Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

Muangalie fulani ana biashara nzuri, yule binti amewajengea wazazi wake nyumba, yule mliyesoma nae ana watoto wawili, kijana yule kawawekea wazazi wake mashine ya kusaga, wewe unakwama wapi? Hayo ndio maneno tunaambiana

Ha haa haaaa umenifurahisha, ila kiukweli akikwambia maneno kama hayo uliyoandika wewe hapo juu, ujue huyo kakupenda. Wengi wao watakwambia "basi wewe unagundu"
 
Kwahiyo kumbe wanaume wengi wanapooa wanakuwa hawajui thamani ya mwanamke bali wanaoa ili wake zao wakawafundishe huko huko ndoani? Aise kuna wanawake wana huruma jamani yaani wanakubali kuolewa na wanaume wasiojua thamani ya mwanamke?

Hivi ninyi wanaume mnaweza kuoa wanawake ambao hawajui thamani ya mwanaume na mkwafundisha huko huko ndoani? Siyo ninyi mnaotakaga wanawake ambao ni ready-made kitabia? Sasa mbona sisi tukitaka wanaume ambao ni ready-made kiuchumi mnatuona kama vile hatuna mapenzi ya dhati?
Oh nadhani umewahi sana kutafuta hoja ya kujitetea, lakini upande wa pili umesahau kwamba hakuna mtu asiye fanya makosa, kama mume alifanya makosa mwanzo kwa kumsaliti mkewe haimanishi kwamba ndio tiketi ya kuja kunyanyaswa na mkewa baada ya kuporomoka kiuchumi, kwasababu mtu huyu pia anaweza kubadilika, lakini kubadilika kwake si kwa kumkomoa hilo unapaswa kujua.

Alafu,ukweli ni kwamba mwanaume anapokwenda kuoa haimaanishi kwamba atataka apate mwanamke atakaye kuwa msafi asilimia mia, kwasababu hakuna mtu wa hivyo duniani, kauli ya kusema kuwa tunataka mwanamke aliye funzwa ni kwa lengo la kutaka kupumguza mapungufu lakini tunaamini bado atakuwa nayo tu kama binadamu hivyo tunajiandaa kuyavumilia, ndio maana wanasema ndoa ni kuvumiliana ( ukishindwa kujua hili basi ndoa huiwezi kamwe).
Mtu kufanya kosa la usaliti kwa mke au mume si kwamba alioa au kuolewa na mume au mke asiyajua thamani yake, hapana, ila ni katika hali ya udhaifu wa kibinadamu na hilo anaweza kutenda yeyote iwe mume au mke.
Sasa je ni njia gani sahihi ya kumrejesha katika hali yake ya kwanza ya kutambua uthamani wa mwenza wake, hapo utaona kwamba kumkomoa, kumdhihaki na kumkatisha tamaa sio njia sahihi badala yake itazidi kumjengea chuki na atakapopata uwezo tena hali itakuwa mbaya kuliko mwanzo, lakini kumbe kama ungekuwa naye karibu ingemfanya ajifunze kujirudi kwa makosa aliyo fanya, kama ni mtu mwenye akili atabadilika.
(Ila kama hauna mpango tena na huyo mtu basi kumkomoa itakuwa njia nzuri kwako)
 
Kwani hapa tunaongelea kumpanda kichwani au kumtia moyo? Mimi binafsi mume awe na pesa asiwe na pesa unyenyekevu wangu kwake uko pale pale mimi siwezi kushindana na mwanaume ila kama wakati ana pesa alikuwa hanisaidii chochote na alikuwa ananisaliti siku zikimuishia kwanini ndo anikumbuke mimi?

Wanaume bwana yaani mnahangaikaga na michepuko huko nje mnasingizia kwamba sisi wake zenu ndo tunawafanya mchepuke ila yakitokea ya kutokea hiyo michepuko yenu ikiwakimbia ndo mnajifanya kurudi kwa wake zenu wawatie moyo kwanini na kipindi mambo yakiwa magumu msiende kwa hiyo michepuko yenu mliyokuwa mnaihonga kuliko wake zenu?
mume wako anapokuwa kwenye matatizo hasa mporomoko wa kiuchumi halafu wewe hauonekani kumtia moyo wala kum console obvious lazima atakuuliza. Sasa na wewe kwa sababu ulikuwa unajiona huko manyanyasoni kipindi hajapata matatizo utajikujuta unamjibu kwa jeuri tu na hapo ndio mwanzo wa kumpanda kichwani.
 
Hahaha afu lizarazu what happened to you? Siku hizi una comments negative sana juu yetu; nakushushia gazeti lako la kutuita "old cargo"
duuhh.. hii comment yako imenifanya nijitafakari sana swahiba. halafu magazeti yako huwa nayaogopa ngoja nika edit yangu mapema kabla ujalishusha gazeti lenyewe pengine labda itasaidia kulipunguza uzito.
 
kmmmae yani balaa sana. Wanawake wa kibongo wameumbwa kuhudumiwa tu. Wakikosa huduma ni vita kali ya taarabu!
wana vikauli vyao wanakwambia "umeshindwa kuwa mwanaume, mwanaume hashindwi kuhudumia hata iwe vipi" na hapo haijalishi hata kama huko nyuma uliwahi kumnunulia Rolls Royce kabla mambo hayajaenda mlama.

Wanawake wa kibongo wana self-entitlement mentality mbaya sana.
 
Kama kuna mtu asiejua kua maisha ni safari isio tambarare namhurumia, maisha hayajawahi kua smooth hata siku moja.
Mimi binafsi nasemea upande wangu kamwe siwez muacha mwenzangu anasononeka wakat hata kumwambia tu husband worry out haya ni kama maji yatapita, utapata kama hapa umekosa usisononeke kesho huijui, na si kwamba sipitii changamoto, la hasha napitia kama zilivyo ndoa zingine lakini alhamdulillah tunahandle hivo hivo na maisha yanakwenda, kupeana moyo na matumaini ndio inavyotakiwa
Dah kiukweli uliyo yasema hapa kama ni kweli basi nimpe hongera zake huyo jamaa kwamba kapata mwanamke mwenye sifa za kuitwa mke. Lakini ukweli ni kwamba ni wanaume wengi sana wamajikuta wakikimbiwa na wake zao ama wapenzi wao kwasababu ya kuteteleka kiuchumi, mara nyingi sana wanawake wamekuwa si watu wavumilivu katika suala la ugumu wa maisha unapowakuta wenza wao. Hili la kusema maisha ni kupanda na kushuka wanao lijua ni wachache sana. Hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa ama mahusiano kwa lengo la kulelewa au kuhudumiwa na si kujenga familia, yaani familia kwao ni jambo la pili lakini kubwa kwake ni kupata huduma. Siwalaumu kwasababu ni jukumu la mume kulea familia yake lakini wanawake wanapaswa kutambua kwamba maisha hayawezi kuwa sawa siku zote. Usimdharau masikini unae muona leo huwezi jua kesho atakuwaje.
 
Oh nadhani umewahi sana kutafuta hoja ya kujitetea, lakini upande wa pili umesahau kwamba hakuna mtu asiye fanya makosa, kama mume alifanya makosa mwanzo kwa kumsaliti mkewe haimanishi kwamba ndio tiketi ya kuja kunyanyaswa na mkewa baada ya kuporomoka kiuchumi, kwasababu mtu huyu pia anaweza kubadilika, lakini kubadilika kwake si kwa kumkomoa hilo unapaswa kujua.

Alafu,ukweli ni kwamba mwanaume anapokwenda kuoa haimaanishi kwamba atataka apate mwanamke atakaye kuwa msafi asilimia mia, kwasababu hakuna mtu wa hivyo duniani, kauli ya kusema kuwa tunataka mwanamke aliye funzwa ni kwa lengo la kutaka kupumguza mapungufu lakini tunaamini bado atakuwa nayo tu kama binadamu hivyo tunajiandaa kuyavumilia, ndio maana wanasema ndoa ni kuvumiliana ( ukishindwa kujua hili basi ndoa huiwezi kamwe).
Mtu kufanya kosa la usaliti kwa mke au mume si kwamba alioa au kuolewa na mume au mke asiyajua thamani yake, hapana, ila ni katika hali ya udhaifu wa kibinadamu na hilo anaweza kutenda yeyote iwe mume au mke.
Sasa je ni njia gani sahihi ya kumrejesha katika hali yake ya kwanza ya kutambua uthamani wa mwenza wake, hapo utaona kwamba kumkomoa, kumdhihaki na kumkatisha tamaa sio njia sahihi badala yake itazidi kumjengea chuki na atakapopata uwezo tena hali itakuwa mbaya kuliko mwanzo, lakini kumbe kama ungekuwa naye karibu ingemfanya ajifunze kujirudi kwa makosa aliyo fanya, kama ni mtu mwenye akili atabadilika.
(Ila kama hauna mpango tena na huyo mtu basi kumkomoa itakuwa njia nzuri kwako)
Sasa bora wewe unajua kuwa kwenye ndoa wote mwanaume na mwanamke wanapaswa kusameheana na kuvumiliana mimi nawazungumzia wale wanaume ambao wanataka wao wakifanya makosa wake zao wawasamehe na wawavumilie

Ila wake zao wakifanya makosa wao hawataki kuwasamehe wala kuwavumilia yaani ni lazima watafute adhabu yoyote ile ya kuwapa wake zao kati ya kuwapiga, kuwasaliti, kuwaongezea wake au kuwapa talaka kabisa na aina hiyo ya wanaume ni wengi na wanadai kuwa huo ndiyo uanaume je hiyo ni sahihi?
 
duuhh.. hii comment yako imenifanya nijitafakari sana swahiba. halafu magazeti yako huwa nayaogopa ngoja nika edit yangu mapema kabla ujalishusha gazeti lenyewe pengine labda itasaidia kulipunguza uzito.
Uzuri nilishascreen shot comment yako; so uzito upo pale pale (kidding). Me nimemzoea a sweet lizarazu; all of a sudden namuona kawa bitter. Tusamehe kama tumekukosea
 
Kama kuna mtu asiejua kua maisha ni safari isio tambarare namhurumia, maisha hayajawahi kua smooth hata siku moja.
Mimi binafsi nasemea upande wangu kamwe siwez muacha mwenzangu anasononeka wakat hata kumwambia tu husband worry out haya ni kama maji yatapita, utapata kama hapa umekosa usisononeke kesho huijui, na si kwamba sipitii changamoto, la hasha napitia kama zilivyo ndoa zingine lakini alhamdulillah tunahandle hivo hivo na maisha yanakwenda, kupeana moyo na matumaini ndio inavyotakiwa
Dah, kama ni mke kweli jamaa yetu amepata aisee. Nasaha kama hizi huwezi kuzikuta kwa Slay Queen. Hongera sana kwa kutambua nini maana ya maisha...hii ni kwa mara ingine tena. Usije ukabadilika tu ukawa kama hawa wahuni wa mjini.
 
Kuna marafiki wengine wanasubiri uanguke ili wakucheke vizuri..
Nanukuu..
"Natamani siku upate shida uje uniangukie ili nikusaidie"
Kutoka kwa bestfriend eti....huwa najishangaa hadi sasa kwa nini bado tunawasiliana, ni kwa neema tu
 
"Liangalie lina kazi ya kulewa tu na pombe haitokufikisha Mahala popote " nikaamua nimpige chini niendelee na mpenzi wangu muaminifu bia and guess what npo extra miles kuliko alivyoniacha

Huwezi fananisha pombe na mambo ya ajabu
 
Hivi wewe si umesoma na john! Mbona john ana magari mawili na nyumba wewe umezubaa tu, nakwambia ukweli maisha yakiendelea hivi ntachoka
Hawa ndo wanawake tulio nao, badala ya kukutia moyo anakua ndo wa kwanza kukukebehi mambo yanapoenda kombo.
 
mume wako anapokuwa kwenye matatizo hasa mporomoko wa kiuchumi halafu wewe hauonekani kumtia moyo wala kum console obvious lazima atakuuliza. Sasa na wewe kwa sababu ulikuwa unajiona huko manyanyasoni kipindi hajapata matatizo utajikujuta unamjibu kwa jeuri tu na hapo ndio mwanzo wa kumpanda kichwani.
Sasa ndo kwanini mkipata matatizo msiende kwa hiyo hiyo michepuko yenu mliyokuwa mnaihonga kuliko wake zenu wakati hamna matatizo?
 
50 Reactions
Reply
Back
Top Bottom