cha CCM kikiamua kwenda kutoa msaada kwenye shule fulani ni kosa kuvaa sare zake??!. Je, Mkuu wa shule kuwaita wana CCM amevaa sare za chama unadhani si kosa kisheria???. Tatu, chukulieni kuwa Mkuu wa shule hiyo hajavaa sare akawaalika wanaCCM kwenye shule hiyo na lengo la kikao ni kujadili maendeleo ya chama tu na si vingine na wakafanyia ofisi ya Mkuu wa shule, nyie mnaonaje???

Ukiweza kujibu maswali hayo bila uchama kuuuweka utajua ukweli kama ni ruksa kuendesha kikao cha chama ikulu ya Tanzania.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom