Mtu wetu mh. Gosbert blandes, huna ubavu wa viumbe hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu wetu mh. Gosbert blandes, huna ubavu wa viumbe hawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Jul 13, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]
  Naam vipo, vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana:

  [/FONT]
  [FONT=&quot]CHADEMA kama Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo maana hawana jeshi, hata hivyo huweza kujenga hoja ambazo sisi CCM tunaziona ndogo na za kawaida zikawa kubwa kutoka vishimo hadi vichuguu vikubwa kila mtu akaviona na kushtuka.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]CHADEMA ni viumbe vyenye uwezo mdogo maana hawaongozi Serikali yenye chombo cha habari kama TBC, wala hawakusanyi kodi za wananchi tena ni wachache sana Bungeni hata hivyo huwasimamisha wale wachache wenye uwezo mzuri na walio mahiri katika chaguzi na wakiwa bungeni hujenga kambi yao ya upinzani mahala pagumu mjengoni kama walivyo Pelele wawezao kujitengenezea nyumba zao kwenye miamba. [/FONT]

  [FONT=&quot]CHADEMA hawana Rais lakini kama Nzige wasio na Mfalme, pamoja na malumbano ya hapa na pale, hujitahidi kwenda pamoja vikosi vikosi, wakisaidiana kutatua matatizo yao ki-Chama na kujengana kuliko sisi CCM ambao tunazidi kugawanyika na kusambaratishana wenyewe kwa sababu za maslahi binafsi na muendelezo wa makundi ya wenye-magamba, wasio-magamba na walio katikati ya hao .

  [/FONT]
  [FONT=&quot]CHADEMA kama Mijusi wanaweza kushikwa kwa mkono na kupelekwa polisi, lumande na hata kuhukumiwa chap-chap hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme na kupenyeza katika vyombo vya Usalama, Wizarani na Wavuti-zamivu (deep-web) wakapata siri kupitia top clandestine and reconnaissance gears mithili ya zile za uzao wa Juliana Paul Assange toka kwa watu waliokula viapo kutozitoa, wakaanika mwaaa! ukweli au kile kiitwacho classified information.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Naam, yuko mtu mmoja anasisimua na atavuta lukuki katika mwendo wake, naye ni Tundu Lissu. Kama simba, mwenye nguvu na kwa madaha miongoni mwa wanyama wengine wa kawaida sana kama mtu wetu Mh. Gosbert Begumisa Blandes au Mh. Murtaza Magungu [/FONT] [FONT=&quot]ambao wakati, jasiri Mh. Lissu anakiita kinyesi jina lake halisi mavi, wao wangependa ayalembe na kupoteza maana kwa lugha ndefu isiyo na tija kuwa ni chakula adhimu kipitacho utumbo mwembamba na kutokea tundu linalomalizikia na silabi ‘-ndu’.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Hili ndilo balaa linalotujongelea sisi wana CCM, ambapo Wananchi wanatuona tuna mzaha na hatuna juhudi za dhati toka moyoni kupambana na harufu mbaya ya rushwa, ukiukwaji wa taratibu za nchi tulizokubaliana, mgawanyo usio matiki wa keki ya Taifa Bungeni na uzembe makazini!
  Mwenye masikio ya kusikia na asikie neno hili ambalo Babykailama[/FONT]:A S-baby:[FONT=&quot] anawaambia wanaCCM wenzake na wote wapenda maendeleo.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Naibu Spika, Mh. Ndugai, uvaapo vazi lenye nakshi na kukaa mahala pa juu palipoinuka katika kiti cha madini ukilindwa kikatiba na ishara ya Siwa inayoashiria mamlaka, huna haja wala si kazi yako kutolea maelezo wala ku- dilute tuhuma zilizoletwa na Mbunge, wacha Wahusika (aliyetoa tuhuma au majibu ya aliyetuhumiwa) yaletwe panapostahili ukweli ujulikane. Kazi yako ni kutoa miongozo, maagizo, kuongoza majadiliano na kutangaza matokeo au adhabu husika. Jifungie maktaba na utembelee Kanuni za Kudumu za Bunge (LETU SIO LAKO), sehemu ya 5 Ibara ya 63, kama kuna mtu kasema uongo na si vinginevyo.[/FONT] [FONT=&quot]Naam, moja au yote ni dhahiri kati ya haya mawili yafuatayo:

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Ama[/FONT][FONT=&quot] baadhi ya WanaCCM ndani ya Serikali wamechoka na hali ya kutojirekebisha kwa watu tuliowapa dhamana na hivyo kuamua kwa makusudi kutoa taarifa hizo kwa Wapinzani au ni kwamba WanaChadema wametuzidi akili na ujuzi wa kutumia nafasi walizo nazo kuimba korasi za nyimbo wanazopenda Wananchi kwa kujenga hoja (ikibidi kuzikuza kwa ufundi) hadi sisi tunabaki kuonekana hafifu!

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Vyovyote ilivyo, sauti ya mwanadamu inanyamaa sasa kwa kuwakumbusha kuwa shoka limekwisha wekwa tayari kila mti usiozaa matunda mema utakatwa na kutupwa motoni 2015! [/FONT]:A S cry:
   
 2. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  A good read, in my opinion.
   
 3. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 513
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Asante kwa kuwakumbusha wana CCM wenzio. Vyovyote iwavyo uongo ujitenga na ukweli. Hata kama mzoga utapuliziwa perfume kali bado harufu yake itasikika tu! Lakini pia sikio la kufa halisikii dawa. Nawaunga mkono wapambanaji wote, wabunge na wanaharakati na raia wema walioamua kwa kauli moja kusimamia haki, raslimali na maslahi ya watanzania kwa kila nyanja. Na hili wanalifanya kwa moyo wa dhati na mapenzi mema kwa nchi yao na watu watu. Hakika sauti zao hazitapotea bure.
   
 4. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Du nimebaki mdomo wazi, JF ina Waandishi.Ok, Baby tueleze hizo top clandestine and reconnaissance gearsndio zipi hizo Baby?Tujuze tuwe pamoja.
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Vipi kamanda wetu Deusdedith Jovine yuko mzima?
   
 6. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tsunami limeingia,hoja hujibiwa kwa hoja ukiona hoja inajibiwa kwa malumbano ujue mtu huyo ama amekatwa kichwa au ana uchi wa akili.CCM utopia umekubamba mpaka wasomi
   
 7. a

  andrews JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​chadema for karagwe 2015 ccm wote ni majambazi hatuwataki m4c people's power
   
 8. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  brilliant
   
 9. R

  RC. JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  good!guy
   
 10. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  CCM tunajiuwa wenyewe kwa kuwakilishwa na watu wasiotaka kuuona ukweli na pia wasiosimamia yanayopendwa au tarajiwa na wananchi. Hatutakubal, tutabanana hadi wabovu ndio wakimbie wenyewe!
   
Loading...