Mtumishi anaevaa sare za chama akiwa ofisini na mtu anaendesha vikao vya chama Ikulu, wana tofauti?

Inaelekea wanajamvi wengi humu hawajafanya kazi seikalini ama bado watoto wa shule maana hoja nyingi za kisiasa hasa za upinzani huwa hazina mashiko ama uelewa wao mdogo poleni kulalama
 
Sheria za utumishi wa umma kwa ufahamu wangu haziruhushu mtumishi wa umma kuingia kazini/ofisini akiwa amevaa sare za chama fulani cha siasa au kuwa na chochote chenye muelekeo huo.

Sasa watu wanaofanya kikao cha chama Ikulu tena muda wa kazi,wana tofauti gani na mtumishi atakaeamua kuingia kazini na sare za chama fulani cha siasa?

Mliposema watu wafanye kazi mpaka mkazuia mikutano ya kisiasa huku nyinyi mkifanya vikao vya chama Ikulu tena muda wa kazi tuwaeleweje?
Siku izi umekuwa pungu auni hivi
 
Haya ndo majibu

Haya ndo majibu ambayo yana nia ya kujenga na si kubomoa, wengine hata ukiuliza swali la msingi wanawaza uchama tu. Hongera sana kwa majibu haya hata kama si kweli au kweli but umejibu kwa ufasaha.
Nilichojifunza ni kuwa baadhi ya wakererketwa, wafurukutwa na wanachama wa vyama vya kisiasa nchini wanasahau kwamba madhara ya matendo maovu ya viongozi wa nchi humkumba kila mtanzania, na uongozi na siasa safi ni faida kwa ustawi wa nchi nzima.
 
Yes, but you don't get it.... umeweka picha za watu wa Chadema wakiwa wamevaa mavazi ya kaki. Swali langu lilikuwa: Ulifikiri mavazi hayo ni ya chama? yaani rangi ya kaki ni rangi ya Chadema kama ilivyo kijani waliyovaa CCM?
Mm nmeelewa kuwa hao ni wanachama chama cha scouts
 
Pamoja na kuwa ni makazi pia ya rais, alipaswa kuendesha vikao nje ya muda wa kazi! Rais ameendesha kikao cha chama ndani ya muda wa kazi jambo ambalo ni kosa
Kwa uwezo wako wa kufikiria M/kiti wa CCM Taifa atakuwa anafanya vikao vya chama Jumapili??

Halafu kule kazini huwa hamna off?

Rais akiwa hofu kwa majukumu mengine lazima uone barua iliosainiwa na Msigwa
 
Kiufupi raisi alipaswa kuonesha mipaka ya chama na serikali Kama alivyowahi kusema mwandishi mmoja katika makala yake kwenye gazeti fulani kuwa chama tawala na serikali ni sawa na shule ya bweni ya wasichana na wavulana kuwa wanapaswa kuchanganyika ktk shughuli mbalimbali lakini lazima mchanganyiko huo lazima uwe na mipaka.Bila ya kuwepo mipaka shule husika haitakuwa shule tena bali ni balaa au majanga
 
Hapo ilikuwa Raisi kikwete kakutana na uongozi wa chadema, leo Raisi Magufuli kakutana na uongozi wa CCM tabu iko wapi. Mwambieni Mbowe amlete Ben na si kulia lia.
Watu wanaweza kudhani umemtaja Ben kwa dhihaka lakini wengine tunafahamu kuwa hautanii kwani pamoja na chuki zako kwake lakini uhawara haufi.
Alikuacha lakini huwa unakumbuka mahanjamu wakati mwingine
 
Licha ya Ikulu kuwa Ofisi ya Rais lakini ndio makazi yake pia.

Kwa watu wenye uelewa kama wako hata akiwa Off kazini mtajua yuko kazini kwa sababu umemuona Ikulu.

Kuhusu vikao, hata Mzee Lowasa huwa anahost vikao fulani fulani vya Chama nyumbani kwake

Ikulu sio sawa kwenu ambapo hamuwezi kuhost hata vikao vya harusi.

RAIS si sawa na Baba yako, hata akiwa mwenyekiti wa kamati ya harusi ni lazma aende ukumbini.

Mwisho kwa kuwa umeanza kwa kurejea Sheria ya utumishi wa Umma ni vema kama ungesema ni sheria ipi Rais ameivunja, vinginevyo post yako ni chuki dhidi ya Utawala.

Still bado uwezo wako wa kutoa hoja umeachwa mbali sana na mto hoja..Muwe mnajikita kwenye hoja coz ndio kitu pekee kitakachokufanya uthink critically na kuacha hizi bra braaa..
 
Back
Top Bottom