Mtuhumiwa auawa kituo cha polisi

M

MegaPyne

Guest
Hii naonyesha watanzania hawamini LEGAL system ya tanzania. Walijua huyu mtuhumiwa anaweza kutolewa reja reja. Heri hata walimalizia huko huko. The same has to happen kwa mafisadi!

Mtuhumiwa auawa kituo cha polisi * Ni mtuhumiwa wa mauji ya watoto wawili
* Wananchi walivamia kituoni na kumuuaNa Gasper Andrew, SingidaWANANCHI wenye hasira wamevamia Kituo Kidogo cha Polisi cha Ilongero, Wilaya ya Singida mjini na kumpiga mtuhumiwa, Mohamed Nkindwa hadi kufa na kisha wakachoma moto kituo hicho.Tukio hilo lilitokea juzi jioni baada ya kundi la Wanakijiji kuvamia kituo cha polisi na kuwazidi nguvu askari 10 kutoka Singida Mjini na wenzao wa hapo na kuanza kumpiga mtu mmoja ambaye alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kuwalawiti hadi kufa watoto wawili.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Lawrence Tarimo, zinaeleza kuwa pomoja na juhudi za askari hao kupiga risasi hewani ili kutawanya umati wa watu waliokuwa wamezingira kituo, lakini hazikuzaa matunda.

Tarimo alisema watu hao baada ya kuwazidi nguvu polisi walivunja milango mitatu ya jengo la kituo na kumvamia mtuhumiwa huyo kwa kupiga kwa fimbo na silaha mbalimbali hadi kufa mtuhumiwa Mile Mohamed Nkindwa (20).

Alisema kundi la watu hao lilielezwa kwamba mtuhumiwa huyo hakuwa mmoja wa watu walioshiriki kubaka watoto na kwamba alipekwa kituoni hapo na baba yake mzazi baada ya kutengwa na wanakijiji wenzake lakini hawakuwasiliza.

Wanakijiji hao walidai kuwa polisi hawataweza kumfikisha mahakamani kijna huyo ndipo walipoamua kuchukua sheria mkononi na kumuua.Naye Diwani wa Kata ya Ilongero ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauli ya Wilaya Singida, Ramadhan Samwi, alisema marehemu alidaiwa kushiriki kuwabaka na kuwalawiti hadi kufa watoto wawili wenye umri wa miaka mitano na 13.Marehemu anadiwa kutenda kosa hilo Oktoba 14 mwaka huu kati ya saa 1:00 na saa 2:00 jioni na kwamba kati ya watoto hao mmoja alikuwa anasoma darasa la tatu.

Oktoba 16, mwaka huu gazeti hili liliripoti kuwa watoto wawili wamenajisiwa hadi kufa wakati wanamwagilia bustani ya mboga ya familia yao na watu wawili ambapo mmoja wao alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini wakiwa njia wananchi wenye hasira walitaka kumuua lakini wakashindwa baada ya kutokewa akari walikuwa kuwa na bunduki.Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja kituo cha polisi kuvamiwa ambapo mara ya kwanza ilitokea mkoani Kagera baada ya wananchi kuvamia kituo cha polisi na kukichoma moto, kwa madai kuwa kulikuwa na mahabusu ambaye alikamatwa kwa tuhuma za kuwa na ngozi za watu.Source: Mwananchi
 
Kwani mpinzani pekee nchi hii ni Mbowe tu?

Hata Mzee wetu marehemu Ndesamburo alikuwa muasisi wa upinzani nchi hii lakini hayakutokea haya mbona, Jibu ni kwamba aliheshimu SHERIA na taratibu za nchi yake maana upinzani siyo kuacha kuheshimu serikali iliyopo madarakani.


Mbowe aangalie alipokosea na siyo kusema anaonewa chuki, huko ni kutafuta huruma kwa watu wasiojielewa

Sheria gani amekiuka? Iweke hapa precisely siyo kkupiga ramli za kipumbavue kwa sababu tu umekaririshwa.

Hawa manyang'au wamefuata sheria? Sheria ipi inayowapa mamlaka ya kuharibu mali? Jibu bila hadhithi za kipumbavue!
 
Back
Top Bottom