Mtukufu mimi ni kati ya wale shetani wako nisikilize japo kidogo

Mbona mishahara inatoka mapema na wateja wana pesa. Faida ipo.
kuna mtu kaongelea kuchelewa kwa mishahara hapa? hii mishahara ambayo haijapanda tangu aikute? mishahara ambayo almost yote ina one-third ambayo hazina kiutaratibu hawakubali kuikata zaidi lakini hawa jamaa wametubambikia deni la Bodi Ya Mikopo ya Elimu ya Juu wakakata hivyohivyo?
 
2. Unaamini Serikali ingeendelea kuwaajiri wahitimu wote wa ualimu miaka yote?

3. Huo uzoefu wa kijeshi wa wanafunzi walionao kwanini usidhani kuwa wanaweza kuutumia kwenye kilimo na sio ujambazi mtsani?
4. Wazazi kuwa na chuki na Rais huo utafiti umeufanya lini na namna gani?

Nyie ndio watu mnaoiweka majaribuni JF yetu. Yani kinachokuja kichwani mnaomwaga tu hapa jukwaani.
Watu tunapata shida wewe hako ka mshahara unakokapata ndo kanakupa jeuli, kumbuka mshahara wako unatokana na kodi za wananchi kama huwezi kuwa mkweli utakuwa MTU wa ajabu.
 
Watu tunapata shida wewe hako ka mshahara unakokapata ndo kanakupa jeuli, kumbuka mshahara wako unatokana na kodi za wananchi kama huwezi kuwa mkweli utakuwa MTU wa ajabu.
Wewe kwakuwa unapata mshahara unadhani sote tunaishi kwa kutegemea mshahara????

Jishughulishe kijana kwa njia halali utaona matunda yake...kupiga kelele hakutakusaidia kitu zaidi ya kukuongezea stress za maisha
 
Hata ukifanya kazi pesa mtaani hakuna kabisa maana Mimi ni mfanyabiashara
hapa hata mimi imenipa shida sana mpaka nikajiuliza inamaana taifa lilikuwa linaendeshwa kwa Upigaji?

Maana hata wateja hakuna unapouza bidhaa yaani biashara zimedorora sana.

Utawakuta mama ntilie wanarudi na chakula chao nyumbani baada ya kukosa Wateja.

Nikajiuliza kimoyo moyo ina maana watanzania sasa wameanza mfungo kabla ya muhula wake?

Inikajibiwa na ufahamu wangu kwamba tutatengeneza kama taifa wagonjwa wengi sana wa vidonda vya tumbo mbeleni.

Ni ushauri wangu kwa serikali ijitafakari uenda ikawa kuna maali wameteleza kidogo juu ya sera fulani Ambayo yapasa waitazame ili kuondoa sinto fahamu hii.
 
Pesa mtaani hazipo, mishahala inatoka mapema sawa, wafanyakazi wengi walikopa kwenye mabenki na taasisi zingine za kifedha, mwisho wa mwezi slary slip zina soma ziro, walikuwa wakitegemea za kupiga sasa hazipo. Mtaani lazima Pesa ikosekane
 
2. Unaamini Serikali ingeendelea kuwaajiri wahitimu wote wa ualimu miaka yote?

3. Huo uzoefu wa kijeshi wa wanafunzi walionao kwanini usidhani kuwa wanaweza kuutumia kwenye kilimo na sio ujambazi mtsani?
4. Wazazi kuwa na chuki na Rais huo utafiti umeufanya lini na namna gani?

Nyie ndio watu mnaoiweka majaribuni JF yetu. Yani kinachokuja kichwani mnaomwaga tu hapa jukwaani.
Kwanini wasiwaajiri walimu kama hamna umuhimu waondoe course za ualimu vyuoni
Utalima wapi wakati hata ukilima mazao yanaharibikia ghalani...kodi tele...na pembejeo zote ukumbuke zipo kijijini mamsera hazijafika..kwanini nisiwe jambazi wakati kila aina ya silaha najua
 
Nao zamu yao ya msoto inakuja, watasoma sana sayansi na wataishia kuwa mafundi mchundo tuu, labda madaktari, kandarasi kubwa zote za umeme, barabara, gesi, mafuta bado zinafanywa na wageni( Wachina?!)
 
1. Mtukufu najua unajiamini na kufurahi sana kwa kubana uchumi ila ujui unatengeneza chuki, umaskini, majambazi, wajinga na kadharika, tambua kuwa hali ikiwa ngumu sana hata nyie mnaopata keki ya serikali hamtaweza kuitumia maana majambazi wataishia kuwaua.

2. Umewanyima waliosoma Sanaa ajira, umetengeneza kundi kubwa sana la watu wanaoshinda mtandaoni na kuuchambua uongozi wako na we hupendi kukosolewa mtukufu.
3. Wanafunzi wengi wamekosa mkopo tunao mtaani na wamepitia jeshi, hapo ndo patamu maana hawa ndo watageuka majambazi wenye mafunzo.

4. Wazazi wanachuki na wewe sana maana watoto wao umewanyima mkopo na wengine hujawapa ajira, patamu hapooo!!!
5. Madreva wanapigwa faini kila baada ya kilometa moja ilimradi vijana wako wakusanye kodi ya kukuridhisha wewe.
6. Walimu wanafundisha ili mladi siku ziende ila maandalio na silabasi vunaisha mapema sana. Patamu hapooo!!!

Mengine mtaongeza wanajamvi.

Onyo langu kwako acha jeuri umma unanguvu sana ukichoka na ukaamua kuzitafuta haki zao utaumia.

Najua hauna nguvu za kupigana ila unajivunia askali na jeshi.

Nikukumbushe kuwa hao askali na familia zao wanaishi mtaani umeshindwa kuwasitili. Fikiria watakulinda wewe au wake na watoto wao?

Pia hao makamanda wako familia zao wako huku wanaangaika kama sisi fikilia watakulinda wewe au watalinda mama zao na baba zao. Fikiri Mara mbilimbili ingawa najua umezaliwa kwenye mikoa ya wapenda sifa.

Ukipitia hapa ukanielewa nipe hata like kwa kukumbusha umejisahau sana mtukufu wangu.
Pia mbona anasema hii nchi ni yake wakati walioipatia uhuru hawakusema yao anapata wapi uo upuuzi.....
Pia ajue hatumuogopi bali tunamheshimu
 
Back
Top Bottom