Mtume Mwamposa: Kama kuna mahali umeambiwa ukija Kawe hatukuziki, Waambie asante sitakufa sasa

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Wakuu,

Hayo ni maneno yaliyosemwa na Mtume Mwamposa(Bulldozer) katika ibada ya kwanza Jana Jumapili tarehe 29.05.2022. ambapo alisema;

Najua watu wengi wanafuatilia ibada mikoa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

"Kama kuna mahali umezuiwa,umeambiwa ukienda Kawe hatukuziki usiogope kufa,waambie Asante kwa sababu sitakufa sasa.

Kwanza mtu anaekwambia ukifa hatukuziki,anakuingizia hofu ya kifo na anataka ufe mapema.

Na wakikataa kukuzika nitatoa namba za simu kwenye radio na TV na kutakuwa na timu utazikwa vizuri sana popote pale.
Usiogope kutishwa,unajua Kiongozi unaweza kudhani unawasaidia watu kumbe ndio unawaua.

Nachosema,Mimi Mungu amenituma kwa ajili ya watu wa dini zote na lazima nikusaidie,Usiogope kutishwa,Nataka nikupe maandiko yatakayokusaidia kutoka kwenye Bibilia Yohana 9:8 na kuendelea(msomaji anasoma)

Yohana 9
8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba?

11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.

12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.

13 Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani.

14 Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho.

15 Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.

16 Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao.

17 Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.

18 Basi Wayahudi hawakusadiki habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hata walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona.

19 Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa?

20 Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu;

21 lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe.

22 Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.

23 Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.

24 Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi.

Mtume akaendelea;

"Hapa kuna kipofu aliponywa na Yesu akaanza kuona,ilikuwa siku ya sabato.Wakampeleka kwa Mafarisayo wakaanza kumhoji jinsi gani ameponywa,akawaambia.

Baadae Mafarisayo wakasema bila shaka mtu huyu(Yesu) hakutoka kwa Mungu kwa sababu haishiki sabato.

Mara nyingi miujiza au nguvu za Mungu hazifuati au zinaweza zisiendane na kanuni za dini yako. Nguvu za Mungu zina kanuni zake.

Aliyetema mate ni nani?(Yesu)Aliyempaka tope la mate ni nani?(Yesu) Aliyemwambia kanawe Siloamu ni nani (Wanajibu Yesu).

Basi Mafarisayo wakasema mtu huyu(Yesu) hatoki kwa Mungu,wengine wakasema ni mwenye dhambi.

Sasa namimi nawauliza kati ya Yesu na Mafarisayo nani katoka kwa Mungu?Je Yesu hatoki hatoki kwa Mungu?

Nakupa misingi ya nguvu za Mungu zinavyofanya kazi,njia zake sio njia za watu.

Sasa kati ya Yesu na dini au Sinagogi kipi cha muhimu?

Hapa tunaona hata wazazi wa huyu kipofu washindwa kukiri kwamba ni Yesu ndiye kamponya mwanao kwa hofu ya kutengwa na dini yao.

Nimejisikia nikufundishe hiki kitu,kitakusaidia kwenye maisha yako.

Tarehe 9 nitakuwa Tunduma na tayari timu ipo kule,watu kutoka Congo,Zambia na nchi jirani na mikoa jirani watafika.

Na nikikasirika nikitoka huko natua Mbeya mjini au Songea au narudi tena Iringa(huku akishangiliwa).

Hapo awali katika ibada aliwataka waumini wote wanaomwombea yeye kuwaombea pia watumishi wote wa Mungu,wainjilisti,wachungaji,manabii,maaskofu na mapadri nchini.

Ikumbukwe wiki moja iliyopita Kanisa katoliki huko Iringa ilipiga marufuku waumini wake kuhudhuria makongamano ya Mtume Mwamposa na waliobainika kuhudhuria walisimamishwa kushiriki baadhi ya huduma za kanisa hilo mpaka hapo watakapotubu.
 
Mimi hipo siku nikitulia hapa nitatoa somo zito kuhusu imani.
Ukiwa na imani yote yanawezekana maana hata maandiko sehemu mbali mbali yanazungumzia kuhusu imani, utapata kitu chochote kile kama utaamini kwa dhati kwamba utapokea.

Marko 10:27
Yesu akawakazia macho akasema kwa wanadamu haiwezekani bali kwa Mungu yote yawezekana.

Yeremia 29:11-24

Pia Marko 11:24
"Kwa sababu hiyo nawaambia yoyote myaombayo mkisali amininini ya kwamba mnapokea nayo yatakua yenu"

Mimi sisali kwa mwamposa lakini anachofanya mwamposa ni Ku trigger hiyo imani na kuikuza na kuona unaweza kupona ukitumia maji na mafuta, believe me Kama uamini uwezi kupona wala kupata kitu.

Siri iliyopo hapa ni kumjua Mungu kujua mapenzi yake na utukufu wake, na kumfata kwa ujasiri maana yeye ni mwaminifu katika kutimiza ahadi zake so si lazima kwenda kwa mwamposa issue hapa ni imani tu.

Isaya anasema tumpelekee BWANA hoja zetu za nguvu naye atasikia maana sikio lake si zito kusikia yale tumuombayo.

So issue ni imani either uende kwake au usiende but Mimi ningependa wakristo wajikite zaidi kumtafuta Mungu.
 
Back
Top Bottom