Mtuhumiwa mauaji ya mke amtumia sms mama mkwe

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
428
996
Moshi. Ni matukio nadra kutokea katika jamii, baada ya mtuhumiwa anayesakwa kwa udi na uvumba na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mkewe, kumwandikia mama mkwe ujumbe mfupi (SMS), kuelezea ushiriki wake katika tukio hilo.

Mtuhumiwa anadaiwa kutuma ujumbe huo wakati polisi wakiwa tayari wamechukua sampuli kwa ajili ya kupima vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kama mwili uliokutwa umeteketea kwa moto Februari 19, 2023 ni wa Josephine Mngara (27).

Mwili wa mwanamke huyo ulikutwa umeteketea kwa moto kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika (pagale) ambapo kulikutwa pia michirizi ya damu kutoka kwenye nyumba ya mkazi wa eneo hilo.

Katika ujumbe huo aliomtumia mama mzazi wa marehemu, Theodora Msuya, mtuhumiwa anadaiwa kusema roho inamuuma kwa tukio lililofanyika. Mwanamume huyo ambaye jina limehifadhiwa ndiye alikuwa akiishi na marehemu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msuya alisema katika sms aliyotumiwa, mtuhumiwa alielezea nini kilitokea siku hiyo na kwamba alimkuta mwanamume mwingine na mkewe na ukatokea ugomvi na ametaja jina la mtu anayedai ndiye muuaji.

SMS hiyo iliyohaririwa inasomeka “Mama samahani si kosa langu, nilimkuta (anamtaja) na mke wangu kwangu, nikavunja mlango tukaanza kupigana. Mimi nikashika panga na yeye akachukua mpini wa jembe.
“Akawa anarusha nikakwepa ndo akampiga mke wangu mpaka chini. Akanipa nauli akaniambia sepa niachie mimi... Muulize (anamtaja), mama mimi sijui roho yangu inauma sana mchana mwema.”

Mama wa binti huyo, alidai kama waliotenda tukio hilo wamejitokeza na kuomba radhi, wanaliomba Jeshi la Polisi kuwapa mabaki ya mwili wa mtoto wao kwenda kuzika kwa kuwa ni muda wameweka msiba nyumbani bila kujua mwafaka. “Mpaka sasa hatujapewa mwafaka na Jeshi la Polisi juu ya kuzika na nini kinachoendelea, tumeweka msiba hapa nyumbani tuna zaidi ya wiki sasa, watu wamekaa hapa wameacha shughuli zao na familia zao wako hapa nyumbani.

Hapa nilipo nimechoka jamani, tunaomba tupewe hayo mabaki ya mwili wa mwanangu tukazike maana kwa kweli nimechoka,” alisema mama huyo.

Inadaiwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori alieleza kuwa, baada ya polisi kuchunguza walikuta michirizi ya damu kutoka nyumba jirani kuelekea eneo ambalo mwili ulikutwa.

Alisema mabaki ya mwili huo, ikiwemo mifupa na sehemu nyingine za mwili huo vimehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC kwa ajili ya taratibu nyingine za kiuchunguzi.

Februari 23, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa alisema tayari Jeshi la Polisi limechukua sampuli ya vinasaba (DNA) kwa ajili ya kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kujiridhisha kama ni mwili wa mwanamke huyo.

“Tumepeleka DNA kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili tuthibitishe ule mwili ni huo au ni mwingine, hivyo tumechukua vitu muhimu kwa mama mzazi wa huyu binti ili kujiridhisha na tukio hilo,” alisema Kamanda Maigwa.

MWANANCHI
 
Mbona kama haiingii akilini, mtu amuue mkeo/mpenzio halafu akupe nauli ukimbie kwa ahadi ya yeye kulimaliza hilo tukio. kuna mengi nyuma ya hili tukio la mauaji huu ni mwanzo tu.
Hii si kweli, halafu mlikua kwenye fighting, hahaha wakaamua kukaa chini wakaongeaz wakakubaliana kuwa ampe nauli aondoke, na yeye kapokea nauli kaondoka bila kwenda kutoa taarifa kwa MTU....
 
Hii si kweli, halafu mlikua kwenye fighting, hahaha wakaamua kukaa chini wakaongeaz wakakubaliana kuwa ampe nauli aondoke, na yeye kapokea nauli kaondoka bila kwenda kutoa taarifa kwa MTU....
Wameuungana baada ya walichokua wanagombea kufa, Sasa si wangeuungana wakati huyo Mwanamke yuko hai ili wote awahudumie kwa zamu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kabaangggg
KATAA NDOA tushaingia.

Tukiwaambia MSIOE huwa hamuelewi,
Huwa mna kauli zenu za kashfaaa sijui Wewe shoga, umelelewa na familia dhaifu na so for.

Ila mngejua Dunia ya sasa imejaa ma predators na feminism basi woteee mngeunga mkono kampeni hii ya kuokoa Waaume.

KATAA NDOA

NDOA NI KIFO.

#YNWA
 
hasira nyingi huishia hasara, Hivi hawa wanaofumania bado hawakomi kufanya fujo? Acha akaozee jela tu
Hasira za kuua zinatokana na Sheria ya Ndoa kutoa unafuu Mkubwa Kwa mgoni kuliko mwenye MKE.

Haki yoyote hukamilika panapokua na mifumo ya kumlipia kisasi aliyodhulumiwa na SIO kumbeba aliyedhulumu.
Bila Sheria inayolipa kisasi Haki haiwezi kusimama. Haki ikiwa hailingani na kosa lililotendeka Jamii inafanya Mob justice au vinginevyo. Kisasi hakiangalii kama kinamuathiri aliyekifanya au aliyefanya alimradi pawe na majuto makubwa.

Kama wezi wangekua wanaiba halafu hakuna Sheria ya kuwakamata na kuwafunga gerezani Bila shaka mauaji yangekua Mengi sana. Wahalifu wanapokamatwa kisheria na kupelekwa polisi Kisha kufungwa gerezani husababisha Jamii kuepuka kuchukua Sheria mkononi.

Hivi unaweza ukakamatwa nyumbani Kwa Mkuu Wa Majeshi Wa Venezuela au Jaji mkuu Wa Komoro au waziri mkuu Wa Madagascar ukiwa unafanya mapenzi na MKE wake halafu ubaki hai. ? Haiwezekani kabisa. Kama Kwa wakubwa haiwezekani na kamwe hawawezi kuvumilia basi Hata Kwa watu Wa chini haiwezekani.
Hata Mwanaume au Mwanamke awe Malaya vipi kamwe hapendi mume au MKE wake achukuliwe na MTU Mwingine Kisha amfumanie.
Akimfumania ni lazima patokee timbwili. Tofauti ya timbwili inatokana na Silaha aliyokuwa nayo wakati Wa kufumania . Kama ana bastola ataipiga MTU risasi na kama ana panga atakata MTU panga ,kama ni Maji ya moto atamwagiwa.

Hizi Sheria za Ndoa waliozitunga Wameweka mwanya Wa mweye nacho au mwenye uwezo au mjanja anaweza akafanya anachotaka Kwenye ndoa ya MTU alimradi tu awe na uwezo Wa kulipa fidia na wamekubaliana tu bila kujali upande Wa mwenza katika Ndoa na Ustawi na usalama Wa familia .

Sheria ya Ndoa ipitiwe upya Ili kuilinda Jamii ya Kiafrika. Wazungu walipuuza na Sasa kwao Kila kitu kimevurugika wamebaki na majumba na magari huku Jamii Yao imiwa inapukutika PAMOJA na kuwa na maisha ya Juu yaliyojaa anasa za Ulevi na mambo ya hovyo hovyo kutokana na kukosekana Kwa familia zinazofuata maadili mema KIROHO na kimwili.
 
Kabaangggg
KATAA NDOA tushaingia.

Tukiwaambia MSIOE huwa hamuelewi,
Huwa mna kauli zenu za kashfaaa sijui Wewe shoga, umelelewa na familia dhaifu na so for.

Ila mngejua Dunia ya sasa imejaa ma predators na feminism basi woteee mngeunga mkono kampeni hii ya kuokoa Waaume.

KATAA NDOA

NDOA NI KIFO.

#YNWA
Waambie wasenkeee hawa
 
Back
Top Bottom