Mtulia azidi kumwaga ahadi

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE (CCM) KINONDONI NDG. MAULID MTULIA KATA YA MZIMUNI TAR. 11FEB*

"Mzimuni mnanijua toka utoto, shida zenu nazijua vyema. Nichagueni niwe Mbunge nikazitutatue kupitia chama imara kinachoongoza dola" - Mtulia

"Najua kuna kero ya mabonde. Mabonde ya Mto Msimbazi, Mto Kibangu yanaleta mafuriko nyakati za mvua. Mnakumbuka nilivyosimama kidete Mahakamani bomoabomoa ikazuiwa kwa wakazi wa Mabondeni ." - Mtulia

"Najua kuna matatizo ya barabara zetu mitaani, bima za afya kwa Wazee nimejiunga na chama chenye ilani inayoongoza dola nina uhakika yote haya yatatatulika" - Mtulia

"Kuna matatizo ya elimu hapa haswa ya uzio, Waziri wa Elimu yupo hapa amelisikia. Nichagueni nikasimamie vyema matatizo na kero zote za elimu tuzimalize" - Mtulia

"Nilifanya juhudi kuzungumza na Shirika la Nyumba na Mashirika mengineyo tuwe na ujenzi wa Maghorofa na kuwe na mipango ya maboresho ya makazi. Nilipata vikwazo kutokana na chama nilichokuwepo, nikaamua kujiondoa CUF na kujiunga na CCM kwa maslahi yenu wana Kinondoni ili mipango ikamilike. Huo ndio usaliti" - Mtulia

"Nilipata vikwazo vingi vya kuwaletea maendeleo kutokana na chama nilichokuwepo awali. Nimejiunga na CCM naona njia itakuwa nyeupe ya kuwaletea maendeleo. Huo ndio usaliti? - Mtulia

"Nimetoka kwenye chama chenye migogoro, kisicho na dola na kujiunga kwenye chama imara chenye dola na ilani ya kimaendeleo inayoendesha nchi. Huo ndio usaliti? - Mtulia

"Nikishinda Ubunge nitashirikiana na Serikali iliyopo madarakani kukomesha matatizo yanayowapata waendesha bodaboda kwa kuwapa namba ya utambulisho watambulike. Pia tutawakopesha Vijana bodaboda toka asilimia 5 za Manispaa" - Mtulia

"Akina Mama nao pia mjue kuna pesa zenu asilimia 5 zenu toka Manispaa. Nichagueni niwe Mbunge wenu nikasimamie mpatiwe mikopo hiyo" - Mtulia

"Nazidi kuwasisitiza Februari 17 mjitokeze kwa wingi vituoni mapema muende kunipigia kura za ndiyo niwe Mbunge wenu wa Kinondoni. Kuchagua CCM ni kuchagua maendeleo" - Mtulia
IMG-20180211-WA0041.jpg
 
Back
Top Bottom