Mtume kupigwa faini kwa kutabiri tetemeko la ardhi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mwanaume mmoja wa nchini Taiwan ambaye alijitangaza kuwa yeye ni mtume amesababisha mtafaruku nchini humo baada ya kutabiri litatokea tetemeko kubwa la ardhi nchini humo mwezi mei na kusababisha watu waanze kuzikimbia nyumba zao.
Serikali ya Taiwan imetishia kumpiga faini mwanaume mmoja wa nchini humo anayejiita yeye ni mtume kwa kusababisha mtafaruku nchini humo.

Mamlaka za Taiwan zimesema kuwa Mtume huyo anayejulikana pia kwa jina la “Teacher Wang” aliandika kwenye blogu yake utabiri wa kutokea tetemeko kubwa la ardhi litakaloambatana na Tsunami.

Mtume huyo feki pia aliwataka watu wazikimbie nyumba zao kwani hazitaweza kuhimili tetemeko hilo la ardhi na kuwashauri waishi kwenye nyumba zilizotengenezwa kwa makontena ya mizigo.

Wataiwan wengi wamekuwa wakizikimbia nyumba zao na kuuhama mji na kwenda kuishi kwenye nyumba zilizotengenezwa kwa makontena kwenye miji ya ukanda wa kati wa Taiwan.

Jumla ya makontena 170 ya mizigo yameishageuzwa nyumba huku watu wengi zaidi wakitarajiwa kufuata utabiri huo wa Mtume Wang.

Serikali ya Taiwan imemtaka Wang aondoe utabiri wake kwenye blogu yake au la atapigwa faini ya dola milioni moja za Taiwan ambazo ni sawa na takribani Tsh. Milioni 50.
 
Back
Top Bottom