Mtuhumiwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
pix.gif

Na Mwandishi Wetu
The Supermodel, aliye pia Miss Tanzania 10 Bora 2008-09 anayedaiwa kufanyiwa unyambilisi wa kubakwa kisha kupigwa picha chafu, anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine, hii ikihusu kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ubakaji huu...
Gazeti ‘High Quality’ Risasi Jumamosi halina cha kupoteza kwa kumtaja kijana, Patrick Trey kuwa ndiye mtuhumiwa wa ubakaji huo na nukta hii tayari amekwishanaswa na mkono wa sheria.

Patrick (pichani kulia), anashikiliwa na Kituo cha Polisi Kawe, Dar na shauri lake limendikwa ndani kitabu cha ripoti za polisi kwa nambari KW/RB/2325/2010.

Data zilizopo ‘mjengoni’ zinaanishwa kwamba awali, Patrick aliswekwa lupango kwenye Kituo cha Selander Bridge, Seaview, Dar na kufunguliwa jalada lenye namba SBR/RB/470/2010 lakini baadaye alihamishiwa Kawe kutokana na sababu za ‘kiprotokali’.

Vyanzo vyetu vinaweka wazi kuwa Patrick alikamatwa siku moja baada ya tukio hilo analodaiwa kulitenda baada ya mtego wa Miss Tanzania huyo kuzaa matunda.

Ilielezwa kuwa baada ya mrembo huyo kuamka asubuhi na kujikuta hana nguo, amechafuka, mchovu na maumivu mwilini nyumbani kwa Patrick, inaelezwa kwamba kijana huyo bila woga alijibu kwa kujigamba kumtendea unyambilisi huo.

“Miss alipohoji ilikuaje mpaka akawa nyumbani kwa Patrick tena akiwa hana nguo, Patrick alijibu kuwa alimbaka, tena si yeye peke yake, walikuwa watatu na walimtenda kwa kushirikiana, yaani mtungo,” alidai mtoa habari wetu na kuongeza:
“Patrick alimwambia Miss kuwa ni siku nyingi alikuwa akimtaka kimapenzi lakini akawa anamzungusha ndiyo maana alimfanyia unyama huo.”

Mtoa habari huyo aliendelea: “Kuona hivyo, Miss ilibidi ajifanye anamkubalia na anampenda, akamlaghai wakaenda nyumbani kwao, akashirikiana na ndugu zake wakampeleka Selander Bridge lakini kwa sababu tukio lilifanyika Mbezi Beach nyumbani kwa Patrick ikabidi shauri lihamishwe Kituo cha Kawe.”
Miss huyo (jina linahifadhiwa), anadaiwa kufanyiwa unyama huo Machi 14, 2010, baada ya kuleweshwa.

Inaelezwa kuwa Mss huyo na Patrick walikutana SeaCliff Hotel na baadaye walihamia Club Bilicanas ambako inadaiwa mrembo huyo aliwekewa ‘dawa’ kwenye kilevi, hivyo kupoteza fahamu na alipoamka, alijikuta amekwishatendwa.
Habari zinazidi kudai kuwa Patrick wakati akimtenda Miss huyo, alikuwa anamchukua picha za mnato kupitia simu ya mkononi, kamera ya kompyuta (laptop) na video.
 
mhhhh watu wengine sijui wagonjwa......
unambaka mwanamke ili iweje???
wanawake wangapi wazuri wanarafuta wanaume na hawapati?????
una nyumba mbezi beach bado unahitaji kubaka mwanamke????????
 
mhhhh watu wengine sijui wagonjwa......
unambaka mwanamke ili iweje???
wanawake wangapi wazuri wanarafuta wanaume na hawapati?????
una nyumba mbezi beach bado unahitaji kubaka mwanamke????????[/QUOTE]​


The Boss, hari za jumapili........ kuwa na nyumba mbezi beach ni leseni ya kupata mwanamke yeyote unaemtaka?


Annina
 
mhhhh watu wengine sijui wagonjwa......
unambaka mwanamke ili iweje???
wanawake wangapi wazuri wanarafuta wanaume na hawapati?????
una nyumba mbezi beach bado unahitaji kubaka mwanamke????????[/QUOTE]​


The Boss, hari za jumapili........ kuwa na nyumba mbezi beach ni leseni ya kupata mwanamke yeyote unaemtaka?


Annina

sio yeyote kwa maana ya exactly yule unaemtaka.
but yeyote kwa maana ya ukimkosa huyu utampata mwingine........

za jumapili safi upoo?
 
Mbakaji ana ugonjwa wa kisaikolojia. Hata Kariakoo sokoni anaweza kubaka tu. Labda kwa kuwa miss TZ jamaa alikuwa anatafuta bikira? Si nasikia mamiss ni mabikira?
 
Jamani mtuhumiwa atakuwa kwanza siyo mzima pili hatakama mtu ulikuwa unamtaka for a long time sasa ndio mtumie na wengine jamani huyo ni mnyama tena mmmh haoni haya kujibu eti ndio nimekubaka atakuwa mwehu lazima.
 
Back
Top Bottom