Mtuhumiwa EPA aandaa harambee kuchangia CCM

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,737
405
*NI MARANDA, WAMWALIKA RAIS KIKWETE




MTUHUMIWA wa wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), Rajabu Maranda anadaiwa kuandaa harambee kwa ajili ya kuichangia CCM mkoani Kigoma kwa ajili ya uchaguzi mkuu, harambeee ambayo Rais Kikwete amealikwa kuwa mgeni rasmi.



Habari za kuaminika zimesema harambee hiyo itafanyika Februari 6 jijini Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Maranda, ambaye ni kada wa CCM, ndiye aliyeratibu harambee hiyo.



"Harambee kwa ajili ya kuchangia CCM mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, itafanyika Februari 6, mwaka huu, Maranda ndiye mratibu wa hili jambo na Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi," alisema mpashaji wetu wa habari hizo.



"Na kuna kamati imeundwa kwa ajili ya kufanikisha hilo... Maranda ameteuliwa kuwa katibu wakati mwenyekiti wake ni mzee Iddi Simba."


Kwa habari zaidi gonga hapa..


My take


Nadhani unefika wakati vyama vya siasa viangalie ni watu wa namna gani wanashirikiana nao kwani waswahili huwa tunaamini kuwa ukitembea na mwizi nawe pia ni mwizi tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom