Mtu wa kwanza kukutana naye kila unapotoka nyumbani kwako ndiye huashiria mafanikio ya huko uendako

kwa ambaye ameoa si mkeo ndo huwa anakuandalia kila kitu kuanzia chai nguo ya kuvaa na kukukagua kama umekaa sawa na anakuruhusu kutoka sasa huyo mwanamke mwingine wakukutana naye yupi na huku umeshaagana na mkeo :eek: au swala hili ni kwa wale ambao hawajaoa.
 
Ubongo kizibo kazi sana.... kama mentality yako ni ya nuksi na kukosa utakosa tuuu hata ukutane na Dewji asubuhi akupe na mkono.. kama mentality yako ni ya kushindwa utashindwa tu...
Argument cheap cheap so mtu akikaa eneo limezungukwa na wanawake na kila akipata kifungua kinywa anahudumiwa na wanawake yeye atakua na mikosi mambo yote afanyayo?????
Ujinga ni mzigo. Endelea tu kubadili nguo na kukemea hata visivyohitaji kukemewa.
 
Hii inafanya Nazi kuanzia nje ya nyumba yako getini unakuwa unatoka
Kwa hy mfano mimi nimebarikiwa kupata ka usafiri, halafu jirani ambaye ni mwanamke anafanya kazi karibu na ofisini kwangu na kwa bahati mbaya hajabahatika kupata usafiri, sasa ananitegemea kila asubuhi nimsaidie 'lift' kwenda job. Kama nitafuata huo ushauri maana yake wiki nzima niahirishe safari au niwe natoka nje nikimuona tu pale nje narudi ndani kubadili nguo, huo sasa si ndio uchawi?.... Halafu kila mtu ana malengo anayokuwa amejiwekea kama yanaenda sawa na ulivyo plan, kwa nn utafute hizi imani tata. Ki ukweli kama hicho kitu kingekuwa kweli basi mimi maisha yangu yangekuwa vumbi tupu. Kwa sababu kabla sijapata ki baby walker changu na mm nilikuwa ninategemea usafiri wa jirani yangu kwa miaka karibia mitatu na ni mwanamke. Kila asbh nilikuwa natoka namvizia njiani nikichelewa ananipigia honi... Ila kuna mahali kwenye biblia wameandika "Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo", kila kitu kinafanya kazi kwa imani. Ukiamini inakuwa, lkn sie wengine ukikutana nae ndio kwanza unamwambia jirani umependeza. Na mambo yanakuwa sawa.
 
Habari wana ndugu,

Katika hali fulani, naomba niwajuze jambo hill;

Unapojiandaa kwenda safarini, kwenda kazini au popote ambapo unafukuzia jambo lolote, mtu wa kwanza kukutana naye nje ya nyumba yako ndiye hutoa viashiria vya bahati nzuri au mbaya ya mafanikio yako huko uendako.

Mara nyingi unapotoka na kuanza kukutana na mtu wa kiume (jinsia ya kiume) huashiria mafanikio au bahati nzuri huko uendako na hii inadaiwa kwamba wanaume wengi kiroho hawajazungukwa na majini (pepo waharibifu).

Kwahiyo; endapo kama unafukuzia kazi, pesa, safari au ahadi yoyote unapokutana na mwanaume hutoa ishara ya asilimia kubwa kwamba jambo lako litafanikiwa huko uendako.

Pia elimu hii imeendelea kuchimba zaidi na kuonyesha kwamba endapo unapotoka nje kwenda - ukaanza kukutana na mtu mwanamke (jinsia ya kike) hapo unakuwa na asilimia ndogo sana ya kufanikiwa huko uendako (hii ni kutokana na majini wanaodaiwa kuwa wengi waharibifu hukaa kwa mwanamke)

Kwa maana hii, unapopishana na jinsia hiyo basi huko uendako mambo huwa magumu, au kama ulikuwa unakwenda sehemu hutapata ulichofuata, ama utakosa usafili, au utapata kwa shida na pengine hadi utagombana, kama ni ofisi utakuta ama imefungwa, hawapo, au misukosuko isiyo na lazima itakujia.

INASHAURIWA
Endapo ikatokea ukaanza kukutana na mwanamke basi ghairisha safari kwa mda rudi badiri chochote japo nguo halafu toka tena, au kama wewe ni mtu wa imani "punde unapokutana na mwanamke KEMEA KIMOYO MOYO NA KUYAFUTA MABAYA YOTE KWA JINA LA MUNGU. Halafu endelea na safari yako.

===============

"Matokeo huwa ni mazuri zaidi endapo ukijiwekea utaratibu wa kushiriki ibada za alfajiri/ asubuhi kila siku hutakaa ujute hata siku moja, utafanikiwa popote uendako bila vikwazo"
Ushirikina tu
 
"Matokeo huwa ni mazuri zaidi endapo ukijiwekea utaratibu wa kushiriki ibada za alfajiri/ asubuhi kila siku hutakaa ujute hata siku moja, utafanikiwa popote uendako bila vikwazo"
Hapa nakubaliana nawe 100%
 
Pia nimewahi kusikia Hili swala lina ukweli ndaniyake mi pia napo kutana na jinsia ya kike asubuhi biashara yangu huwa haiendi inakuwa ngum nilichokuwa sijui niendapo nikikutananae nifanyeje .asante mkuu
 
Jamaa mmoja humtuma mwanae wa kiume atoke alafu arudi wakutane ndo atoke, dadeki, hii kitu kwa wazee wetu ipo sana, ata dingi akitaka kwenda safar ya kutafuta hunituma kwanza nirudi nikutane naye kwanza ndo aende
 
Yap ni mipango mizuri hata wanawake wanalijua hilo, huwa wanaomba wakutane na mwanaume ili iwe bahati
 
ni kweki kabisaa na inashauriwa ukikutana na mwanke rudi ndani lambachumvi kidogo kisha endelea na safari

Jambo hili limetoka kuzimu kabisa. Haya ni makufuru ambayo hayafai kuendeleza. Urudi ndani ukalambe chumvi. Haya ukitoka nje tena, huyu mwanamke mwingine urudi ukalambe chumvi, ukitoka huyu tena mwingine. Kibobo cha chumvi si kitaisha kwa kulamba tu?
Mwanamke hakuumbwa kwa udongo bali ni nyama na mfupa wa mwanamume. Hishima hii ya Mnyaazi Mungu mnaidhalilisha?? Kwa nini muwaze vibaya hivyo? Hivi una mke kweli?? Sijui huyu wangu wa moyo kaniwekea limbwata! Mbona simuwaziagi mabaya kihivyo?? Tuwapende wake/wanawake wala hakutakuwa na tatizo. Majini humkaa yeyote bila kujali jinsia.
 
hapana unalamba mara 1tu yatosha kwa kutwa nzimaaaa! HATA HIVYO NI KWA MTU WA KWANZA KUKUTANA NAE NA SI VINGINEVYO
 
Back
Top Bottom