Mtuhumiwa wa Escrow afutiwa mashtaka ,kesi hiyo ambayo bado ilikuwa katika hatua za upelelezi.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,380
2,000
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameamua kuiondoa mahakamani kesi ya Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa ikimkabili Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Theophillo Bwakea.

Bwakea alikuwa akikabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kupokea Sh161,700,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering & Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.

Jana, Bwakea aliachiwa huru baada ya DPP kuamua kuiondoa mahakamani kesi hiyo ambayo bado ilikuwa katika hatua za upelelezi.
 

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,260
2,000
Kama kuna mipesa mingine kwenye akaunti yoyote naomba mnichoree ramani nikakwapue mipesa. Naimani sitafungwa maana hii nchi tajiri bwana itapata mihela mingine
 

DAFU NA NDIMU

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,456
2,000
Acha kupotosha
Kosheria hakuna mtu anayeweza kushtakiwa mara mbili kwa kosa lilelile....km angetaka kuipeleka kesi basi angeihamisha na siyo kuifuta
Hahahaha, mbona povu mkuu.
Unajua sababu za kufutiwa kesi ikiwa ktk ngazi ya upelelezi?
Tujuze mkuu.
 

Tyetyetye

JF-Expert Member
Dec 3, 2014
899
1,000
Arudi kazini
ILIKUWA SI HAKI ASHITAKIWE YEYE PEKE YAKE. MBONA WALIOPOKEA RUSHWA HIZO WAKO WENGI SANA WENGINE WAKO BUNGENI. NAO NI NGELEJA, TIBAIJUKA MAARUFU KAMA MAMA WA KISAMVU CHA MILIONI KUMI, MAJAJI KADHAA NA WENGINE AMBAO SERIKALI ILIAMUA KUFICHA MAJINA YAO KWA GHARAMA YOYOTE.
 

makilo

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
1,567
2,000
Dpp Kaamua kunawa mikono maana mlolongo wa waliopokea mapesa ni zaidi ya watu 20 lakini maahaman kapelekwa mmoja tu.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
34,473
2,000
ILIKUWA SI HAKI ASHITAKIWE YEYE PEKE YAKE. MBONA WALIOPOKEA RUSHWA HIZO WAKO WENGI SANA WENGINE WAKO BUNGENI. NAO NI NGELEJA, TIBAIJUKA MAARUFU KAMA MAMA WA KISAMVU CHA MILIONI KUMI, MAJAJI KADHAA NA WENGINE AMBAO SERIKALI ILIAMUA KUFICHA MAJINA YAO KWA GHARAMA YOYOTE.
Siku zote mnyonge hana haki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom