Mtukufu Rais umepata kusikia maneno haya ya Jakaya Kikwete?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,793
71,206
RAIS mstaafu wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete , alipata KUSIMULIA:

"Siku moja usiku, nilipokuwa mtoto, nakumbuka kumwona MAMA yangu akituletea chakuka mezani nikiwa na BABA.
MAMA aliniwekea sahani ya CHAPATI, huku akimwekea BABA sahani yenye chapati ILIYOUNGUA.

Nilijaribu kumuangalia BABA ili kuona ATAFANYAJE. Baba alianza kula CHAPATI ile iliyoungua huku akiniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni.

Sikumbuki nilichomjibu, ninachokumbuka ni kumsikia MAMA akimtaka RADHI baba kwa KUUNGUZA chapati. Na kamwe sitasahau majibu ya BABA pale alipomjibu MAMA kwa kumwambia, 'Oh, usijali MKE WANGU. Huwa NAPENDA pia chapati za KUUNGUA.'

Baadaye , nilipokwenda kwa baba na kumtakia usiku mwema, ndipo nilipomuuliza kama ni kweli hupendelea chapati za kuungua.

Alianza kuniambia, 'Leo, MAMA yako alitingwa mno na MAJUKUMU ya kazini hata akawa amechoka sana, ndipo akaunguza chapati. Lakini, kwa bahati, chapati ILIYOUNGUA haiwezi KUMUUMIZA mtu kiasi cha KUMCHOMA MOYONI, walakini MANENO makali yanaweza KUMUUMIZA. Hivyo, sikuwa na sababu ya KUMSHUTUMU kwa MANENO makali. Hata kama sipendi chapati za kuungua, ila kumjibu vile kumemfanya awe huru. Unajua MAISHA nayo hayako KAMILI kama TUSIVYO kamili SISI wanaadamu. Kwahivyo, ili kudumisha FURAHA na kuboresha MAHUSIANO na MAELEWANO baina YETU, ni lazima TUJIFUNZE kuyakubali na kuyakabili MAPUNGUFU yetu - Chapati za kuungua hazidumu milele, zikishasagika tumboni utakwenda kuzitoa msalani. Lakini, MANENO makali huacha majeraha ya kudumu MOYONI....
UPANDE WANGU:
Ukizungumza na RAIA wako umezoea kutamka maneno makali na hata kuchanganya na matusi jee haudhani kuwa hilo laweza kuwa sababu ya hii kasi ya kuwa unpopular?
Unadhani maneno kama yale uliyotoa Bukoba kuna mtu atasahau?
 
Siku moja nitakuwa raisi,

Nitawaonesha ilivyo rahisi kuleta maendeleo bila kuminya haki ya mtu yeyote.

Nitawaonesha nguvu waliyonayo wananchi katika kuleta maendeleo ya nchi yao wenyewe.

Nitaonesha jinsi ambavyo unaweza kuongoza nchi kwa uwazi.

Siku moja nitakuwa raisi na wabunge watawatumikia wananchi.

Siku moja nitakuwa raisi na kila Mtanzania atakuwa na sauti.

Siku moja.
 
Ni upofu waliopigwa na Mungu hadi maandiko yatimie,wako wanaobisha kuhusu TB Joshua kukimbia kuwepo kwenye uapisho wake ingawa alienda kumpokea airport,na hata kutembea pekupeku ilikuwa ni maombolezo kwa Tanzania,wasaidizi na washauri wakuu ni kina bashite,hapi na mnyeti unatarajia ni nchi ya aina gani hiyo
 
Kwa kila binadamu aliyestarabika, hutenda na kuuishi ustarabu huo daima awapo hapa duniani. mfano halisi ni mzee mwinyi, sijamsikia akifoka wala kutukana hadharani. kwa mtazamo wangu, JK na Mzee mwinyi wana haiba zinazofanana.

On Contrary, Magu hajastaarabika. hana ustaarabu wowote na hatakuja kustarabika. Ili binadamu aweze kuwa civilized, kuna stages of evolution anazopitia kufikia hatua hiyo. Kwa bahati mbaya, JPM hakubahatika kuishi kama binadamu wengine hapa chini ya jua..

Nimeishi Mwanza na wilaya zake zote, 1991 nilikuwa nafanya research wilaya ya Bukwimba-Ngudu. almost 2/3 ya maisha yangu nilikuwa kanda ya ziwa. Wasukuma ni watu wema, wapole, hawana visasi sana, wanapenda kusaidia watu wenye shida. Je huyu JPM mbona hauishi usukuma? @Pascal Mayalla
 
Moyo wake hauna amani, umejaa visasi, wivu na chuki iliyopitiliza. Sasa usitegemee akiongea atoe maneno ya faraja. Ni pakanga.

Huyu mtu hata awe kwenye umati wa heshima mfno katika kanisa, ataongea hewa kabisa, hana logic au mtiririko mzuri wa kupangilia maneno, wala sidhani kama anafahamu neno lipi ni sahihi au si sahihi. Pia anapenda ujivuni, hivyo hata atakapo ongea upuuzi na mkacheka na kushangilia ataurudia hivyohivyo rejea kauli zake juuu ya nabii tito pale kanisa la anglican wakati wa kutiwa wakfu askofu.
Hajakulia katika mazingira ya mazuri ya kuonywa na amekua akijiona yeye tu ndie anayejua sana, sina shaka hata ndugu zake na familia yake huwakaripia upupu kama atufanyiavyo sisi. So sad
 
Kati ya watu wasioeleweka wanapenda nini ni watanzania.

Tukatae tukubali anachofanya JPM ndio asili ya watanzania
Hatueleweki tunataka nini na hatutaki nini

Pia mtanzania kwa asili hawazi mambo kwa akili yake ili kutoa uhuru wa maamuzi yake, waliowengi hupenda kutembea kwenye nyayo za mawazo ya watu

Tuliobahatika kuishi katika awamu zote hizi nne za marais wa Tanzania utaelewa namanisha nini??

Hayupo rais aliyeiongoza Tanzania pasipo makundi na wengi wao waliwachukulia wapinzani wao kama maadui wa Taifa.

Lakini hakuna mtanzania aliyewahi kuja na mawazo huru, watanzania wengi huja na mawazo tegemezi yasiyojitoshereza ndio mana hata harakati zetu hazifiki mwisho kwani wazo husika hatujui chanzo chake ni nini??
 
Kuna kitu kinaitwa nature ya mtu, yaani mtu kuwa jinsi ulivyo, Magufuli na Kikwete ni watu wawili tofauti kabisa, Kikwete wa a gentleman, Magu is not!. Huwezi kumgeuza Magu awe kama JK!. Magu anavyoongea ndivyo alivyo na hili niliishawahi wahi kulizungumza humu,
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni asili tuu ya wasukuma, sio udikteta!

Hivyo kuongea kwa ukali sio hoja, hoja ni the motive behind kuongea huko!.

Hata hivyo kuhusu hili la kuongea tuu chochote, popote, pia niliishawahi kulitolea ushauri humu

Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!.

Paskali

INGEKUA NI KUONGEA TU WALA HAINA SHIDA,LAKI HATA VITENDO VYAKE NI VYA AJABU KABISA KUFANYWA NA KIONGOZI WA NGAZI YA JUU (RAIS) POPOTE DUNIANI,kumbuka anayoyatenda kwa Watumishi hadharani,kumbuka ya bomoabmoa,kwengine sawa kwangine siyo sawa.Mayalla fikiri upya kuhusu hoja zako.
 
Magufuli hakuwa na sifa za uraisi alipitishwa kunusuru chama. Alikuwa hana ushawishi(convincing power), hakujiandaa(alishakiri "nilisukumizwa"). Magufuli ni mbinafsi sana, anapenda kuonewa huruma muda wote na kupenda sifa.

Wanaccm kumpitisha magufuli mtakuja kujuta sana. Miaka2+ tu lakini inchi iko shaghalabagala. Na ukiangalia viashiria vya uchumi HAKUNA matumaini hali itazidi kuwa ngumu.
 
INGEKUA NI KUONGEA TU WALA HAINA SHIDA,LAKI HATA VITENDO VYAKE NI VYA AJABU KABISA KUFANYWA NA KIONGOZI WA NGAZI YA JUU (RAIS) POPOTE DUNIANI,kumbuka anayoyatenda kwa Watumishi hadharani,kumbuka ya bomoabmoa,kwengine sawa kwangine siyo sawa.Mayalla fikiri upya kuhusu hoja zako.
Tumeshalikoroga
 
Moyo wake hauna amani, umejaa visasi, wivu na chuki iliyopitiliza. Sasa usitegemee akiongea atoe maneno ya faraja. Ni pakanga.

Huyu mtu hata awe kwenye umati wa heshima mfno katika kanisa, ataongea hewa kabisa, hana logic au mtiririko mzuri wa kupangilia maneno, wala sidhani kama anafahamu neno lipi ni sahihi au si sahihi. Pia anapenda ujivuni, hivyo hata atakapo ongea upuuzi na mkacheka na kushangilia ataurudia hivyohivyo rejea kauli zake juuu ya nabii tito pale kanisa la anglican wakati wa kutiwa wakfu askofu.
Hajakulia katika mazingira ya mazuri ya kuonywa na amekua akijiona yeye tu ndie anayejua sana, sina shaka hata ndugu zake na familia yake huwakaripia upupu kama atufanyiavyo sisi. So sad
Mtasema weeeee mkichoka nendeni mkakojoe mkung'ute miguu mlale.. tunajua propaganda zenu..Mh Rais anayofanya ni kwa manufaa ya nchi na sio ubinafsi uliowajaa..iam telling you, in this battle the majority shall win. No matter what..!!!
 
Kwa kila binadamu aliyestarabika, hutenda na kuuishi ustarabu huo daima awapo hapa duniani. mfano halisi ni mzee mwinyi, sijamsikia akifoka wala kutukana hadharani. kwa mtazamo wangu, JK na Mzee mwinyi wana haiba zinazofanana.

On Contrary, Magu hajastaarabika. hana ustaarabu wowote na hatakuja kustarabika. Ili binadamu aweze kuwa civilized, kuna stages of evolution anazopitia kufikia hatua hiyo. Kwa bahati mbaya, JPM hakubahatika kuishi kama binadamu wengine hapa chini ya jua..

Nimeishi Mwanza na wilaya zake zote, 1991 nilikuwa nafanya research wilaya ya Bukwimba-Ngudu. almost 2/3 ya maisha yangu nilikuwa kanda ya ziwa. Wasukuma ni watu wema, wapole, hawana visasi sana, wanapenda kusaidia watu wenye shida. Je huyu JPM mbona hauishi usukuma? @Pascal Mayalla

Maneno yako ni kweli. Nilikuwa kwa Rafiki yangu fulani msukuma nilikutana naye kwenye hafla fulani akanialika kwake Mimi na familia yangu, Kwa kweli siku tuliyokwenda kwake kwa alivyotukaribisha tuliiona siku imekimbia haraka sana. Huwezi kuamini tulikuwa kama ndugu tuliokimbiana kitambo.
 
Back
Top Bottom