Mtukufu Ramadhani!

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Mtukufu Ramadhani!



Date: 7 September, 2007
  1. Bismilahi Raufu, Mhariri gazetini,
    Mimi sio maarufu, hapo kwenu kilingeni,
    Nataka kuwaarifu, Islamu na Misheni,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  2. Mwezi huu mtukufu, jina lake Ramadhani,
    Utende matakatifu, ninatoa ilani,
    Utapata utukufu, mwisho wake duniani,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  3. Najaribu kuhubiri, bado kupata yakini,
    Imekuwa desturi, ifikapo Ramadhani,
    Kutuuzia futari, bei juu magengeni,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  4. Mwezi huu mashuhuri, asiyejua ni nani?
    Biashara hushamiri, dukani hata sokoni,
    Yafaa ujihadhari, unapo uza sokoni,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  5. Kiumbe fanya nadhari, bei ziwe wastani,
    Usitake utajiri, kudhulumu maskini,
    Watu wote si tajiri, wanunuao sokoni,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  6. Imekuwa staili, ifikapo Ramadhani,
    Bei zenu kubadili, sokoni na madukani,
    Bidhaa kuuza ghali, hata haya hamuoni,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  7. Natoa hii kauli, AN-NUUR gazetini,
    Wasikie Waswahili, walio bara na pwani,
    Lanikera jambo hili, tumugope Manani,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  8. Huo ndio ukafiri, mimi nawaambieni,
    Kudhulumu mafakiri, waliojaa madeni,
    Hii kweli sio siri, mimi sijui kwa nini?
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  9. Mohammadi na kakiri, huko kwao Arabuni,
    Alizifanya safari, akiwa biasharani,
    Aliuza kwa kadiri, hakufanya uhaini,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
  10. Katitamati shairi, Mhariri samahani,
    Mungu atakusitiri, uiendeleze fani,
    Na akujaze na heri, upate nishani,
    Mwezi huu Mtukufu, kiumbe wacha dhuluma.
Ustadh Abdallah Aziz (Darigube)
Masjid Qiblatain English Medium Primary School,
DAR ES SALAAM
 
Last edited:
Karibu Mwezi Mtukufu Ramadhani, wafanyabiashara zingatieni haya ili mpate fadhila na kubariki biashara zenu katika mwezi huu mtukufu.
 
VIDEO - Obama Awatakia Waislamu Mfungo Mwema wa Ramadhan
2885254.jpg

Rais Barack Obama wa Marekani Saturday, August 22, 2009 9:18 AM
Rais Barack Obama wa Marekani ametoa video maalumu akiwatakia waislamu wote duniani mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhani ambao umeanza leo sehemu nyingi duniani. VIDEO ya ujumbe huo wa Obama mwisho wa habari hii. "Kwa niaba ya Wamarekani, waislamu wa Marekani na waislamu duniani kote nawatakia Ramadhan Karim" alianza kwa kusema rais Obama.

Katika video yake maalumu ya kuwatakia waislamu mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhani ambao umeanza leo sehemu mbali mbali duniani ambayo inapatikana kwenye website ya ikulu ya Marekani, Rais Obama aliuelezea mwezi wa ramadhani kwa undani.

"Mwezi wa ramadhani ndio mwezi ambao waislamu wanaamini quran iliteremshwa kwa mtume Muhammad (s.aw) kwa kuanzia na neno Iqra" alisema Obama.

Rais Obama katika ujumbe wake alisema kwamba mwezi wa ramadhani unawakumbusha waislamu kufanya mambo mazuri ambayo pia wakristo katika dini yao wanatakiwa kuyafanya.

Rais Obama alikumbushia pia jitihada zake za kukuza uhusiano kati ya waislamu na Marekani.

Angalia video chini kwa ujumbe kamili wa rais Obama.


VIDEO - Ujumbe wa Ramadhan toka kwa Obama

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2885254&&Cat=2

 
nitapita tena kwa upolee zaidi nami niweke changu.

Akhasantum sana Ustadh Abdallah Aziz (Darigube)
wa Masjid Qiblatain English Medium Primary School,
ya .DAR
 
As-salaam Aleikum,


Ya ayyuha allatheena amanoo kutiba AAalaykumu alssiyamu kama kutiba AAala allatheena min qablikum laAAallakum tattaqoona

O ye who believe! Fasting is prescribed to you as it was prescribed to those before you, that ye may (learn) self-restraint,- ( Al Baqarah 2:183)





The above ayat is the core foundation for the Holy Month of Ramadhan. It is what we know to be the "raison-d-etre" for the fasting that is prescribed for us during the Holy Month of Ramadhan. A month where we are to restrain ourselves while developing good habits for our life.





Upon closer analysis however, an interesting detail comes up. This pertains to the DURATION of the fasting activity rather than the fasting itself. Fasting has been prescribed for a period of a month so depending on conditions etc, anything from 28 to 30 days for the Islamic Lunar Calender.




It is now emerging that 30 days is a significant duration for the purposes of of sinking in a new habit. Dictionary.com defines habit as " an acquired behavior pattern regularly followed until it has become almost involuntary".. So important is this phenomenon of 30 days as a personal growth tools n terms of habits, that it is termed the "30 day Principle".




The "30 day Principle" simply entails practicing a new habit continously for 30 days. The outcome is that the new habit then becomes engrained in our psyche and we develop unconcious competence for that new skill or habit. Simply put, the new skill becomes involuntary to us and hence becomes... a habit.




This is borne out by numerous applications of the concept. A common example is the 30-day trial period that software sellers use for their products for example. A more credulous and scientific evidence of the concept is an experiment carried out by NASA. They gave astronauts convex lenses ( the outcome was that the astronauts then saw upside down images as opposed to the normal upright ones ) to see with -they expected a number of reactions: nausea,irritability. What they got was something else. Eventually, the astronauts' brains flipped the upside down images to their normal upright position. The unconcious mind somehow managed to re-train the brain to view the images in their proper perspective.




Similar procedures were undertaken at varying number of days and it turned out that any interuption ( the astronauts removing the convex lenses ) before 25 days meant that the astronauts had to start the procedure again continously for 30 days in order the for unconcious mind to "adjust" the upside down stimulus of the images received by the eye.




From this we can see that any new habit or skill has to be sustained for 30 days (certainly not for a period less than 25 days ) for the "new" representation to become accepted in the unconcious mind and hence become an almost involuntary habit.

So we see that in His wisdom Allah (swt) towards making us better human beings, He not only prescribed fasting but prescribed fasting in a time period that has been scientifically proven to be the appropriate time period for engraining new habits ( if practiced without interruptions).




It even becomes more startling when you relate this to the human psyche. We're all aware that we dread making permanent changes...we're more amenable to applying things when we feel that it is for a temporary period. This is because any perceived discomfort of the "new" skill/habit/change is viewed as being temporary and so long as you have a duration ie 30 days, you can always envision your "freedom" at the end of it. So,in reality, the temporary perception is actually the foundation for forming lifelong habits.





The import of all of this for you : for the coming Ramadhan, once you have established what your goals are in the major areas of Ibadah/knowledge - you need to keep them up and practice them consistently and without interruptions for the whole month . At the end of the month , they become second nature to you.

At that point, you will be applying the skills/knowledge involuntary ,with the promise of earthly benefits but more importantly for the benefits of the hereafter.
 
Ya ayyuha allatheena amanoo kutiba AAalaykumu alssiyamu kama kutiba AAala allatheena min qablikum laAAallakum tattaqoona

O ye who believe! Fasting is prescribed to you as it was prescribed to those before you, that ye may (learn) self-restraint,- ( Al Baqarah 2:183)
.

Barubaru tusomee hapo nilipoweka red.

Ok all in all, ujumbe umefika. tunaomba kila kheir mfungo huu mtukufu.
 
Back
Top Bottom