Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwalimu Frola Mariki akamatwa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Mkazi wa Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam, Flora Mariki (34) anadaiwa kuuliwa na mtoto wa shemeji yake, binti mwenye umri wa miaka 22 baada ya kutokea ugomvi baina yao.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Janet Magomi amesema tukio hilo lilitokea Jumapili Mei 30, 2021 na mtuhumiwa huyo (ambaye hajatajwa jina lake) anashikiliwa kwa mahojiano.

Katika maelezo yake Kamanda Magomi amesema, “tunamshikilia binti huyu kwa ajili ya uchunguzi zaidi na upelelezi utakapokamilika tutamfikisha mahakamani kwa hatua zaidi.”

Mmoja wa majirani wa Flora ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema mauaji hayo yalitokea saa 3 usiku baada ya mume wa marehemu aliyemtaja kwa jina moja la Asenga kumueleza binti huyo jinsi alivyobadilika tabia na kuwa mkorofi.

“Wakati Asenga akizungumza na binti huyo ambaye ni mtoto wa kaka yake, Flora alisikia na wakati akizungumza na huyo binti, Asenga aliwaacha na kwenda chumbani, lakini baada ya muda kulikuwa kimya na ndipo ilipobainika kulikuwa na tukio la mauaji,” amesema.

Kuhusu mauaji, soma: Mwalimu Shule ya Msingi, Flora Mariki auawa kwa kuchomwa kisu na mtoto wa shemeji
 
Mtuhumiwa hajapelekwa mahakamani mpaka leo hata mahabusu hajapelekwa polisi wameshachukua pesa wameamua kumwachia mtuhumiwa
 
Back
Top Bottom