Kiberiti Kidogo
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 575
- 917
Mh. Magufuli na wana JF habari za kazi? Rejea kichwa cha habari hapo juu....chahusu kuwahimiza wanafunzi vyuoni kudesa.
Wandugu suala la kudesa ndo kila kitu ulimwenguni. Mimi nimesoma chuo kikuu mara zote nilitumia akili yangu kusoma na kufanya mitihani. Ufaulu wangu haukuwa mkubwa sana. Ila kwawale wenzangu waliokuwa wanadesa mara zote walinikimbiza darasani. Kuna wakati nilitamani kudesa ila kwa vile nilijiona kipanga niliogopa kuitwa KILAZA. Ila leo niko mtaani naishi maisha ya kawaida sana bado wale waliodesa wananikimbiza hatari kimaisha.
Raisi alivosema anataka Tanzania ya Viwanda ukweli nilitabasamu sana nikaona ni fursa kwangu pia ya kuajiriwa endapo viwanda vitakuja. Ukweli Mwijage anapokuwa anaongea kuwa hadi sasa kuna viwanda 2000 toka JPM aingie huwa simwelewi maana huwenda anaongea mambo ya karne ya 14.
Nilijaribu fatilia na mimi kwa undani suala la kumsaidia Raisi ili kufikia malengo ya uchumi wa viwanda. nimepitia sera kadha wa kadha duniani. Licha ya kuwa mhandisi ila historia ya mapinduzi ya viwanda naijua hatari.
Nilichogundua ni kwamba bado wale WADESAJI ndo wameshika pia uchumi wa Viwanda ulimwenguni. Nikiangalia nchi za Ulaya, Asia na America wako mbali sana kwenye teknolojia ya viwanda. Ila nilichogundua ni kwamba wamefanikiwa kwasababu wanawatu ambao wanajua KUDESA. Teknolojia nyingi ambazo baadae huzaa viwanda duniani zimeanzia Vyuoni pamoja na kwenye Majeshi. Wengi wao walitumia silaha moja tuu na muhimu ya KUDESA. Mapinduzi ya viwanda yalianzia bara uropa na baadae kusambaa kwa njia ya KUDESA(COPY AND PASTE). Leo hii tunamuona mchina au mkorea au mmarekani au mhindi au mjerumani wako juu ila silaha yao ni kudesa. Inanipa raha sana kuona Mmarekani anatoa Iphone 7 hafu kesho mchina anatoa COPY. Hii inaonesha wako vema kwenye suala la kudesa. Toka tumeanza kufurahia smartphone na komputa tumeshindwa KUDESA??? Nilitegemea bodaboda, komputa, simu, gari, baiskeli, na aina yoyote ya mashine inayotoka na sisi tunakuwa na yetu. Nikagundua tunakatazwa KUDESA. Ukidesa unaonekana KILAZA kumbe wenzetu wanapaa kisa wanajua KUDESA. Kama nilivosema teknolojia nyingi zimeanzia Vyuoni ningependa kumshauri rais ahimize wanafunzi kudesa. Tena ningefurahi sana kama atakuja ata na simu ya Tochi samsung awape vijana DIT, COET, AIT wakomae wachape kopi. Watu husoma Electronics eng, electrical tele na computer eng kwaajili gani kama hatuoni matunda? Mtukufu kuna machine nyingi sana zipo mitaani ambazo naimani kabisa UKIWAHIMIZA WANAFUNZI VYUONI KUDESA tunaweza kuzalisha kopi zake na sisi kuzibadili kidogo walau Kabla hatujafa tuwe na stika zilizoandikwa MADE IN TANZANIA. Na ndipo tutakuja kujivunia uchumi wa viwanda. Mkuu wawezeshe vijana KUDESA. Adolf Hitler historia inasema alidiliki hadi kuua mtu alieshindwa KUDESA kutoka kwa wayahudi. Mmarekani, mjapani, ,mchina,mrusi na wengine wameDESA kwanza.
Ukweli nimekazania sana teknolojia ila hata kwa fani nyingine zote wahimize KUDESA. Huwenda yangekuwepo hata mashindano ya mavyuo ya KUDESA tuwe na mfumo wetu na sisi. Ni hilo TUU mkuu.....