KERO Mtumishi akihoji kuhusu stahiki zake tu Sabasaba Health Center anahamishwa

KERO Mtumishi akihoji kuhusu stahiki zake tu Sabasaba Health Center anahamishwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
"Mimi ni mtumishi hapa Kituo cha Afya Sabasaba Health Center, Morogoro. Ningependa kueleza kero kubwa inayotuumiza na inayohitaji uchunguzi wa dharura kutoka mamlaka za juu.

Ndani ya kituo chetu, kuna uonevu unaoendelea; watumishi wote wanaothubutu kuhoji au kudai haki na stahiki zao za msingi wanashughulikiwa kwa kuhamishwa vituo vya kazi. Hatua hii ya kukomoana inarudisha nyuma na kuzotesha sana utendaji kazi wetu wa kila siku.

Mfano halisi ni kwenye idara yetu ya upasuaji. Wataalamu wa kutoa dawa za usingizi (Anaesthetists) wamehamishwa kwa mtindo huu huu wa kuandamwa baada ya kudai stahiki zao, na matokeo yake sasa wamebaki wawili tu kituo kizima!

Hali hii inasababisha kuzorota kukubwa kwa utoaji wa huduma. Hawa wataalamu wawili waliobaki wanalemewa na mzigo mkubwa wa kazi na kuchoka kupitiliza, jambo ambalo ni hatari kwa usalama na maisha ya wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa dharura.

Tunaomba Serikali ije ifanye uchunguzi hapa Sabasaba, kwani kudai haki kusiwe kigezo cha mtumishi kuhamishwa."
 
Mfano halisi ni kwenye idara yetu ya upasuaji. Wataalamu wa kutoa dawa za usingizi (Anaesthetists) wamehamishwa kwa mtindo huu huu wa kuandamwa baada ya kudai stahiki zao, na matokeo yake sasa wamebaki wawili tu kituo kizima!
Mmebaki wawili? Mkuu hujajichoma kweli hapa?
 
Back
Top Bottom